Haya ni maji ya ziwa. Ziwa lipo very much polluted.
Wataalam wanasema maji mazuri kabisa kwa Tanzania ni MKWAWA, ni ya chemichemi, ni natural water, siyo pure water. Shida ya hayo maji ya MKWAWA, yanapatikana kwa shida sana. Nadhani hiyo chemichemi haitoi maji mengi sana.
Kiujumla maji mazuri kabisa kiafya, ni maji yasiyotoka kwenye vyanzo vile vinavyosafiri sana au vilivyotawanyika sana. Kwa mfano, maji yanayotoka Ziwa Victoria, ziwa linaunganisha nchi 3, ni ziwa la pili kwa ukubwa wa eneo la maji fresh Duniani. Kuna takataka nyingi za kutoka viwandani zinatiririshwa ndani ya maji hayo. Maji haya yanatajwa kuhusishwa na uwepo wa cases nyingi za saratani zinazowapata jamii zinazoishi kando kando ya ziwa hili kwa mataifa yote matatu.
Maji mengine yasiyofaa ni yale ya mito mikubwa inayosafiri maelfu ya kilometa. Mito hii inakusanya kila aina ya hatari kwa afya, hasa chemicals zitokazo viwandani, na hata mashambani.
Tatizo jingine kubwa sana ni hizi mamlaka za ukaguzi zilizojaa rushwa. Kampuni hizi za maji zinatakiwa kuwa na wakemia, na wakemia wanatakiwa kufanya random samples check, na wakigundua maji yamekosa kufikia viwango vya ubora, wanatakiwa kuzuia batch yote kuingia sokoni, lakini hilo halifanyiki. Kuna case moja mkemia wa kampuni aligundua maji yamekosa ubora, akazuia batch kuingia sokoni, kilichofuatia, alifukuzwa kazi mara moja. Baada ya kufanyiwa uovu huo akatoa taarifa kwa mamlaka ya Serikali, wakamwambia taarifa inafanyiwa kazi. Wachunguzi walienda, lakini inasemekana, baada ya kupewa fungu zuri, biashara iliendelea kama kawaida.
Kwa Tanzania, kutokana na rushwa ilivyoshamiri, hivyo viwanda hata vikichota tu maji na kujaza kwenye chupa, hakuna mamlaka ya kuchukua hatua.
Kuna wakati tulinunua mtambo wa kuchuja maji kwaajili ya matumizi ya wafanyakazi wa kampuni, na kila mwezi tulikuwa tunachukua samples za maji ya chupa kwa kampuni zote, pamoja na yale yaliyochujwa na mtambo wetu, tukawa tunapeleka kwenye maabara South Africa,. Siku zote, yale maji yaliyochujwa na mtambo wetu mdogo, yalikuwa na ubora kuzidi maji ya makampuni yote.