Baada ya kupoteza kazi iliyokuwa inanipa heshima mjini pia nimepoteza na marafiki zangu wote

Baada ya kupoteza kazi iliyokuwa inanipa heshima mjini pia nimepoteza na marafiki zangu wote

Unajuwa, hatukujileta wenyewe hapa duniani, Mungu ndiye aliyetuleta, na alituleta hapa duniani kwa makusudi maalumu (asiyeamini hili namuonea huruma sana).

Kwa hakika kila leo yako, Mungu alishaijuwa kitambo. Kwa kuwa Mungu ni pendo, humpenda kila mtu, na ndio maana alimleta duniani, basi, jambo lolote linalotokea kwako, amini ni mapenzi yake.

Pengine anataka kukupa majukumu mengine, na kwamba usingeweza kuyafikia majukumu hayo bila kuacha hayo uliyokuwa nayo, hivyo, yawezekana ni kipindi cha mpito (transition period) kuelekea huko.

Tumepewa mamlaka makubwa sana na Mwenyezi Mungu (labda kushinda viumbe wengine wote), ya kuwasiliana na Mungu wetu wakati wowote (nasikitika wengine hili hawalijuwi). Basi, upatapo muda mzuri (faragha), omba na kusali huku ukimwomba Mungu akuonyeshe lililo mbele yako, maana uwezo huo ametupatia.
 
Mimi siamini katika marafiki kabisa. Nimeshawahi kuwa na marafiki watatu kwenye maisha yangu, wote wakaniangusha at the end. Naamini katika kuishi vizuri na watu (Iwe majirani, coworkers, kanisani na popote pale nitakapochangamana na watu), siamini katika urafiki ule wanaita wa kushibana, ni kujibebesha unnecessary mzigo.
 
Sijajua nini kilikusababishia upoteze kazi,nashangaa sana umepata akili timamu kwa kuchelewa sana namaanisha baada ya kufyekwa
 
Yote kwa yote hili ni funzo kwa sisi wengine japo bana ikiwa hayajakukuta hizi zote unaeza ona ni porojo na kuona mwenzio hakuwa na maono ya kuwaza mbele na hata kujua ni rafiki gani afaaye.
 
Mi huwa nawashangaa sana watu mnaoendekeza habari za marafiki then mnakuja kuwalaumu. Kwani huwezi fanya mambo yako mwenyewe?

Kama kazi ndiyo ilifanya muwe karibu kipi cha ajabu wakiondoka baada ya kazi kuisha?

Ukiona mtu analalamika kukimbiwa na marafiki ujue huyo ni mtu wa pombe. Marafiki wa kukutana baa kuzungusha raundi mtu ndio anaona hao ni marafiki. Anasahau kila anaezungusha raundi anafanya hivyo akijua kabisa wenzie nao watazungusha. Sasa wenzio wakishajua umefukuzwa kazi lazima wakukimbie maana wanajua kabisa utawatia hasara na uwezo wa kupiga raundi huna.
 
Mbona kawaida tu hiyo man...mtu ambae hajui maisha ndo atakuona wewe ni mzembe. Sasaiv utaona true colors of people
 
Very true
Ninachofanya ni kuangalia movies kama sina ishu ya kufanya kabisa.
Mimi siamini katika marafiki kabisa. Nimeshawahi kuwa na marafiki watatu kwenye maisha yangu, wote wakaniangusha at the end. Naamini katika kuishi vizuri na watu (Iwe majirani, coworkers, kanisani na popote pale nitakapochangamana na watu), siamini katika urafiki ule wanaita wa kushibana, ni kujibebesha unnecessary mzigo.
 
Let them go jipange upya
JamiiForums45981748.jpg
 
Mkuu ulikuwa unapata pesa u akunywa na kula na marafiki tu bila kuwekeza?
Kama bado uko nyumba ya kupanga na una mke na watoto nakushauri,waambie waende kwa wazazi wako/wake ili ujipange upya.
La sivyo utadata na mkeo ataliwa na bodaboda au wauze genge/urembo kiulani.
Mwisho tueleze qualifications zako huenda ukapata mchongo mpya.
Kila la heri!
Hahah 😂😂kwani akienda kwao au nyumbani kwa mwanaume ndio hawezi kuliwa?!! Hapa kwenye kuliwa inategemea ni mwanamke wa aina gani. Jamaa apambane na amuombe mwenyezi mungu kwan kufukuzwa kazi sio mwisho wake inawezekana ikawa ndio njia ya yeye kwenda kwenye maisha bora zaidi, mwenyezi mungu ndiye ajuaje hatma ya mja wake
 
Back
Top Bottom