Baada ya kustaafu katelekezwa na mke na watoto wake. Anaugua ugonjwa wa akili kwa sasa

Kwani watu wakistaafu hawapewi visent kiasi mbona mi mzee wangu kastaafu, Ila mara nyingi nikikwama ananitoa, na wananitumia vitu vingi Mara nyingi tu, au Kuna tofauti ya wastaafu.
 
Kabisa mkuu ni kukaa kwa kujihami sana na hawa wanawake.
 

Wakat mwingine mkuu njia za giza hutumika
 
Huyo kazingua unapoamua kutokuoa basi lazima utaweka mda wako kwenye kitu flani na hicho ndio kitakacho kufahamisha mtu mpaka utoe harafu inaonekana huna makuu kwenye jamii yako.
 
Hakuna kukataa ndoa ila mwanaume unatakiwa kukaa kitaalamu nakujiandalia mazingira mazuri
 
Kwani anashundwa Nini kuanza kutafuna hayo majumba aliyojenga?

Kwa mtazami wangu huyo Mzee kastaaafu Hana kitu na pension kahonga. Full stop
Afadhali hata wewe umesema, kuna wazee wengine wakiwa kazini wanakuwa wababe hatari kwa wake zao, sasa akitaafu anahonga na kumaliza pesa yote sasa mke afanye nini hapo, kama anamajumba anashindwa nini kufaidika nayo!
 
Kama bado yu hai hizo si bado ni zake , pole yake
 
Tatizo ni hili ukioa oa mwanamke ambaye umri mnakaribiana ili mkizeeka mnazeeka wote saaa wewe una 40 unaoa wa23 Miaka wewe una 60 mwezako ana 35 mtasumbuana tu
Acha wakome hujioana vidume mtu anastaafu mke ndiyo kwanza anaitafuta 40 kwa mbaali anategemea nini hapo, huku visukari juu, hapo hapo wakati ana afya alimtemi kwa ndoa, huwa tunasubilia uzeeni ha ha haaaa
 
Mimi nimeona mzee akitelekezwa na watoto baada ya kustaafu!! Akawa anatembea mitaani kuomba omba buku!!
Na ukute alipostaafu alishauriwa akagoma na pesa zake akaenda kutumbua na vidosho sasa zikiisha ndiyo anaomba huruma kwa mke ha ha ha ukimkuta mwanamke kauzu lazima uwe omba omba.
 
Wangapi ndugu zao wanawatenda, au watoto wa ndugu anawanyanyasa vyakutosha, sema nikumuomba Mungu akupe mwenza wa kufanana naye.
 
Mkuu chimbia hata ardhini 😂😂

Ila hakikisha mwanaume hukosi fungu lako la kujisapoti mwenyewe wakati mambo yanapo geuka.
Heeee!!!! 😳Aridhini tena aisee.... Hapo pagumu huwez chimbia zote
Labda ufungue bank account ya Siri alfu uandike majina ya mwingne Ili kikija sanuka Mahakama uonekane huna kitu
 
Hii kaka umeongea sahihi kabisa aiseee
 
Hapo Ni mchaga kwa mchaga kafanywa hivyo
Sasa wewe Muha/Mngoni/ Msukuma kaoe migombani uje uone Moto wake ukistaafu.
 
Hii ndio tunaita one sided story, tupe story ya upande wa pili, mwanaume ukiwekeza vizuri kwenye upendo kwa familia itakuja kukulipa siku za usoni.
Ni jambo nzuri kusomesha, ila kumbuka kuna mengine, acha kuhonga na mavituko ya hovyo huko nje, na kama una michepuko, basi ifanye siri sana, tumia nguvu nyingi kuficha.
Nina mjomba wangu kwa sasa yupo kijijini anakipata cha moto, ana bahati mkewe amebaki naye wanateseka wote maana mke kashikilia dini.
Mjomba alihonga sana enzi zake, na hakua anaifanya siri.
 
Mimi nimeona mzee akitelekezwa na watoto baada ya kustaafu!! Akawa anatembea mitaani kuomba omba buku!!

Usiombe ya kukute! Ata wewe Mwanaume unaesoma hapa Jitafakari!Je umeoa Mke mkeo au......Unaishi na Mwanamke alieleta Rafiki zake(Watoto mliozaa) ili watumbuwe mali zako kisha kusepa na kukuacha uoshe vyombo na kusugua masufuria ya Ugali peke ako uzeeni??
 

Attachments

  • AD9258C6-6C14-4889-87DD-690669F961D6.jpeg
    32.4 KB · Views: 2
Mjomba wako wa nchi gani? Wewe ni Mkenya wa mchongo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…