Baada ya Maji ya Kilimanjaro Kuchakachuliwa, Je Maji Yako Bora ni Yapi?

Baada ya Maji ya Kilimanjaro Kuchakachuliwa, Je Maji Yako Bora ni Yapi?

Sidhani kama yamechakachuliwa.

Nimewahi kufanya kazi kampuni ya maji ambayo mshindani wa karibu in terms of ubora ni Kilimanjaro. Yaani pH za hizi kampuni mbili inaruhusu maji yao kuuzwa hata ubalozi wa Marekani.

Kwa kampuni niliyokua nafanyia kazi ilikua maji ya nusu lita yanauzwa 1500, wakati Hill, Uhai kwa 700 unapata 1.5 litres na maji mengine mfano Pangan unapata kwa 500.

So, soko kubwa limetekwa na wanunua maji ya 500, na wewe unaweza shindana nao ila ni mpaka umodify pH ili uzalishaji usile hela nyingin na 500 ikupe faida.

Mfano wewe ndiyo Kilimanjaro, utalifuata soko la walipa 500 ila unamodify pH au utaacha maji yawe na ubora wa kimataifa ila soko lako liko very selective na kuna muda utawala ulifanya maji yako kuonekana kwenye mataasisi ishindikane?

Nafikiri matokeo ndiyo haya ambayo mleta uzi anahisi maji yamechakachuliwa
 
Kibiashara ni vigumu kuchakachua maji ya Kilimanjaro kuliko maji ya kampuni zingine, na hiyo ni kwa sababu kuu moja tu, maji yale kipekee yanazalishwa na kiwanda cha Bonite kule Moshi, na hao wazalishaji wanasimamia wao wenyewe mchakato wote wa kusambaza kuanzia kuyatoa kiwandani mpaka kwa muuzaji wa mwisho na randomly kila hatua mara kwa mara huchukua sampuli ili kwenda kuzipima.

Ikiwa mzalishaji mwenyewe anasimamia na kuhodhi supply chain ya bidhaa zake, sio rahisi kuingiza mzigo fake.
Sio kweli ...maji halisi ya Kilimanjaro ni yale yanayozalishwa Moshi na kampuni ya Bonite na haya husambazwa mikoa hasahasa ya Kaskazini .Kiwanda cha CocaCola Mwenge wanazalisha pia maji ya Kilimanjaro kwa kutumia formula ileile ila yana ladha tofauti na yale ya Moshi na haya ndio yanasambazwa sehemu kubwa Tanzania.
 
plastiki za chupa za maji zina kemikali haribifu kwa vichochezi vya mwili, ambazo zinasababisha upungufu wa shahawa.

jitahidi sana usitumie maji ya chupa kadri uwezavyo.
 
Haya ni maji ya ziwa. Ziwa lipo very much polluted.

Wataalam wanasema maji mazuri kabisa kwa Tanzania ni MKWAWA, ni ya chemichemi, ni natural water, siyo pure water. Shida ya hayo maji ya MKWAWA, yanapatikana kwa shida sana. Nadhani hiyo chemichemi haitoi maji mengi sana.

Kiujumla maji mazuri kabisa kiafya, ni maji yasiyotoka kwenye vyanzo vile vinavyosafiri sana au vilivyotawanyika sana. Kwa mfano, maji yanayotoka Ziwa Victoria, ziwa linaunganisha nchi 3, ni ziwa la pili kwa ukubwa wa eneo la maji fresh Duniani. Kuna takataka nyingi za kutoka viwandani zinatiririshwa ndani ya maji hayo. Maji haya yanatajwa kuhusishwa na uwepo wa cases nyingi za saratani zinazowapata jamii zinazoishi kando kando ya ziwa hili kwa mataifa yote matatu.

Maji mengine yasiyofaa ni yale ya mito mikubwa inayosafiri maelfu ya kilometa. Mito hii inakusanya kila aina ya hatari kwa afya, hasa chemicals zitokazo viwandani, na hata mashambani.

Tatizo jingine kubwa sana ni hizi mamlaka za ukaguzi zilizojaa rushwa. Kampuni hizi za maji zinatakiwa kuwa na wakemia, na wakemia wanatakiwa kufanya random samples check, na wakigundua maji yamekosa kufikia viwango vya ubora, wanatakiwa kuzuia batch yote kuingia sokoni, lakini hilo halifanyiki. Kuna case moja mkemia wa kampuni aligundua maji yamekosa ubora, akazuia batch kuingia sokoni, kilichofuatia, alifukuzwa kazi mara moja. Baada ya kufanyiwa uovu huo akatoa taarifa kwa mamlaka ya Serikali, wakamwambia taarifa inafanyiwa kazi. Wachunguzi walienda, lakini inasemekana, baada ya kupewa fungu zuri, biashara iliendelea kama kawaida.

Kwa Tanzania, kutokana na rushwa ilivyoshamiri, hivyo viwanda hata vikichota tu maji na kujaza kwenye chupa, hakuna mamlaka ya kuchukua hatua.

Kuna wakati tulinunua mtambo wa kuchuja maji kwaajili ya matumizi ya wafanyakazi wa kampuni, na kila mwezi tulikuwa tunachukua samples za maji ya chupa kwa kampuni zote, pamoja na yale yaliyochujwa na mtambo wetu, tukawa tunapeleka kwenye maabara South Africa,. Siku zote, yale maji yaliyochujwa na mtambo wetu mdogo, yalikuwa na ubora kuzidi maji ya makampuni yote.
 
Back
Top Bottom