Baada ya kumsafirisha mke najisikia amani, furaha na wepesi wa kutosha. Ndoa inahitaji umakini usiomithilika

Baada ya kumsafirisha mke najisikia amani, furaha na wepesi wa kutosha. Ndoa inahitaji umakini usiomithilika

Basi atulie asilalamike. Nimemfungua tu mawazo inawezekana uwezo wa kununua Tv mbili anao lkn hakuwahi kufikiria hilo.

Inawezekana ni kati ya wale wababa wabinafsi ambao akiwepo nyumbani wengine hawaangalii TV ni yeye tu anajipendelea.

ni sawa mke ana mdomo lakini ukute anaongea kitu cha kweli.
Ndoa ni biashara ya mwanamke. Ununue TV mbili kwasabb ya mwanamke😁😁😁
 
Umuofia kwenu!!

Kama mada ilivyo, nimempeleka kwanza kwao kwa muda usiopungua miezi miwili.....akajifunze kitu (kama ni mwenye kujifunza). Siku moja tu baada ya kutoka kwake;........

1. Leo kwa mara ya kwanza, katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu, nimefanikiwa kutulia nyumbani saa mbili usiku na kuangalia taarifa ya habari mwanzo mwisho. Kabla, ilikuwa sikai maana nikibadilisha channel tu na kuweka kituo changu pendwa cha StarTv kuangalia taarifa basi manung'uniko yenye kukera huanza kukimbizana kutoka nje ya kinywa chake.......
"Tutaacha vp kubadilishiwa channel wakati TV sio yetu na hata bei yake hatuijui..."
"Hata kuzima we zima tu, nini kubalisha channel" Dah

2. Nimepumzika kushuhudia mabegi na makwapa ya mke wangu yakionwa na watoto muda wote awapo nyumbani. Jitihada za kumrekebisha ili aendane na desturi yangu, daima huenda sambamba na ugomvi....

3. Nimepumzika kuona sura ya kununanuna pale ninapotoa maelekezo....

4. Udokozi wa vielfu tano tano vyangu katika tigopesa yangu utakoma kwa muda....

5. Nitapumzika kusikia matusi kama 'nyoko we' n.k yanayotolewa kwa watoto kila siku....

6. Nitafurahia vichenji vinavyobaki katika matumizi madogomadogo na kuziweka mezani. Kwa kawaida hivi hutoweka dakika moja tu baaada ya kuviweka.....hata kama akiwa amelala basi huamka ghafla na kuvichukua kisha kulala tena.

Mbona nina furaha sana sasa?!!! Atarudi kweli?!!!!! Arudi ili nije kupata stress tena?!!!!!!!

Ndoa..........mh!
Aseee! Ukweli mtupu. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Muwe mnatupa likizo kama huyo mwenzenu alivyofanya jamani. Ni muhimu sana
Huyo jamaa ni immature tu. Likizo kwenye ndoa means mnaenda wote as in vacation, more likely inatakiwa iwe kama fungate, mnaenda mnapumzika pamoja na kuyaongea yale ambayo yanawakwaza kwa utaratibu na kuona whats a way forward ili ndoa isiwe chungu to both of you. Sasa mmoja kati yao akienda kwao inasaidia nini..? Utoto tu
 
Huyo jamaa ni immature tu. Likizo kwenye ndoa means mnaenda wote as in vacation, more likely inatakiwa iwe kama fungate, mnaenda mnapumzika pamoja na kuyaongea yale ambayo yanawakwaza kwa utaratibu na kuona whats a way forward ili ndoa isiwe chungu to both of you. Sasa mmoja kati yao akienda kwao inasaidia nini..? Utoto tu
Ukimpeleka kwao iwe umemuacha moja kwa moja na sio utegemee arudi amejirekebisha.
 
Back
Top Bottom