Al jazeera: Bei ya mafuta imeshuka katika kiwango ambacho hakijawahi kuonekana toka kuanza kwa vita vya USA-Israel dhidi ya Iran. Vipi huku kwetu?

Al jazeera: Bei ya mafuta imeshuka katika kiwango ambacho hakijawahi kuonekana toka kuanza kwa vita vya USA-Israel dhidi ya Iran. Vipi huku kwetu?

Mkono Mmoja

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2019
Posts
4,994
Reaction score
9,625
Shalom Shalom wakuu...!!

Katika kuperuzi kwangu mtandaoni nimekutana na taarifa kutoka kwa shirika la habari la kimataifa la Al Jazeera ikisema kuwa bei ya mafuta imeshuka sana katika viwango ambavyo havijapatwa kushuhudiwa toka vita ya Marekani akishirikiana na Israel dhidi ya taifa la Iran.

Wamesema kuwa pipa moja la Mafuta ghafi lililokuwa likiuzwa dola za kimarekani 126 sasahivi limeshuka mpaka kufikia dola za kimarekani 70. Huku wakitazamia bei ikiendelea kushuka kwa kasi zaidi mwezi Agosti.

Chanzo :" Oil prices fall to levels not seen since start of US-Israel war on Iran


Swali langu kubwa ni kwanini bado tunaendelea kuuziwa mafuta kwa bei ya sh 4000-4300 kwa petrol na dizeli?

Ina maana huku kwetu bado vita vinaendelea wakuu?

Wakulima na wadau wa utumiaji wa sekta ya usafirishaji tunaumia maana vijijini lita moja tunauziwa kwa sh 5000....!! Nauli sehemu tuliyokuwa tukilipa elfu 6 sasa hv tunalipa 20,000.

Wachumi na watu wa mamlaka ya EWURA pamoja na Wizara ya nishati na madini jitokezeni mtueleze kwanini mafuta nchini Tanzania hayashuki bei???

Watu wa LATRA mpo kimya jinsi nauli za mabasi zilivyo juu huku uchumi wa mwananchi mmoja mmoja ukiwa chini na unazidi kudidimia. Tunataka kama vile mlivyotoka haraka kupandisha bei za nauli vilevile mtoke haraka kutangaza kuwa nauli zishuke bei zirudi kabla ya vita maana kisingizio cha vita na meli kutopitika katika mlango wa bahari wa Hormuz haupo tena.

Au mtuambie kuwa vita sasa hv bado vinaendelea tujue moja...Wakulima tunashindwa kumwagilia mashamba yetu kutokana na kupanda kwa gharama za petrol na dizeli...mimea inakauka....TUNAUMIA WAKUU?

MBOLEA ZENYEWE HAZIPATIKANI MADUKANI, WAUZAJI WANASEMA KUWA BADO VITA SIJUI VINAENDELEA NA UKIIPATA UNAUZIWA 120,000.

Asanteni

​
Screenshot_20260705-114033.jpg



CC: Wizara ya Nishati na Madini
CC : EWURA
CC: LATRA
 
A forum user, Mkono Mmoja, highlights an Al Jazeera report stating that global crude oil prices have significantly dropped from $126 to $70 per barrel, reaching levels not seen since the "US-Israel war on Iran" began.

The user questions why, despite this global decline, fuel prices in Tanzania remain high at TZS 4000-4300 per liter for petrol and diesel in urban areas, and up to TZS 5000 in rural areas. The poster challenges the common excuse of war and shipping disruptions in the Strait of Hormuz, arguing it's no longer valid.

This situation is causing severe hardship for farmers (due to high irrigation costs and expensive, scarce fertilizer at TZS 120,000) and the transportation sector (with bus fares increasing dramatically from TZS 6,000 to TZS 20,000).

Mkono Mmoja urges regulatory bodies, specifically EWURA, the Ministry of Energy and Minerals, and LATRA, to provide an explanation and promptly reduce fuel prices and transportation fares to pre-conflict levels. The user demands a clear answer: whether the "war" is still considered ongoing locally, or if prices should finally reflect the global market.
 
Wakati vita ikiianza tuliambiwa kuwa nchi ina akiba ya mafuta mpaka kufika mwezi July....

Mungu sio MRISHO mpoto ...Vita vimeisha kabla ya mwezi July ila cha ajabu mafuta tumepandishiwa bei toka mwezi April..

Nazungumza kwa uchungu sana na nieleweke kuwa sifungamani na itikadi za chama chochote cha kisiasa .
 
Back
Top Bottom