Hauko serious wewe mwendazake hayupo hafu sie twateseka na bundle Bei juu, kwahili tuipongeze serikali aiseehuu utawala naona unatafuta umaarufu kwa kumpaka matope dr. magufuli hata kabla ya siku 21 za maombolezo hazijakoma.
Airtel *148*60# ingiaaa namba 3 un offer ipo kama kawaidaHahaha.. nimejaribu kila line niliyonayo kutafuta kifurushi chenye unafuu awapi!
Ule mkongo wa taifa unatusaidiaje sasa!
Hatari sana
Ushindani usio na bei elekezi ulifanya kampuni za simu zishindanie wateja... Bei ELEKEZI NI HATARI
Walikuwa wanapima upepo tu na hili tulilisema humu.
Mitandao ina nguvu sana!
Dr.Slaa sasa atapongeza uamuzi huu
Dr Slaa tunakuomba ujitokeze kwa mara nyingine tena kupongeza serikali .Walikuwa wanapima upepo tu na hili tulilisema humu.
Mitandao ina nguvu sana!
Dr.Slaa sasa atapongeza uamuzi huu
Angekuwepo bwana yule angefurahia sana kupanda kwa gharama maana walifanya hivi kumfurahisha mfalme Alfu Lela Ulela. Jamaa alihakikisha wanatengeneza Regulations ili kubana hela ipatikane maana aliona akiendelea kuzima mitandao atakosa kodi na hakuwa na akili ya kutafuta means mpya za Kodi. Kudos serikali ya Rais Samia Suluhu kwa kusikia kilio chetu watanzania maana hii ilikuwa disaster.Dar es Salaam. Saa chache baada ya kutangazwa kwa bei mpya za vifurushi, Serikali imetangaza kusitisha kutumika kwa gharama hizo hadi hapo itakapotangazwa baadaye.
Uamuzi huo unaweza kuwa habari njema kwa watumiaji wa mitandao ya simu ambao, tangu kutangazwa kwa bei hizo mpya mapema leo Ijumaa ya Aprili 2, 2021, wamekuwa kwenye mjadala mzito kwani, matarajio ya wengi ilikuwa ni kushuka kwa gharama hizo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala, amesema matumizi ya bei mpya ya vifurushi yamesitishwa kwa muda.
Hata hivyo, amesema uamuzi huo utahusu vifurushi vya data pekee huku vile vya ujumbe mfupi wa maneno na kupiga zitaendelea kama ilivyotangazwa mapema leo Ijumaa.
“Tumesitisha matumizi ya gharama mpya za vifurushi hadi hapo itakapotangazwa baadaye. Lakini, hili litahusu vifurushi vya data pekee na vile vya sms na kupiga vitaendelea kama kawaida,” amesema Mwakyanjala alipozungumza na Mwananchi kwa njia ya simu dakika chache zilizopita.
Kanuni ndogo za gharama na tozo za vifurushi, utangazaji wa huduma na ofa maalum zilizotungwa na TCRA, zimeanza kutumika leo ambapo, matumaini ya wengi ilikuwa ni bei za vifurushi kupungua lakini ikawa tofauti.
Source:Serikali yasitisha bei mpya za vifurushi
View attachment 1741556
Mbona bado vile vile ktk line zangu?au nmeelewa vby mkuu.Dar es Salaam. Saa chache baada ya kutangazwa kwa bei mpya za vifurushi, Serikali imetangaza kusitisha kutumika kwa gharama hizo hadi hapo itakapotangazwa baadaye.
Uamuzi huo unaweza kuwa habari njema kwa watumiaji wa mitandao ya simu ambao, tangu kutangazwa kwa bei hizo mpya mapema leo Ijumaa ya Aprili 2, 2021, wamekuwa kwenye mjadala mzito kwani, matarajio ya wengi ilikuwa ni kushuka kwa gharama hizo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala, amesema matumizi ya bei mpya ya vifurushi yamesitishwa kwa muda.
Hata hivyo, amesema uamuzi huo utahusu vifurushi vya data pekee huku vile vya ujumbe mfupi wa maneno na kupiga zitaendelea kama ilivyotangazwa mapema leo Ijumaa.
“Tumesitisha matumizi ya gharama mpya za vifurushi hadi hapo itakapotangazwa baadaye. Lakini, hili litahusu vifurushi vya data pekee na vile vya sms na kupiga vitaendelea kama kawaida,” amesema Mwakyanjala alipozungumza na Mwananchi kwa njia ya simu dakika chache zilizopita.
Kanuni ndogo za gharama na tozo za vifurushi, utangazaji wa huduma na ofa maalum zilizotungwa na TCRA, zimeanza kutumika leo ambapo, matumaini ya wengi ilikuwa ni bei za vifurushi kupungua lakini ikawa tofauti.
Source:Serikali yasitisha bei mpya za vifurushi
View attachment 1741556
Kichwa kichafu sio kweri sijaona kusitishwa mbona bado ipo vilevile tu.Habari.
Habari ya muda huu inayosambaa kwa sasa ni serikali kusitisha bei mpya ya vifurushi vilivyotangazwa na mitandao husika mwanzo wa mwezi huu.
Na imani yatakuwa maamuzi bora na itakuwa habari njema kwa wananchi.
Nawasilisha Mzee Mkoloni
Cc: Kichwa Kichafu.
Hata Voda ngoma bado iko vilevile,labda wanasubiri saa sita usikuWameshusha mtandao gani mbon huku halotel bon makamuzi bado yanaendelea?
Mzigo umerudi kama kawaida usipokuwa bundles za simu na sms ola internet ni kama kawaidaMbona bado vile vile ktk line zangu?au nmeelewa vby mkuu.
Mkuu kwa mara nyingine niruhusu nikupongeze. Huwa napenda sana style yako ya uandishi ikisindikizwa na reference na facts kutoka vyanzo mbalimbali.Hujuma ndani ya serikali, hawataki kushirikiana asema Katibu Mkuu Kiongozi Hussein Katanga na akashangaa wizara kutofanya kazi kama serikali moja.
TCRA na wizara ya Tekenolojia Hawajui bando hutumika hata vyuoni wanafunzi kupata lecture na material, tele-health video conferencing kwa huduma za afya n.k
Hivi TCRA na wizara mama ya Tekenolojia waliwasiliana na wizara ya elimu, elimu ya juu au wizara ya afya, Wizara ya Biashara na Mapinduzi ya Nne ya Viwanda / Fourth Industrial revolution ktk uzalishaji, masoko , uendeshaji viwanda n.k na kujua umuhimu wa bando nafuu au waliangalia tu Idara ya Maelezo propaganda ya Dr. Abbas ilivyonuia na inavyotaka kama ktk utawala wa mwendazake John Magufuli (RIP) kubana tu maoni ya wananchi ktk kupashana habari na medani ya siasa?
Wanataka kutuchelewesha hawa wafuasi wahafidhina wa mwendazake waliobaki kina Dkt. Hassan Abbas, Msemaji Mkuu (MAELEZO), TCRA, wizara mama na wale makada wa mtaa wa Lumumba Ofisi Ndogo.
View attachment 1741608www.cnn.com
Africans face most expensive internet charges in the world, new report ...
View attachment 1741609
22 Oct 2019 — Citizens of Chad, DR Congo, and the Central African Republic must all pay more than 20% of average earnings
.................................................................
Mbinu za maendeleo katika mapinduzi ya nne ya viwanda : Total Change
Ukisoma hiyo barua inakwambia toka February hayo maagizo yalitoka, Ina maana Hayati ndio alilitengeneza hili jambo Mama limemwangukia tu.
katika hili la kupandishwa kwa gharama za vifurushi wa kilaumiwa sio mama samia, ni mwendazake.
Mwendazake alikuwa hapendi kukosolewa, alionyesha chuki ya wazi kabisa kwa watu waliokuwa wanamkosoa kupitia mitandao ya kijamii. Akafikia hatua ya kutamani malaika washuke wazime mitandao yote.
washauri wake kwa kutambua chuki ya wazi ya boss wao kwenye mitandao, wakaona bora wamfurahishe, wakaja na idea za kutumia vpn kwa upande wa twitter (japo haijasaidia) na kuongeza gharama za vifurushi.
Matokeo ya idea hizo ndio hii bei mpya ya kikatili ya vifurushi. ndungulile na team yake walisukumwa zaidi na utashi wa kisiasa kuliko utu ili wamfurahishe boss wao ambaye kwa sasa ni marehemu.
sina shaka na Mama Samia, najua atafikishiwa malalamiko kuhusu vifurushi hivi vya sasa ambavyo sio rafiki kwa mwananchi mwenye kipato cha chini na haraka sana atatoa amri ya kuvisitisha.