Baada ya kumdhalilisha mumewe, Joyce Kiria asema hataki ushauri kutoka kwa mtu yoyote

Baada ya kumdhalilisha mumewe, Joyce Kiria asema hataki ushauri kutoka kwa mtu yoyote

Huyo mdada ni punguani mbona wakati kamanda analipa hzo bills hakua anakuja kutangaza kwenye mitandao, ktu wasichokijua wanawake ni kwamba kuna siku mmeo ataishiwa na hiko ndo kipimo cha upendo.. Sasa kuja kumuanika kwenye mitandao ndo nin, akina dada wa sku hz sjui akili zao zipo wapi,


Wakat nakua nakumbuka mdingi aliyumba almost 2 years bi mkubwa anaamka saa 11 anachoma maandazi, saa 2 anachoma chapati naomba hela ya shule napewa na bi mkubwa, for 2 years, lakin hawa wa sasa hv ukikosa hela week tu utatombewa had na wauza karanga za sh. 50.
hahahaa mpka wauza Katanga mkuu

hatari mnooo
 
Baada ya Kupost Video yake Kwenye mtandao wa Kijamii Instagram , kulalamika anapigwa na mumewe wakati yeye Ndio anasimamia kila kitu ndani ya nyumba mpaka kodi ya nyumba wanayoishi analipa yeye.

Wadau mbalimbali waliotoa mtazamo wao kwa alichokifanya Ila mwanaharakati huyu wa wanawake alisema Hataki ushaur wa namna yoyote ile.

Nb
**Kama hawa Ndio mfano wa aina ya wanaharakati tulionao wanawake, Basi wanawake tunasafari ndefu Sana.

View attachment 681349
Haya in matokeo ya vyuma kukaza.

Zamani maisha yalikuwa safi sababu mlizoea kuishi kiujanjaujanja.

Maisha ya kunyoosha mstari

Shame on you Kiria, kitakachofuatia hapo ni kuingia kujiuza
 
mara nyingi usimwamini mwanamke anapokwenda mbele ya watu nakusema mambo ya ndani ya maisha yao si mwanamke mzuri halafu wanawake kama joyce utaishi nae kwa raha na utampa kila kitu lakini pindi akipata bwana mwingine akampenda basi ukimgusa tu atatafuta sababu akuaibishe mbele ya umma atasahau yote uliyomfanyia na atakuzushia mambo mengi yalinikuta haya mke wangu wa ndoa nilikuwa nampa kila kitu mpaka gari la kifahari 4x4 anaenda nayo offisini lakini ni bure leo hanijui
 
Kesi za ndoa usihukumu kabla hujasikia pande zote mbili.
Muwamba ngoma......
Lkn family issues kuzianika kwenye media ndiyo tatzo pekee lenye kutoa taswira ya ndoa yao ilivyo.
 
tiku wewe siyo binaadam ni malaika kwa kweli


kwa wale wanaume ambao huwa wanahudumia familia watashangaa, na wanawake wanao hudumiwa watashangaaa ila liko kundi kubwa la joyce kama mimi hapa, nimehangaika na mwanaume namlisha namvika yani kilakitu mimi, badae nikaona kama labda kipato chake kidogo hawezi kunihudumia nikampeleka shule amesoma kozi nzuri ya afya ambayo anaweza kufanya kazi hata private nimelipa ada miaka 3 nimeishi kwa kujibana sana na mwanangu kila mwezi namtumia matumizi na ada maana alisoma private chaajabu amemaliza chuo hataki kufanya kazi anataka niendelee kumlisha cha kushangaza niliuza kiwanja ili kusapot mambo ya ada na matumizi akiwa mwaka wamwisho yule mnunuaji akatoa hela nikamtumia ametumia zimeisha na shule kamaliza kuja waandikishane akakataa eti hiyo hela hajafanyia kitu hajanunua viatu, suti, na vitu vizuri sasa ili kuondoa lawama nikaenda vikoba nikakopa hela milioni moja nikampatia ndo akaandikishana ,hapo hakunipa hata senti moja na zimeisha yani nina hasira kuliko za joyce niko najipanga kumfungulia mashtaka ya kudai talaka simtaki, kibaya zaidi muhuni , mchoyo, muongo, mwizi. akikuta cmu hapo anapitia, hela anapitia afu mlokole anajiita mtumishi wa bawana , unashangaa hata akipata kidogo utasikia tu ah fulan alinisaidiaga alinipa hela kiasi fulan lkn mimi hajawahi nipa sioni umuhimu wake nimeona nipige chini. humu jamii forum niliwahi kuomba ushauri kipindi cha nyuma hakuna hata alonijibu vya maana
 
Uyu si ndo anawasemeaga wanawake wenzake imekuaje nayeye tena.ataje sababu yakweli zayeye kupigwa sio kukimbilia kutafuta huruma kwa watu maana inawezekana yeye ndo mwenye matatizo,maana mwanamke mwenye akili kamwe hawez kuanika mambo yake na nyumba yake hadharani.Alafu wanawake wanataka 50/50 sasa kwanin alalamike kulipa bills.Kazi tunayo wanaume.
 
Huyu joisi hajasema alimtamkia nini mume wake mpaka akaamua kumfundisha adabu! Aseme alifanya nini mpaka kupigwa? Sio unaleta abali za kupigwa na kugalimia família unaacha chanzo!,sababu ya kupigwa umeificha. Sio ajabu alimtusi mume, au ashaanza kugegedwa uko nje. Labda niwaeleze wadada mnaosimamia familia kwa faida yenu. Wanaume mnaowaghalamia ni Atari kuliko wanaowagharamia. Wanaitaji kueshimiwa zaidi, kwani unapomkosea anahisi ni kugharamia sababu ya wewe kumdharau!!. So kuweni mákini zaidi. Usijedhani mume anajali au kuesabu gharama unazoingia katika swala la kumuheshimu! Unadhani mume wa kilia kwa pato lake angepanga jumba iloo? Huyu mdada mwambieni ajenge sio kupanga nyumba za gharama, ukihisi kubanana unatoa shobo, lazima upigwe tu. Amna jinsi. Uwe na adabu kwa mume.
 
.kumbe mwanaharakati na mtetezi wa wanawake anapigwa na mumewe?
Wengi huwa wanahubiri yaliyowashinda wao wenyewe. Wale kinamama wengi waliopo TAMWA etc ni masingle moms. Haya mambo magumu.
 
tutaaminije kama kileo hatoi hata senti ndani ya nyumba? au anatoa kidogo tofauti na mkewe anavyotaka kulingana na hali yake ya kiuchumi? lazima tusikie upande wa pili ili tuweze kujaji.hata hivyo anakosea masuala ya ndani kuyaanika nje kwa faida ya nani?
 
Jamani tunapowapiga wanawake na tuwapige kwa akili. Huyu kipigo kilimzidi hivyo ubongo umepararaizi maana si kwa miropoko hiyo.
 
Binafsi sijawahi kumkubali Joyce Kiria kiviile japo ana mambo ambayo huwa anafanya yana positive impact kwa jamii ila kuna mahali huwa anajichanganya sana hadi mtu unajiuliza huyu mama vipi?!

Jana kapewa kichapo kitakatifu na mume wake, yule jamaa handsome sana nadhani yule mwanamke alimpush to the limit.

Anadai eti yeye mwanamke ndo analipa bills zote za familia hadi kodi ya nyumba. Sasa nimetafakari japo mimi huwa sijali mambo ya watu, huyu mwanamke anaishi nyumba ya kupanga Mbezi Beach tena ghorofa(Mimi nilidhani nyumba yao)

Anaishi maisha ya juu sana, je hasara kwa nani? Acha alipishwe mwenyewe hizo bills.

Na nyie wanaume unaishije nyumbani hata sabuni hununui jamani? Kweli? Acheni hizo makamanda!

Ndo maana mimi sipendi wanaume wa CHADEMA bora wazee wa Lumumba buku saba daily sio mbaya.

VIdeo akimchamba mume asiyelipa hata kodi ya nyumba


Duh.... Mi ndio maana naona ni Bora tuachane hadi nipate mkwanja
 
Mwanaume habadilishwi kwa malalamiko ya mitandaon yeye Kama anaona Maisha yameshabadilika angeomba talaka baada ya hapo yeye Kama mwanaharakati angetoa Hiyo video ya blah blah zake kuwashaur wanawake wasikae Kwenye ndoa za mateso wafanye maamuzi magumu .

Hivi kila mwanamke akiaza kujirecord nakutupia matatizo yake na mume wake kwenye mitandao si patakuwa hapatoshi.
Uko sahihi kabisa mkuu, yaani pale ameongeza tatizo na sio kutatua, kutoa siri za mwanaume unayelala nae kitanda kimoja mkiwa watupu ni kujidharirisha na wewe mwenyewe

Moja kati ya sifa za mke bora ni kubeba mapungufu ya mumeo, kumsitiri na kumsaidia afikie malengo. Kama unaona hupati ulichokitarajia, unasepa tu kistaarabu sio kujianika mtandaoni kutafuta huruma kwa jamii
 
Back
Top Bottom