kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Nimerudia kuitazama mara tatu ile mechi kati ya Kaizer Chiefs vs Yanga mashindano ya TOYOTA Cup nimebaini kuwa Kaizer Chiefs haikuwa timu mbovu hata kidogo, ni makosa madogomadogo ya kukosa pumzi na muunganiko kuliko Yanga kulikosababisha Kaizer kuchapwa 4-0. Nabi hana kazi ngumu sana kuifanya Kaizer kuwa timu tishio kwenye ligi yao na hata kutwaa ubingwa au kuchisha nafasi ya pili kwenye ligi yao.
Wafanyabiashara wanapenda kuwekeza kwenye timu imara kama Yanga, wakijua kuwa watapata mileage kubwa ndani na nje ya nchi husika kama ilivyo Yanga ambayo ni bigwa Tanzania, inayoshiriki caf champions, yenye wachezaji wakubwa kama Aziz Ki na walioshinda Toyota cup, 2024.
TOYOTA ni kampuni kubwa sana sana duniani, tumieni fursa hii ya sasa kuomba udhamini wao, maana 98% ya magari yote Tanzania ni kutoka TOYOTA, uwezo wa toyota kuwakatalia ni mdogo sana. Waombeni kujenga uwanja wenu (TOYOTA Stadium).