Baada ya kumsafirisha mke najisikia amani, furaha na wepesi wa kutosha. Ndoa inahitaji umakini usiomithilika

Baada ya kumsafirisha mke najisikia amani, furaha na wepesi wa kutosha. Ndoa inahitaji umakini usiomithilika

Wewe umeoa gube gube. Huyo hata umuweke kwao miaka 10 hatoacha tabia yake.

Usitarajie mabadiliko yeyote toka kwao maana huko ndio chimbuko la tabia zake mbovu. Cha zaidi tarajia kuongezeka kwa tabia mbaya akirudi maana sasa yupo mafunzoni.
😳😳😳 mkuu unanitisha
 
Kama ana tabia ya kukwapua vijichenji vyako sidhani kama atakuja kuacha, hiyo ndio tabia yake inaonekana halafu anaonekana ni mtu ambae hana malezi bora kabisa, itachukua miaka mingi sana mpaka aje abadilike.
Oh, sasa nifanyaje mkuu?!!
 
Wanawake wana mambo sana, kuna siku kwenye daladala mama mmoja akapiga simu alikuwa anaongea na house girl nadhani, akamuuliza baba kakupata sh ngapi ya matumizi....akaendelea basi sawa tumia elfu saba tu hyo elfu tatu weka pale tunapowekaga. Nilichoka na kuchoka mke anashirikiana na house girl kula ganchi kwa mumewe.
Aisee!!!!
Sijui tumewakosea nini....
 
Unaongea kama vile jambo rahisi rahisi tu kambadili tabia mtu mzima.
Hapo hata aweke msimamo vipi hayo matusi ni tabia ipo kwenye ubongo na damu.
AmiIdisha msimamo wata achana tu.
hivi kweli watoto watatoa matusi kama utakuwa mkali wa kutosha? Au ndiyo akina nyinyi munaogopa watoto?

Tabia yo yote mtu anaweza kubadili pale anapokubali, labda kama kuna issues nyingine ambazo zimejificha.
 
Umuofia kwenu!!

Kama mada ilivyo, nimempeleka kwanza kwao kwa muda usiopungua miezi miwili.....akajifunze kitu (kama ni mwenye kujifunza). Siku moja tu baada ya kutoka kwake;

1. Leo kwa mara ya kwanza, katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu, nimefanikiwa kutulia nyumbani saa mbili usiku na kuangalia taarifa ya habari mwanzo mwisho. Kabla, ilikuwa sikai maana nikibadilisha channel tu na kuweka kituo changu pendwa cha Star TV kuangalia taarifa basi manung'uniko yenye kukera huanza kukimbizana kutoka nje ya kinywa chake.

"Tutaacha vp kubadilishiwa channel wakati TV sio yetu na hata bei yake hatuijui..."

"Hata kuzima we zima tu, nini kubalisha channel" Dah

2. Nimepumzika kushuhudia mabegi na makwapa ya mke wangu yakionwa na watoto muda wote awapo nyumbani. Jitihada za kumrekebisha ili aendane na desturi yangu, daima huenda sambamba na ugomvi.

3. Nimepumzika kuona sura ya kununanuna pale ninapotoa maelekezo.

4. Udokozi wa vielfu tano tano vyangu katika tigopesa yangu utakoma kwa muda.

5. Nitapumzika kusikia matusi kama 'nyoko we' n.k yanayotolewa kwa watoto kila siku.

6. Nitafurahia vichenji vinavyobaki katika matumizi madogomadogo na kuziweka mezani. Kwa kawaida hivi hutoweka dakika moja tu baaada ya kuviweka, hata kama akiwa amelala basi huamka ghafla na kuvichukua kisha kulala tena.

Mbona nina furaha sana sasa?!!! Atarudi kweli? Arudi ili nije kupata stress tena?

Ndoa..........mh!
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Acha pesa kidogo kwenye suluari Kama elfu 20 hivi.

Jifanye huna habari nazo kabisa.
Usiwe siriaz stori zako ziwe za furaha furaha tu.

Hapo utapata habari za nguo kufuliwa vizuri na kupigwa pasi iliyonyooka sana.
Itasaidia kuacha tabia?!!!
 
Pole kwa hiyo changamoto.

Ingawa kwa mtazamo wangu nahisi ni tabia ambazo zinaweza kurekebishika.

Binafsi nashukuru wangu hana hiyo tabia ya udokozi.

Yaani huwa naacha hela makusudi kwenye mifuko hivyo vi elfu 14 ama 8 lakini utavikuta vyote

Ishu ya TV nunua nyingine ya pili then kila mmoja awe na room ya kubadili channel apendavyo.

Kukalisha andiko langu, nimebaini ni kama huyo mwenzako umemchoka.

Wanasema ukimchoka mtu utamtafutia visababu ila mradi usiweze kuishi naye.
 
Bado mna utoto.Mmeoana mwaka mmoja tu ndiyo unaweweseka?Mkwe bado haujakua.
Si utoto na wala si mwaka mmoja, hicho kipindi ni tangu pale nilipoamua kuzikabili changamoto kwa kukaa mbali. Ndo maana nikasema nina mwaka na nusu sijaangalia TV kwa ukamilifu.
 
Katika vitu nimejiandaa kuingia navyo kwenye mahusiano ni kumiliki uchumi wangu binafsi wa kifedha.
Nitazinguana na mwenzi wangu kwa issue nyingine sio za kifedha, Inshort mwenyewe najimudu. Hizo zake ni km za ziada.
Mwanamke anayesachi pesa kwenye suruali ya mumewe namshauri atoke maghetoni.
Aende zake kabisa😃
 
Back
Top Bottom