Afande Tanzania
JF-Expert Member
- May 3, 2020
- 460
- 1,169
Mkuu Erythrocyte baada ya October 2020 Nahisi tutatofautiana iwapo tu sheria ikipindishwa kuwasamehe wahalifu wa awamu ya5 na wale waliowatangulia huko nyuma. Rais mtarajiwa TAL akiwasamehe wahalifu waliotangulia nyuma yake hakika hatakuwa na utofauti wowote na hao wahalifu, anatakiwa awe mfano wa utawala wa sheria ambao amekuwa akituhubiria kila siku, AWAHUKUMU KWA MUJIBU WA SHERIA!Kuna haja ya kulijadili hili mapema ili kutoana hofu, hasa baada ya Watanzania wengi kuahidi kumchagua Tundu Lissu ili awe Rais wao.
Bila shaka madaraka yanalevya na kuna wanaofahamika kutumia madaraka yao vibaya kwa kudhani kwamba watakuwa madarakani milele, sasa ni dhahiri kwamba muda wao umekwisha ghafla bila wenyewe kujiandaa, huku ikitajwa kwamba ujio wa lissu "The Game Changer" umeharakisha kung'oka kwao.
Sasa nimekuja kwenu wana JF kuuliza hivi, hawa waliotumia madaraka yao vibaya tuwakusanye uwanja wa Taifa tuwaonye na kuwakaripia kwa uchafu wao na kuwasamehe tu au tuache Sheria ichukue mkondo wake?
Kwa upande wangu mimi ni muumini wa kufuata Sheria na haki.
List ni ndefu kidogo, kila mtu ahukumiwe kadiri ya uhalifu alioufanya