Baada ya Malalamiko ya wananchi, Serikali yasitisha bei mpya za vifurushi

#BREAKINGNEWS Serikali imesitisha gharama mpya za vifurushi hadi hapo baadae.Imeangiza vifurushi vya zamani kuendela kutumika.

 

asante mama samia kwa kusikiliza kilio chetu.
 

Kwa hili kosa ilitakiwa Dr Faustine Ndugulile ajiuzulu mara moja kwa kudanganya umma ,alishupalia kwamba gharama zitashuka za data kutoka sijui Tsh 50 hadi 2 mpaka 9 Tsh ,cha ajabu gharama zime double , yaani 1000 napata MB 350??? 10000 GB 4 kutoka GB 12? TCRA inabidi wakusanye maoni upya maana tunarudi nyuma ,nchi nyingi gharama za internet zipo chini sana ila huku wanazidisha.

Na pia wasiangalie gaharama kubwa za data ,waangalie pia Mobile Money ,tozo za kutuma na kutoa pesa ni kubwa sana ,kila siku tunaona makampuni wanatoa records zao za faida kwa kuwakamua wananchi...imagine voda inaingiza mabilioni ya shillingi kwa mwezi kutoka kwenye Mpesa yaani wanatengeneza faida maradufu kwenye Mpesa,why TCRA wasi regulate faida kama EWURA wanavyoregulate price ya mafuta? How Mpesa waingize faidi ya zaidi ya bilioni 15 kwa mwezi? Huo si wizi? Kwanini gharama za kutuma na kutoa wasipunguze?
 

Walitaka to Kumfitinisha ( Kumgombanisha ) Rais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan na Watanzania ili aonekane mbaya na hafai kisha sababu ipatikane.

Wakasahau kuwa huyu Mama ni Mwanamke Mwerevu, Mjanja, ana Exposure Kubwa, Mtoto wa Mjini vile vile halafu siyo Mshamba ( Mbwiga ) kama wengineo hivyo nae kawawahi mapema mno.

Na kutokana na Upuuzi huu huenda Siku ya Jumanne ijayo Mtu au Watu yakawakuta makubwa kiasi hata cha kuweza Kugharimu Vyeo vyao kwani Kitendo walichokifanya Leo kilikuwa ni Kuwakomoa na Kuwakandamiza Watumiaji Simu Wanyonge wa Tanzania.
 
Samia oyeee.Ndugulile ondoa idea za Magufuli. Magufuli alitaka kupandisha vifurushi ili watu wasiingie mitandao ya jamii,ili wasihabarike. Maana mitandao ya jamii ndo source ya habari. Magufuli kafa. Acheni kufufua idea zake za kijinga.
 
Aisee!!

Sema tu kwamba, kutukana ni Matumizi mabaya ya akili!!

Serikali hongereni kwa hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…