Baada ya kupaona nyumbani kwa marehemu Mafuru, sina budi kusema bado nina safari ndefu sana ya kutafuta pesa

Utajiri na mafanikio ni mfumo wa maisha na sio wingi wa mali.

Kuwa na familia imara, makazi mazuri, usafiri wa uhakika, miradi miwili mitatu, kuwa sehemu ya watawala na wafanya maamuzi zaidi ya yote kuwa na afya njema.

Usisahau kujiburudisha wewe, familia yako na marafiki. Tenga kipindi cha mapumziko na kula bata.

Hayo ndio mafanikio na utajiri.

Tofauti na hapo utakuwa na maisha ya mahangaiko daily japo una mali nyiingi.
 
Nipo msibani kwa marehemu bunju A karibu na mianzini. Hakuna anayelia hata mmoja sijui kwann?
Umeachiwa bangalow ndani ya heka 1 unalia ili iweje? Bado kuna bunda refu liko CRDB na EQUITY BANK hapo mama hana presha kabisa. Tunalia misibani wale ambao hatujajipata sababu mzigo wa ada na kodi ni mwiba mchungu sana kwa afya ya akili.
 
Bila shaka hata wakati wa Mazishi yake hawatasahau pia Kumzika Kaburini pamoja na hiyo Nyumba yake ya Kifahari ili tukiwa Mbinguni Siku ya Hukumu kwa yale mabaya tuliyoyafanya hapa duniani basi aamkie katika hiyo Nyumba kuja Uwanja Maalum wa kuhesabiwa Dhambi zako na Kuhukumiwa.
 
Umeachiwa bangalow ndani ya heka 1 unalia ili iweje? Bado kuna bunda refu liko CRDB na EQUITY BANK hapo mama hana presha kabisa. Tunalia misibani wale ambao hatujajipata sababu mzigo wa ada na kodi ni mwiba mchungu sana kwa afya ya akili.
Huko bank waweza kuta hakuna kitu au itategemea aina ya ugonjwa aliougua kama alikuwa anagharamiwa na serikali hapo akaunti zitasalimika
 
Sawa baba jenga mahekalu.
 
Ufahari wa duniani tu dogo wekeza pia na mbinguni amkako hakuna mchwanna kutu
 
Mkuu we kumbe uliya note hayo yote, sisi majirani ilikuwa ni neema ya misosi mwanzo mwisho yaani majumbani kulikiwa hamna haja ya kupika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…