Baada ya Master J kumkejeli Ali Kiba kuwa ni mbana pua, Ali Kiba ajibu mapigo

Usiseme kapaniki, kama yule alikuwa free kusema vile basi hata Ali yupo sahihi kureact
Jibu kwa Kazi si kwa maneno kuna nyimbo moja inaitwa taita - sugu ft bilnas

Kuna mstari ndani sugua anasema "walisema wife wangu mgumba sikuwajibu nikawajibu kwa mimba
Sahivi watoto wapo kwenye mjengo wanabadilishana tu vyumba"
 
Jibu kwa Kazi si kwa maneno kuna nyimbo moja inaitwa taita - sugu ft bilnas

Kuna mstari ndani sugua anasema "walisema wife wangu mgumba sikuwajibu nikawajibu kwa mimba
Sahivi watoto wapo kwenye mjengo wanabadilishana tu vyumba"
Kazi gani? Kwanini huyo anaekaa kuwaongelea wanaume wenzake asitoe kazi yeye zikawa kama mfano?
 
Mmeanza wazee wa kukariri

Shule muhimu +exposer
 
Kwanini asitoe yeye huyo anaekaa kukosoa wanaume wenzake na akapige hizo show yeye watu waige mfano toka kwake?
 
Mtoto wa Tandale ameshazoea kitukanwa,kuongelewa vibaya na angekuwa anajibu sizani kama angefika alipokuwepo leo.
 
Utakuaje Mwanaharakati wa muziki wakati Una akili kiduchu na unaropoka .

Yaani mropokaji Kama huyo unamuita Activist ?

Kama Una namba yake mwambie aache wivu na chuki awaache vijana watengeneze hela .

Kila msanii ana ladha yake katika huu muziki.
Mj hajawahi na kamwe hatokuwa na akili kiduchu. Kwenye ulimwengu wa muziki, watu wa zamani kukosoa na kutoa maoni kwa wasanii wapya si kitu kipya

MJ anaongelea vitu technical kimuziki, sio chuki kwa hiyo mtu asieujua muziki anaweza ona kama anawachukia kizaxi kipya cha muziki japo stage ya Trace imeonesha chochote alichosema alikuwa sahihi. Alichosema si uongo Ila kaongelea katika njia isiyo sahihi
 
Hata wewe ungekuwa judge sidhani harmonize yule ungemkubali. Na bongo star search sio shindano la biashara ya muziki ni shindano la VIPAKSA. Kwa hiyo inabidi uwe na kipaji kuingia

Na BSS imetoa best vocalists wengi ambao si harmonize wala K2Ga wanaweza kaa nao level moja kimuziki.

Harmonize kapikwa kwa showzbiz na anaweza tengeneza mashairi na melodies Ila kwenye kuimba. Hawezi kukaa kwenye sentesi moja na Peter Msechu au Bella Kombo

Tatizo mnaongea kihisia, master anaongea vitu technical
 
Haihitaji Bongo yaani pale ni simu kuyoka London ku-terminate contract! Ali Kiba ana shida hata alivyoondoka Trace Zanzibar ni scandalous!
Watu wanamtetea sana Ila ukiangalia interviews zake na za Manager wake Seven. Utajua jamaa ana humbleness ya kipwani Ila ndani kaficha mengi sana
 
Overrated producer

Rose Muhando album ya kwanza, Twanga Pepeta, hadi Kijitonyama choir "Hakuna Mungu kama Wewe".. Hapo hujaigusa catalogue yake ya Bongo flava

Brother, jamaa ni smart na ana exposure.

Wewe naona ni Ali Kiba Fan ndio maana umeichukulia personal. Master Jay yawezekana kakosea mara nyingi but huwezi ondoa impact yake kwenye muziki wa Tanzania.. He is one of the best if not the best versatile producer ashawahi kanyaga bongo hii
 
Alikiba akerwa na Master J baada ya kukerwa na kuchoshwa na tabia ya Master J kujifanya anafahamu sana muziki kwa kuwasengenya wasanii wa Tz

Alikiba alikereka na kauli ya Master J iliyoruka hewani kuwa Alikiba ana bana sana pua kama Wahindi kitendo ambacho kinaonesha watu kuwa Master J ni mtu mwenye dharau mwisho wake ni kushushiwa heshima na wasanii

Ikumbukwe kuwa Master J anaonekana ni mtu mwenye roho mbaya na chuki kwa wasanii kwasababu tangu tumfahamu amekuwa mtu wa kuwadharau vijana wenye kipaji cha kuimba BSS

 
Ms

Master Jay is negative person

Yawezekana alifanya mambo Makubwa katika muziki Ila anabidi kuwekeza katika #Positivity .

Kumkosoa mtu Kwa lengo la kumjenga sio mbaya Ila alichofanya juzi Kati kazingua .

Japo Alikiba amekosea kuongelea upinde Ila Master Jay kazingua kiufupi wote wameonesha immaturity
 
Domo,ally kiba harmonize wote hamna kitu kwenye live performances
 
Wote wamezingua πŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎ
 
Ali kachagua toa wembe nitoe kisu

Sijui hata kama unajua msamiati wa kebehi wa kubana pua ulinzia wapi?
 
Wote hao wawili wanazeeka vibaya
 
Kwani kama anabana pua na washabiki wake wanapenda tatizo liko wapi?
 
Ally ana nafuu kubwa kuwazidi hawa wengine kuimba live ashaimba live nikiwepo sema tu Bien ni kiboko jamani ,master J alitakiwa aongee kwa usawa anapenda mno kukosoa anakeraa
Mario ndio nilicheka jamani hana pumzi kabisa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ wafanye mazoezi jamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…