LGE2024 Baada ya kupuuza Ule msemo wa jinsi ya kula na kipofu, Leo wanatafutwa wananchi wa kujiandikisha Kwa tochi ili kura ziibwe!

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Sasa kama ulimpa balozi Jina na namba Yako, uende kujiandikisha mara mbili?

Jina lako lishaandikwa na litapiga kura kumpa ushindi wamtakaye.
Niliambia kachukua, nitamuuliza anamaanisha nini. 😁😁
 
Maana yake nini mambo haya.
Mbona kiongozi wa sekta ya uandikishaji anadai mwitikio ni mkubwa sana. Nyie takwimu huwa mnazipata wapi?
Tafuta ndugu au rafiki yako ambaye ni DED akupe ukweli, zoezi mpaka jana Halmashauri fulani Mkoani Pwani ni 48% ya matarajio.
 
Safi sana wananchi,hawa watawala wanapaswa kujua kwamba ujinga wao upo dhahiri.
 
Hao wa CCM wako wapi?
Hujasikia kwamba vituo ni vitupu hakuna foleni, waandikishaji wanalala tu USINGIZI bila KAZI?

Nilidhani tatizo kuu ni CHADEMA, kumbe wananchi wasio na vyama nao hawataki kuwasikia.

Tusubiri uchaguzi mkuu.
 
Mkuu siasa safi ni vitendo, kwa maana ya kuwafikia wananchi na shida zao. Hizi nadharia mahali pake ni humu jukwaani.

Huko kwenye vitendo mikoani na vijijini muda huu kuna michakato mingi tu ya ujenzi wa viwanda inaendelea kuna upatikanaji wa umeme karibu kila kona ya Tanzania, miradi ya maji inasambaa na mingine kumaliziwa.

Kibaya ni ingekuwa CCM wanaiba tu pesa bila ya kushughulika na shida za watu. Hawana sababu ya kuiba kura wakati kila siku wapo huko walipo wananchi na wanatatua shida zao.
 
Kwamba unakataa kata kata CCM kamwe haijawahi kuiba kura Wala Kutoa RUSHWA.

Apia!!
 
Kwamba unakataa kata kata CCM kamwe haijawahi kuiba kura Wala Kutoa RUSHWA.

Apia!!
Wanatoa rushwa na pia wanastahili kura zote wanazozipata. Mkuu sisi tunapiga kelele humu mitandaoni lakinj huko mtaani hali ni tofauti kabisa.
 
Sasa ushindi wa kishindo utatoka wapi ikiwa watu wengi hawajiandikishi?
Jumla ya kura zilizopigwa ni 200, mgombea wa CCM kapata kura 190 sawa na 95%... hicho tayari ni kishindo.
 
Jumla ya kura zilizopigwa ni 200, mgombea wa CCM kapata kura 190 sawa na 95%... hicho tayari ni kishindo.
Kijiji chenye watu 10,000, wakijitokeza watu 500 kujiandikisha, wakapiga kura watu 250, mgombea wa CCM akapata kura 150 na kutangazwa mshindi,

Uhalali, legitimacy ya kuongoza hapo uko wapi, haupo,

Haiwezekani mji wenye watu 10,000 mshindi achaguliwe na watu 150 pekee.

Kubali, kataa, chama kinaelekea mwisho wa uhai wake.
 
Hayo yote sio muhimu, hata hivyo CCM inahamasisha watu wajiandikishe...... huku vyama vingine vikishawishi watu wasiende.
 
Maana yake nini mambo haya.
Mbona kiongozi wa sekta ya uandikishaji anadai mwitikio ni mkubwa sana. Nyie takwimu huwa mnazipata wapi?
..sasa ulitegemea atasemaje.. kumbuka huyo ni mfanyakazi wa serikali aseme mwitikio haupo mi ccm imnyambishe? ila anajua kabsaa watu hawataki kujiandikisha
 
Endeleeni kutojiandikisha halafu baadaye mje kuanza kulia lia pale CCM tutakapo beba na kuzoa kila kitu katika uchaguzi.
Bora mchukue mkiwa peke yenu wengine tuendelee na shughuli zingine lakini siyo tusimamishe shughuli kukaa foleni masaa 10 kisha anatangaza mumtakae tusije wafumua marinda bila hisia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…