mtaa umetulea
JF-Expert Member
- Nov 17, 2020
- 1,840
- 2,381
Haya ndio mambo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kabisa yaaniMama aongezewe mda katiba ibadilishwe atawale milele
katika hili la kupandishwa kwa gharama za vifurushi wa kilaumiwa sio mama samia, ni mwendazake.
Mwendazake alikuwa hapendi kukosolewa, alionyesha chuki ya wazi kabisa kwa watu waliokuwa wanamkosoa kupitia mitandao ya kijamii. Akafikia hatua ya kutamani malaika washuke wazime mitandao yote.
washauri wake kwa kutambua chuki ya wazi ya boss wao kwenye mitandao, wakaona bora wamfurahishe, wakaja na idea za kutumia vpn kwa upande wa twitter (japo haijasaidia) na kuongeza gharama za vifurushi.
Matokeo ya idea hizo ndio hii bei mpya ya kikatili ya vifurushi. ndungulile na team yake walisukumwa zaidi na utashi wa kisiasa kuliko utu ili wamfurahishe boss wao ambaye kwa sasa ni marehemu.
sina shaka na Mama Samia, najua atafikishiwa malalamiko kuhusu vifurushi hivi vya sasa ambavyo sio rafiki kwa mwananchi mwenye kipato cha chini na haraka sana atatoa amri ya kuvisitisha.
Friday April 02 2021
Mwananchi Gazeti
Dar es Salaam. Saa chache baada ya kutangazwa kwa bei mpya za vifurushi, Serikali imetangaza kusitisha kutumika kwa gharama hizo hadi hapo itakapotangazwa baadaye.
Uamuzi huo unaweza kuwa habari njema kwa watumiaji wa mitandao ya simu ambao, tangu kutangazwa kwa bei hizo mpya mapema leo Ijumaa ya Aprili 2, 2021, wamekuwa kwenye mjadala mzito kwani, matarajio ya wengi ilikuwa ni kushuka kwa gharama hizo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala, amesema matumizi ya bei mpya ya vifurushi yamesitishwa kwa muda.
Hata hivyo, amesema uamuzi huo utahusu vifurushi vya data pekee huku vile vya ujumbe mfupi wa maneno na kupiga zitaendelea kama ilivyotangazwa mapema leo Ijumaa.
“Tumesitisha matumizi ya gharama mpya za vifurushi hadi hapo itakapotangazwa baadaye. Lakini, hili litahusu vifurushi vya data pekee na vile vya sms na kupiga vitaendelea kama kawaida,” amesema Mwakyanjala alipozungumza na Mwananchi kwa njia ya simu dakika chache zilizopita.
Kanuni ndogo za gharama na tozo za vifurushi, utangazaji wa huduma na ofa maalum zilizotungwa na TCRA, zimeanza kutumika leo ambapo, matumaini ya wengi ilikuwa ni bei za vifurushi kupungua lakini ikawa tofauti.
Mwanzoni mwa Machi, 2021 Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba aliahidi utekelezaji wa kanuni hizo za kukabiliana na malalamiko juu ya huduma ya vifurushi yaliyotokana na maoni 3, 278 yaliyotolewa na wananchi.
Baadhi ya changamoto ambazo watumiaji wa huduma za simu walikuwa wakikutana nazo na kuzilalamikia ni pamoja na gharama za vifurushi kuwa juu na vifurushi vya data kubadilika mara kwa mara.
Jana mitandao ya simu iliwataarifu watumiaji wake juu ya mabadiliko hayo, lakini jambo ambalo limewaibua wengi hususani katika mitandao ya kijamii ni kuminywa kwa vifurushi hivyo kuliko hata ilivyokuwa awali wakati wanatoa malalamiko hayo.
Katika makundi ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp na mitandao mingine ya kijamii inayokutanisha watu kama Twitter, Instagram na Facebook mjadala ni vifurushi ambavyo vimebadilika katika mitandao yote ya huduma za simu wengi wanaomba walau hali irudi kama ilivyokuwa.
Mitandao mbali ya simu kama ilivyo ada katika sikukuu mbalimbali ilituma salamu zao za sikukuu kupitia kurusa zao za mitandao ya kijamii, lakini maoni ya wananchi wengi si kupokea salamu hizo bali ilikuwa ni kulalamikia mabadiliko yaliyofanywa katika vifurushi.
Zaidi, soma: Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi
View attachment 1741566

Slaa ni mchumia tumbo bado haelewi hatma yake kisiasa kwa hiyo tutegemee kumuona akiwa hyperWalikuwa wanapima upepo tu na hili tulilisema humu.
Mitandao ina nguvu sana!
Dr.Slaa sasa atapongeza uamuzi huu
Atake asitake lazima alazimishwe yuleMama tumpe mitano tena
Create a problem-Solve a problem-Become a Hero.
Serikali ya kiki
[emoji23][emoji23]Mama aongezewe mda katiba ibadilishwe atawale milele
🤣🤣We nawe huna hata akili. Sasa unadhani yeye alikua hajui?
🤣🤣🤣🤣Tcra: Tunapandisha bei ya bando.
Mataga: Safi sana bando lipande.
Tcra: Tumesitisha kupanda bei ya bando.
Mataga: Serikali sikivu.
Yani mko kama bendera fwata upepo hamna msimamo mpo mpo tu[emoji1787]
Hivi Huyo Doctor Slaa aliongea nini?Dr Slaa tunakuomba ujitokeze kwa mara nyingine tena kupongeza serikali .
Usaliti ni laana
Bundle sikuhizi ni muhimu mno, hafu mafuta ya kula waweza kula nchensho, pia cement sio wote twataka kujengeMngesimama kwenye mafuta ya kula na cement kama mlivyosimama kwenye bundle mngekua mmefanya lamaana sana.