Unajuwa, hatukujileta wenyewe hapa duniani, Mungu ndiye aliyetuleta, na alituleta hapa duniani kwa makusudi maalumu (asiyeamini hili namuonea huruma sana).
Kwa hakika kila leo yako, Mungu alishaijuwa kitambo. Kwa kuwa Mungu ni pendo, humpenda kila mtu, na ndio maana alimleta duniani, basi, jambo lolote linalotokea kwako, amini ni mapenzi yake.
Pengine anataka kukupa majukumu mengine, na kwamba usingeweza kuyafikia majukumu hayo bila kuacha hayo uliyokuwa nayo, hivyo, yawezekana ni kipindi cha mpito (transition period) kuelekea huko.
Tumepewa mamlaka makubwa sana na Mwenyezi Mungu (labda kushinda viumbe wengine wote), ya kuwasiliana na Mungu wetu wakati wowote (nasikitika wengine hili hawalijuwi). Basi, upatapo muda mzuri (faragha), omba na kusali huku ukimwomba Mungu akuonyeshe lililo mbele yako, maana uwezo huo ametupatia.