Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 15,415
- 29,584
Hi serikali huwa inachezea sana wananchi kwenye suala la bei ya mafuta. Kwa mfano, siku zote huwa tuna akiba ya mafuta yaliyonunuliwa ya miezi mitatu. Vita ya Iran na USA ilipoanza, japo tulikuwa bado na akiba ya mafuta ya miezi mitatu iliyonunuliwa kwa bei poa, serikali kwa makusudi iliamua kupandisha bei ya mafuta ili kujipa faida kubwa ya upepo (windfall profit), ikijua wazi ilikuwa inawaibia wananchi.
Sasa bei ya mafuta soko la dunia imeshuka baada ya makubaliano kati ya Iran na USA. Kwa karata ile ile ambayo serikali ilitumia kupandisha bei ya mafuta huku ikielewa wazi bado tuna mafuta ya bei nafuu, sasa tunatarajia bei ya mafuta ishuke kwa kiwango kizuri mwezi wa saba. Kama kuna suala la kufidia bei basi wafidie kwa fedha za faida ya upepo waliyochukua vita ilipoanza.
La sivyo bei ya juu ya mafuta ni sababu nyingine nzuri ya wananchi kutoka na kuandamana hiyo 7/7, kwa sababu maisha yamekuwa magumu sana na ni kama serikali haijali kabisa maumivu ya wananchi.