LGE2024 Baada ya kupuuza Ule msemo wa jinsi ya kula na kipofu, Leo wanatafutwa wananchi wa kujiandikisha Kwa tochi ili kura ziibwe!

LGE2024 Baada ya kupuuza Ule msemo wa jinsi ya kula na kipofu, Leo wanatafutwa wananchi wa kujiandikisha Kwa tochi ili kura ziibwe!

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
walikojiandikisha kupiga kura Serikali za mitaa wajaa sana kwenye kampeni za CCM,

wachache ambao hawakujiandikisha kwasabb za ushirikina wao, wakua kwenye kampeni za upinzani wakipeana matumaini na muujiza wa kushinda uchaguzi 🤣
 
Wananchi wengi wamejiandikisha tayari kukipa chama CCM ushindi wa kishindo. Huu uzi wenu ni wa kujifariji.
 
Kuna katibu wa chama mtaani kwetu kachukua majina ya watu wazima wote nyumbani (sikuwepo) sijajua anamaanisha nini ingawa anajua tuliojiandikisha na ambao bado.
Jamaa wamejipanga, wanajua kila kaya waliojiandikisha na ambao bado. Na watakaowapigia kura. Wanapata ushindi kwa forecast kwanza kabla ya siku ya kupoga kura.
Hovyo sana.
 
Kituko, uhamasishaji unafanyika mpaka makanisani wananchi wakajiandikishe. Cha ajabu wahamasishaji ni viongozi wa ccm kata, wilaya, mkoa wanaingia makanisani na kusema wametumwa na ngazi za juu kuja kuhamasisha uandikishaji huku wengine wakiwa wamevaa sare zao za kijani. Cha ajabu zaidi wanatoa sadaka nzuri tu hata kama watakuta muda wa kutoa sadaka umepita. Wakishatoa sadaka wanatoka mbio kuwahi kanisa jingine kabla hawajatoka ibadani. Kwa sasa wanawafuata wananchi majumbani mwao kuwaandikisha kwa kuwabembeleza. Wananchi wanawakubalia kuandikishwa japo wanasema hawataenda kupiga kura, hawana muda huo wa kupoteza shughuli zao
😁😁😁

Tanzania ni channel ya comedy kule mbinguni
 
Leo nimewaona watumishi wa manispaa fulani Dar wanavyohangaika kuhamasisha. Zimemwagwa 'reflectors' kibao mpaka kwa bodaboda.Na hapa pia lazima kuna wizi kama kawaida.
 
Wameamua kuwaangushia jumba bovu viongozi wao wanaomaliza muda wao kuwa ndiyo wanaovuruga zoezi la uandikishaji wapiga kura wakati ni wao wenyewe walioratibu uhuni huu ili kuficha aibu ya watu kususia kujiandikisha.
Spana zimekuwa Kali, wanataka kujisafisha kiaina.
 
Wenyewe waliojikoni walishasema kupiga kura na kuhesabu vitu viwili tofauti.
 
Salaam, shalom!!

Viongozi tulikuwa tukiwaonya kupunguza viburi, mlikuwa mkitamba Kwa kauli za kejeli kuwa " Hata msipoipigia CCCM kura Bado itaunda Serekali"

Wengine wakaenda mbali na kudai kuwa " CCM kamwe haitatoka madarakani Hadi ipende yenyewe kama ambavyo Pascal Mayalla amekuwa akidai,

Viongozi wetu mkashindwa kujua kuwa kauli zenu ni sawa na kumshika mkono kipofu wakati mnamwibia chakula chake,

Matokeo ya kauli zenu, wananchi wamestuka, wamesusa,wamepuuza wamekaa pembeni.

Sasa Kuna Ile KANUNI ya ushindi wa mazingira, kuwa, wakijitokeza wapiga kura waliojiandikisha, unaongeza na za wizi Ili ionekane chama kimeshinda Kwa HAKI,

Sasa watu hawajiandikishi, wamegoma, mtaiba kura zipi ilhali watu hawajitokezi!!

Sasa uhalali wa kuongoza utatoka wapi ikiwa wananchi wamegoma kushiriki chaguzi sababu ya wizi na viburi vyenu?

Suluhu pekee iliyobaki mbeleni ni kubadili mgombea wa nafasi ya juu kuliko zote Ili angalau Nchi ipumue, chama kiendelee kuwepo japo Kwa miaka 10 ijayo, tofauti na hapo, yajayo...

Wana chi Si wajinga, mkae mkijua Hilo.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿.

Karibuni 🙏

Elimu ya uraia inahitajika sana, ili raia wajue na kusimamia HAKI na WAJIBU wao.
Ikiwemo hii ya kushiriki katika kuchagua viongozi
 
Uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa maigizo kuliko chaguzi zote zilizopita.

Nipo mtaani tunaandika wapigakura, mabalozi wamejikusanya na orodha za watu wao tunachukua na kuweka waaah (kwa maelekezo kutoka juu) bila hata wahusika kujua. Umri tunakadiria, saini tunagushi, nk. Kweli bongo nyosso sana.
Hiyo KAZI mnayofanya ni kama tu ulozi,

Ukitafuta sababu na faida ya kuwafanya watu kama wajinga huioni.

Ndio maana Hayati Nyerere alitishia kurudisha Kadi!
 
Juzi kulikuwa na msiba mtaani. kwa bahati mwili wa marehemu ulisafirshwa tukabaki baadhi ya watu kama ilivyo desturi yetu.
mwekiti wa mtaa akajiroga akasema vijana mbona hamjiandikishi?
siku zote nilijua ni mimi tu au tupo wachache sana ambao hatuna muda wa kujiandikisha kumbe vijana karibia wote
hawana mpango wa kujiandikisha.

Aliulizwa maswali yaani bado hajajibu kazomewa na aliambiwa tusikuone kabisa umegombea huu mtaa na ukipita hutaacha kuona kila rangi yetu!

Mimi kwa unyenyekevu nikamuuliza ndg mwenyekiti tangu tukuchague umetufanyia nini maana hata bara bara za mitaa gari hazipiti kipindi kwa sababu ya makorongo na hii ndo ilikuwa ahadi yako ya kuhakikisha bara bara za mtaa zinachimbwa na kuwekwe mifereji ya maji?

Alitamani alie halafu akaniuliza swali badala ya jibu Wewe hujaona nilicho fanya kweli? aisee wanatia huruma sana
kwa sasa baada ya swali hilo alizomewa mno ni aibu tupu
Sasa mtamtoaje na hamjajiandikisha? Na hata mkimkataa, anaiba kura,

Njia mbadala ni ipi?
 
Elimu ya uraia inahitajika sana, ili raia wajue na kusimamia HAKI na WAJIBU wao.
Ikiwemo hii ya kushiriki katika kuchagua viongozi
Sasa umejiandikisha halafu unamsikia mgombea anaongea Kwa dharau kuwa, hata msiponichagua,

Mimi ndiye nitakayeshinda uchaguzi na hachukuliwi hatua yeyote,

Nini kinajengeka akilini mwako?
 
Back
Top Bottom