Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 122,494
- 96,074
Tena mapeeemaaaaaBado nakazia NDUGULILE JIUZULU
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tena mapeeemaaaaaBado nakazia NDUGULILE JIUZULU
Walikuwa wanapima upepo tu na hili tulilisema humu.
Mitandao ina nguvu sana!
Dr.Slaa sasa atapongeza uamuzi huu
Angekuwa fulani angesema tunapoteza muda wa kulima kwenye mitandao hivyo tutwangwe haswaaa na angeungwa mkono. Haya mzee Slaa tayari tangazo lingine limetoka wahi ukapongeze. Yani ukimaliza huu mwezi ukiwa balozi nenda katambike!
Dar es Salaam. Saa chache baada ya kutangazwa kwa bei mpya za vifurushi, Serikali imetangaza kusitisha kutumika kwa gharama hizo hadi hapo itakapotangazwa baadaye.
Uamuzi huo unaweza kuwa habari njema kwa watumiaji wa mitandao ya simu ambao, tangu kutangazwa kwa bei hizo mpya mapema leo Ijumaa ya Aprili 2, 2021, wamekuwa kwenye mjadala mzito kwani, matarajio ya wengi ilikuwa ni kushuka kwa gharama hizo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala, amesema matumizi ya bei mpya ya vifurushi yamesitishwa kwa muda.
Hata hivyo, amesema uamuzi huo utahusu vifurushi vya data pekee huku vile vya ujumbe mfupi wa maneno na kupiga zitaendelea kama ilivyotangazwa mapema leo Ijumaa.
“Tumesitisha matumizi ya gharama mpya za vifurushi hadi hapo itakapotangazwa baadaye. Lakini, hili litahusu vifurushi vya data pekee na vile vya sms na kupiga vitaendelea kama kawaida,” amesema Mwakyanjala alipozungumza na Mwananchi kwa njia ya simu dakika chache zilizopita.
Kanuni ndogo za gharama na tozo za vifurushi, utangazaji wa huduma na ofa maalum zilizotungwa na TCRA, zimeanza kutumika leo ambapo, matumaini ya wengi ilikuwa ni bei za vifurushi kupungua lakini ikawa tofauti.
Source:Serikali yasitisha bei mpya za vifurushi
View attachment 1741556
Hao ni mazuzu tu na inaonekana ni kula kulala tu kwa shemeji zao.Kuna watu wanajiita magu2016 na countrywide sjui hapa watashangilia.
Kuwa kijana wa aina ya hawa watu inahitaji uwe ni mjinga na psychopathy wa hali ya juu sana.
Katika hili.Create a problem-Solve a problem-Become a Hero.
Serikali ya kiki
Wa kulaumiwa ni Dr Ndugulile ,hawa wanasiasa ndio wanaifanya serikali ilaumiwe, wanadhani wanaongoza wananchi wa stone ages 1890 wakati sasa hizi ni kidigital, ndio maana tulisisitiza mawaziri wawe wataalam wa eneo husika kama lengo lao ni kumuwakilisha Rais, how come Ndugulile atudanganye? Mama Samia ilitakiwa amfukuze haraka.Tena mapeeemaaaaa
Wange yapata mkuu maana wasije jidanganya kuwa wangetumia mabomu wakatuweza.Naona walitafuta maandamano.
Yule ni Dr sio DkKatika hili.
Ndungulile's days at the ministry are numbered.
Hivi ndungulile Ni daktari wa falsafa PhD au wa COVID?
Maana baadhi ya PhD za bongo flavour Ni nzuri sana.
Ni MD(daktari wa binadamu)Katika hili.
Ndungulile's days at the ministry are numbered.
Hivi ndungulile Ni daktari wa falsafa PhD au wa COVID?
Maana baadhi ya PhD za bongo flavour Ni nzuri sana.
Kwani mtandao upi umeisitisha..hata tigo hvyohvyoAirtel hawajasitisha mpk sasa vifurushi vipo juu
Mungu fundi kweli kweliFedha za kujenga Chato zilikuwa zinatafutwa . Mtu huyu alikuwa wa ajabu sana mishahara haijaongezwa miaka mitano lakini kila kitu kinapanda. Hivi alitakaje?.
Yaani kwake mnyonge alikuwa anatumika kama kitendea maovuMtetezi halisi wa wanyonge anaonekana sio yule mkandamizaji wa wanyonge aliyekuwa anajiita mtetezi wa wanyonge.Huko aliko sijui atakuwa mtetezi wa nani
Duniani kote juhudi kubwa zinafanyika kuwawezesha wananchi kutumia mitandao kwa bei nafuu na ziko sehemu ambako jitihada zinafanyika kuwezesha huduma ya mitandao kwa bei karibu sawa na bure. Hapa Tanzania tunacho chombo (TCRA) kisichozalisha kitu lakini watu wanalipwa mishahara mikubwa eti kwa kubuni njia za kuongeza gharama katika matumizi ya mitandao...ili kubana uhuru wa kujieleza? Ujinga mtupu.Watu wachache sana wanaelewa hili, lakini ipo siku watakuja kujua. Hakukuwa na haja yeyote ya serikali kusimamia sekta kama mawasiliano kwa kiasi hiki, let the market decide
Mwenyezi Mungu ametufuta machozi watanzania, bado hamuamini tu?Honestly.....watanzania kwa sasa serikali tunayo...tumsupport mama...hana baya kwetu kwa hakika.
Mkuu em jaribu kufikiri zaidi ya hapo. Au unafikiri mitambo ya hao jamaa imesetiwa kudetect matamko automatically?Siyo kweli mbona menu inasoneka vile vile kama asubuhi. Hii taarifa nina mashaka nayo