Baada ya kumsikiliza Rais Magufuli, nasema wazi asante sana Jakaya Kikwete

Kabla ya kumuita jakaya kikwete mzalendo..jiulize ni Mali kiasi gani kajimilikisha ukianzia na mgodi wa dhahabu uliopo wilaya ya chunya mkoani mbeya.

Sasa nimeamini tatizo kuu ni Watanzania wenyewe,kuanzia wasomi wetu mpaka wasio wasomi itatuchukua karne nyingi kuendelea,wacha tuwe hivi tulivyo
 
Maskini Tanzania yangu
 
Kikwete hajatuletea JPM. Amemponyoka tu. Hata yeye anaisoma. JPM ni mpango wa Mungu.
 
Hivi ww uonavyo Magufuli ni mzalendo. Kuhutubia kwa kudanganya ndio uzalendo??? Kuua raia wako ndio uzalendo?? Kuua demokrasia ndio uzalendo. Ebu acha hizo Magufuli anafanya watanzania wote ni wapumbafu. Watanzania wote sio wajinga labda hao baadhi yenu na ccm yenu
 
Umeongea vizuri sana kuhusu Magufuli,ila unaposema Kikwete ni mzalendo kwa kuwa alikubali Magufuli awe Rais,unakuwa umekosa insight.
Ukweli ni kwamba hali ya Chama wakati ule ililuwa tete sana.Waliona njia pekee ya kuiokoa CCM ni kumleta mtu ambaye atakubalika na Watanzania walio wengi,na huyu hakuwa mwingine,isipokuwa Comrade Magufuli,na ndio maana uliona alijinadi yeye kama yeye,that was on purpose, sio bahati mbaya.Angenadi chama lingekuwa janga.
Magufuli hakuchaguliwa kuwa mgombea wa CCM kwa kuwa CCM walimpenda mkuu,no, infact he was a thorn even to the CCM status quo!It was a choice out of desperation.Without Magufuli may be CCM would be an opposition party today!Kwa hiyo si kweli kwamba Kikwete ni mzalendo,motive ilikuwa kukiokoa chama ambacho kilikuwa kinazama,sio uzalendo.
 
NA KAKTIKA KIPINDI CHAKE CHA MIAKA KUMI YA URAIS HAKUWAHI KUPIGA PESA INAYOFIKIA 1.5 TRILIONI KAMA ILIYOPIGWA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MIWILI YA JIWE
 
Upo udhaifu wa hapa na pale katika utendaji wake lakini kwa kiasi kikubwa ukimtazama usoni unaona kuwa kile anachokiongea kinatoka moyoni.

Ananifurahisha ile tabia yake ya kufikiria nje ya boksi. Anakuwa na originality kwa kila anachokifanya, hataki kufanana na mwingine, ni kiburi fulani hivi ambacho wakati mwingine kinamsaidia.
 
Raisi anayedirik kulala na mafail kitandani dunian hakuna zaidi ya huyu magufuli.
Tumpe honger san kikwete
 
Tanzania tumewahi kupata raisi mmoja tu! Wengine wote ni porojo tu na ujuaji mwingi mwisho wasiku wanakuja kutuingiza kwenye shida. Taifa bila katiba ya kueleweka bado ni bure kabisa hata ujenge mnara hadi mbinguni.
Hivi hiyo katiba ndo dubwasha gani? Hivi sheria zikiwepo na hakuna anayezifuata zitakuwa na maana?
Kwa nchi hii ilipofikia hatuhitaji katiba mpya tunahitaji viongozi wenye fikra chanya na utekelezaji wa mikakati kwa maendeleo endelevu ya Tanzania
 
Mnaonaje tukimfanya Mtakatifu ?
 
Ukiniuliza marais watatu angalau-angalau Magu siwezi kumtaja. Niambieni mnabonyeza ngapi kuona hayo mnayonena. Mimi bado
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…