walikojiandikisha kupiga kura Serikali za mitaa wajaa sana kwenye kampeni za CCM,Bila kusahau Tlaatlaah
Hovyo sana.Kuna katibu wa chama mtaani kwetu kachukua majina ya watu wazima wote nyumbani (sikuwepo) sijajua anamaanisha nini ingawa anajua tuliojiandikisha na ambao bado.
Jamaa wamejipanga, wanajua kila kaya waliojiandikisha na ambao bado. Na watakaowapigia kura. Wanapata ushindi kwa forecast kwanza kabla ya siku ya kupoga kura.
Wanadhani tatizo ni matangazo ya kuhamasisha, bila kujua watu wameamua hawataki upuuzi tena.Hawaamini macho yao. Naona baadhi ya watumishi wa umma wanaposti poster za kuamashisha watu kujiandikisha. Nadhani watakuwa wamewalazimisha kufanya hivyo. Vituoni hali ni mbaya.
😁😁😁Kituko, uhamasishaji unafanyika mpaka makanisani wananchi wakajiandikishe. Cha ajabu wahamasishaji ni viongozi wa ccm kata, wilaya, mkoa wanaingia makanisani na kusema wametumwa na ngazi za juu kuja kuhamasisha uandikishaji huku wengine wakiwa wamevaa sare zao za kijani. Cha ajabu zaidi wanatoa sadaka nzuri tu hata kama watakuta muda wa kutoa sadaka umepita. Wakishatoa sadaka wanatoka mbio kuwahi kanisa jingine kabla hawajatoka ibadani. Kwa sasa wanawafuata wananchi majumbani mwao kuwaandikisha kwa kuwabembeleza. Wananchi wanawakubalia kuandikishwa japo wanasema hawataenda kupiga kura, hawana muda huo wa kupoteza shughuli zao
sasa kama watu wanasoma samia mitano tena watahamasika vipi kwenda kujiandikisha kupiga kura wakati wameshatangaziwa ni samia tena mingine mitano?Jana nimefatwa na bodaboda yenye bango la lililoandikwa Samia mitano tena
Wanasema panda Kaka ukajiandikishe kama wajibu wa mtanzania
BIla shaka wako mstari wa mbele wakigaragara na kuwasii watu wajitokeze kujiandikisha.
Ata sasa nyie ndio mko kila sehemu kuna kipi kipya mmefanya?.Endeleeni kutojiandikisha halafu baadaye mje kuanza kulia lia pale CCM tutakapo beba na kuzoa kila kitu katika uchaguzi.
Spana zimekuwa Kali, wanataka kujisafisha kiaina.Wameamua kuwaangushia jumba bovu viongozi wao wanaomaliza muda wao kuwa ndiyo wanaovuruga zoezi la uandikishaji wapiga kura wakati ni wao wenyewe walioratibu uhuni huu ili kuficha aibu ya watu kususia kujiandikisha.
Salaam, shalom!!
Viongozi tulikuwa tukiwaonya kupunguza viburi, mlikuwa mkitamba Kwa kauli za kejeli kuwa " Hata msipoipigia CCCM kura Bado itaunda Serekali"
Wengine wakaenda mbali na kudai kuwa " CCM kamwe haitatoka madarakani Hadi ipende yenyewe kama ambavyo Pascal Mayalla amekuwa akidai,
Viongozi wetu mkashindwa kujua kuwa kauli zenu ni sawa na kumshika mkono kipofu wakati mnamwibia chakula chake,
Matokeo ya kauli zenu, wananchi wamestuka, wamesusa,wamepuuza wamekaa pembeni.
Sasa Kuna Ile KANUNI ya ushindi wa mazingira, kuwa, wakijitokeza wapiga kura waliojiandikisha, unaongeza na za wizi Ili ionekane chama kimeshinda Kwa HAKI,
Sasa watu hawajiandikishi, wamegoma, mtaiba kura zipi ilhali watu hawajitokezi!!
Sasa uhalali wa kuongoza utatoka wapi ikiwa wananchi wamegoma kushiriki chaguzi sababu ya wizi na viburi vyenu?
Suluhu pekee iliyobaki mbeleni ni kubadili mgombea wa nafasi ya juu kuliko zote Ili angalau Nchi ipumue, chama kiendelee kuwepo japo Kwa miaka 10 ijayo, tofauti na hapo, yajayo...
Wana chi Si wajinga, mkae mkijua Hilo.
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿.
Karibuni 🙏
Elimu ya uraia inahitajika sana, ili raia wajue na kusimamia HAKI na WAJIBU wao.
Hiyo KAZI mnayofanya ni kama tu ulozi,Uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa maigizo kuliko chaguzi zote zilizopita.
Nipo mtaani tunaandika wapigakura, mabalozi wamejikusanya na orodha za watu wao tunachukua na kuweka waaah (kwa maelekezo kutoka juu) bila hata wahusika kujua. Umri tunakadiria, saini tunagushi, nk. Kweli bongo nyosso sana.
Sasa utahesabu kura zipi ikiwa watu wa kupiga kura hawatokei🤔Wenyewe waliojikoni walishasema kupiga kura na kuhesabu vitu viwili tofauti.
Takwimu tunazipata wapi!!Maana yake nini mambo haya.
Mbona kiongozi wa sekta ya uandikishaji anadai mwitikio ni mkubwa sana. Nyie takwimu huwa mnazipata wapi?
Sasa mtamtoaje na hamjajiandikisha? Na hata mkimkataa, anaiba kura,Juzi kulikuwa na msiba mtaani. kwa bahati mwili wa marehemu ulisafirshwa tukabaki baadhi ya watu kama ilivyo desturi yetu.
mwekiti wa mtaa akajiroga akasema vijana mbona hamjiandikishi?
siku zote nilijua ni mimi tu au tupo wachache sana ambao hatuna muda wa kujiandikisha kumbe vijana karibia wote
hawana mpango wa kujiandikisha.
Aliulizwa maswali yaani bado hajajibu kazomewa na aliambiwa tusikuone kabisa umegombea huu mtaa na ukipita hutaacha kuona kila rangi yetu!
Mimi kwa unyenyekevu nikamuuliza ndg mwenyekiti tangu tukuchague umetufanyia nini maana hata bara bara za mitaa gari hazipiti kipindi kwa sababu ya makorongo na hii ndo ilikuwa ahadi yako ya kuhakikisha bara bara za mtaa zinachimbwa na kuwekwe mifereji ya maji?
Alitamani alie halafu akaniuliza swali badala ya jibu Wewe hujaona nilicho fanya kweli? aisee wanatia huruma sana
kwa sasa baada ya swali hilo alizomewa mno ni aibu tupu
Sasa umejiandikisha halafu unamsikia mgombea anaongea Kwa dharau kuwa, hata msiponichagua,Elimu ya uraia inahitajika sana, ili raia wajue na kusimamia HAKI na WAJIBU wao.
Ikiwemo hii ya kushiriki katika kuchagua viongozi