Baada ya kumwambia mume wangu haniridhishi, kasitisha kufanya tendo la ndoa na mimi kabisa

Hongera sana kwa kuwa na uthubutu wa kulisema hili, inaonyesha unampenda sana mumeo na pia unajiheshimu, kiukweli njia ya kubembeleza inamatokeo ya kuchelewa sana na hasa ukizingatia yeye ndiye amekosea kwa uelewa wangu, maana in first place yeye anachat sms zisizo na adabu simply anachepuka huku majukumu yake hayatimizi, alitakiwa aje yeye kabla yako kusema "mke wangu nashindwa kufanya 1,2,3 kisa hichi ama napambana kuweka sawa na namna gani umsaidie" ila yeye hajali kuhusu ww anachepuka tuu. Wewe kusema ukweli ndiyo asuse? Si sawa kwasababu hasira zako kaleta yeye na yeye angekua mwaminifu na kutekeleza wajibu usingesema. By the way hujataka kikubwa ila avuke tuu toka kamoja, hajui kama kamoja hakatoshi na kama anajua kafanyaje na kama kafanya kitu kubadili hilo kamwambia nani kama si wewe?
 
Sijaelewa kwanini kwenye huu Uzi watu wengi wanamlaumu mleta mada wakati tatizo limeanzia kwa mwanaume.

Kukosa huo uwezo wa kumridhisha sio tatizo shida ni huyo mwanaume kuwa anatoka nje tena bila heshima. Kwamba mwanamke ndo Hana hisia hata asimuulize au ndo asiwe na panic button jamani. We dada hongera sana kwa uvumilivu endelea kuvumilia maana wanasema ndoa inahitaji uvumilivu
 
Mkuu vip
 
Hana tofauti na jamaa angu
 
Ushauri wangu:
Kama umeshamuomba msamaha na hajaelewa (and if not its ok) huna chakupoteza mpaka hapo anakusaliti tuu.
Mpotezee,onyesha hutaki chochotee toka kwake na pia upo biz na yako kipindi hicho mambo yote hapo ndani unatimiza ikiwa pamoja na kumuheshimu na kumfanyia stahiki zake, sisi wanaume tuna wivu sana ataanza kupata shida mwenyewee na kutafuta suluhu.
ZINGATIA; Kua mjasiri na muaminifu sana kipindi hichi,ukionja nje ndoa bye bye maana ukitakacho utakikuta nje.
 
Ushapoteza mume tayar, hiyo kauli hakuna mwanaume anaweza kuivumilia hadi anaingia kaburini...
Ni sawa yeye angekuambia unanuka uchi wakat wa kusex... Just imagine ungejisikiaje hata kama ni uongo...? Kuna kauli ikitoka imetoka hata uombewe msamaha na Yesu kamwe mtu hatakusamehe... Kwa mwanaume kumwambia hvyo ni dharau ya hali ya juu, na nikweli hatakuja kamwe kupata hisia za sex na wew, hata umfanyaje mkishaanza sex hiyo kauli inamuijia akili na network zinakata... PAMOJA NA UPUUZI WAKE HUKUPASWA KUMTAMKIA HAYO...
Wanawake kuna mambo madogo madogo mnafeli, ukweli ni kwamba Wanaume nje ya ndoa zao wanapiga show babu kubwa kiwango cha lami, tatzo wakirud ndani mke analeta mapenz na sex za kisabato (somo pana hili tutaelekezana next time)
 

Wew sio mwanamke acha Kudanganya
 
Kitu ambacho wanawake wengi tunafeli ni kuja juu, wanawake tunaongea sana jamani..... Ukigombana na mume wako au ukimfumania muite ongea nae vzuri kwa upendo atakuelewa lkn ukianzaa ooh ww usimamishi sijui nn tatizo litazaa tatizo.

Sis wanawake tunaweza kutosheka na mwanaume mmja lkn wanaume awawez kutosheka na mwanamke mmja kila siku atataka abadilishe apate mpya

Kitu tunatakiwa kufanya ni kuwahimiza wanaume zetu kutembea na condom hilo ni muhimu zaid
 
Hahaa... Hana lolote lile kapata kichaka cha kujificha

Ulikuwa sahihi kumueleza bayana, ukweli unauma ila ndio njia pekee ya kutatua tatizo.
 
Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, lakini mpumbavu huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe...

Methali 14: 1

Ushauri wangu ni muombe msamaha, fanya ibada...omba toba MUNGU akupe kibali na hekima kwa mumeo...
 
Ndoa ni kulea watoto sio kuridhishana nani kawakaririsheni kuridhishana.kama ukufanya ngono shuleni au chuoni tulia kubali tu uliruka stage imepita.
Jifunzeni furaha yenu isikamilishwe toka kwa mtu mwingine, itengeneze furaha yako toka ndani yako na sio nje yako.
 
Umbea ulikuponza mwanamae....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…