Baada ya Master J kumkejeli Ali Kiba kuwa ni mbana pua, Ali Kiba ajibu mapigo

Baada ya Master J kumkejeli Ali Kiba kuwa ni mbana pua, Ali Kiba ajibu mapigo

Ali Kiba sio mbovu kwenye kupeform live lakini sio kama ana sauti powerful kama ya Bien..
Nadhani master alichokosea ni kuongea kwa kumshusha Ali kiba kupita kiasi na Ali Kiba nae amejibu kiswahiliswahili na kwa jeuri kubwa ambayo huwa anaificha kwenye ukimya wake.
Angekosolewa mtoto wa Tandale wala asingeangaika kujibu kabisa, kwasababu huwa ni sehemu ya maisha yake kimziki. Ila kwa kuwa kakosolewa mtu ambaye hapaswi kukosolewa, mfalme wa mziki wa bongo fleva, basi jamaa ameona Master J kamkosea heshima na kaamua amtukane kimtindo kabisa 🤣🤣🤣.
 
Kumuita master jay ni upinde tayari kamchafua lakini pia imemshusha Ali kiba kwa level mbaya sana. Mitandaoni atapigiwa heko, ila kwa watu wenye ufahamu anaonekana amekosa emotional intelligence
Sasa jiulize waliompa u-ambassador Stanbic ni nani haswa? Na msimamo (policy) wao juu ya kunyanyapaa watu wa upinde ukoje? Ukiwa artist kuwa mwangalifu na unachoandika! Sitashangaa akiondelewa u-ambassador!
 
Angekosolewa mtoto wa Tandale wala asingeangaika kujibu kabisa, kwasababu huwa ni sehemu ya maisha yake kimziki. Ila kwa kuwa kakosolewa mtu ambaye hapaswi kukosolewa, mfalme wa mziki wa bongo fleva, basi jamaa ameona Master J kamkosea heshima na kaamua amtukane kimtindo kabisa 🤣🤣🤣.
Naona huko X wameanza kumripoti kwa Stanbic bank kama balozi wao😂😂
 
Master J ana jealous ana ile kitu inaitwa Crab Mentality
(kaa kwenye ndoo.) Maana anajariibu kuongelea vibaya watu ambao wame-hustle Kwa jasho na Damu kujenga brand zao na Leo they made it

Unaweza kuona kupitia vijana Kama Alikiba jinsi walivyoubadilisha muziki na Kuwa biashara kubwa na kutoa ajira rukuki
Bila shaka hunjui MasterJ vizuri.
Ni kweli ni mropokaji lkn hana wivu wowote.
Jamaa amenyooka sana.
Alichokosa ni ile hekima but jamaa ni mzungu sana tu.

Watuvwa Tangagiza na wapenda unafiki kamwe hawawezi kumwelewa wala kumpenda MasterJ
 
Aliyehaso kwa jasho na damu kujenga brand ni Diamond tu.
Sure.
Tena juzi Diamond alimwambia MaaterJ face to face kuwa huwa ukosoaji wako japo ni mchungu lkn nauchukulia ktk positive way
 
Katika kukosoa kuna kitu kinaitwa

Constructive criticism na destructive criticism.

Sasa unapozungumzia EI Emotional intelligence ambaye hana hiyo kitu ni master J kutokana na umri wake mkubwa lazima awe anatumia Sana akili kuliko hisia na na akiwa amelewa pombe ajizuie kufanya interview

Maana msanii ambaye anafanya mziki wake zaidi ya maika 18 Kama A -list iweje Leo hii useme hajui kuimba

Alikiba alichojibu sio sahihi Ila itamfanya huyo master j next time asiwe mtu wa kuropoka

Hakuna sehemu nimesema master j alikuwa sahihi ila aliongea kitu sahihi katika namna ambayo si nzuri..

Kingine mkuu kuwa juu kimuziki ni package kubwa kwa hiyo kuimba Ali Kiba anajua lakini hana vocal supremacy waliyonayo wasanii wengi tu ambao hawana level ya mafanikio yake.

Nikikuuliza Ali Kiba unaweza muweka kwenye Top 5 ya best vocalist wa bongo flava au watunzi wakali zaidi, ??

Jibu ni HAPANA, kwa hiyo master hakukosea sana kumuweka Ali Kiba kwenye Category za wahindi na waarabu maana sauti yake ina mahadhi hayo. Huwezi muweka Bien na Ali vocally kwenye category moja japo Ali ana mafanikio kumzidi Bien
 
Sasa jiulize waliompa u-ambassador Stanbic ni nani haswa? Na msimamo (policy) wao juu ya kunyanyapaa watu wa upinde ukoje? Ukiwa artist kuwa mwangalifu na unachoandika! Sitashangaa akiondelewa u-ambassador!
Mkuu hayo unayoyaongea kwa wasanii wa bongo ni ndoto kwa sababu wengi hawana hiyo level ya professionalism na bongo hatupo sensitive sana na vitu vingi. Ndio maana Diamond anafanya vitu vingi na bado anapewa endorsements nyingi. Angekuwa nchi za magharibi angeshakuwa cancelled
 
Huyu jamaa sijui huwa shida yake ni nini, huwa anaimba ila wala hayuko comfortable ndio maana kuna baadhi ya key hawezi kupanda... Sauti yake ni kama huwa inaanzia kwenye koo kwahiyo inamfanya atumie nguvu nyingi kwenye kuicontrol.

Inabidi awaprove watu wrong kwa hilo... Mimi ni fun wake ila akiimbaga huwa sipendi apande keys kwasababu huwa naofia asije akawika bure.
 
Master J yupo sahihi
Tatizo ni namna alivyo wasilisha hoja zake.... kuna kebehi ndani yake

Kwa level ya Master J anapaswa kujua jinsi watu walivyo hustle kujenga brand zao kupitia muziki
So unapo toa maoni yako toa kwanjia za kiungwana

Namuelewa kwanini Kiba amekasirika na yeye akajibu mashambulizi
Alikuwa kashautwika si unajua lugha za kilevi zile? Haki ya mama Ali Kiba angekuwepo pangezuka vita yaani kwa zile kejeli Unaweza ukamchapa kofi aisee!
 
Mkuu kwenye ulimwengu wa Bongo fleva “kubana pua” ni tusi kubwa sana...... ni vile tu watu hawajui

Yes Ali Kiba ana ego lakini katika hili amechokozwa na akakasirika
Mtu akikasirika akishindwa kujizuia anakupa za uso ili mradi na wewe uumie

Master J asinge ropoka unadhani Ali angemtusi kweli?

Toka Ali Kiba anaanza muziki walimuita mbana pua kama wasanii wengi tu wa bongo flava mwanzoni..
Japo master jay hakutakiwa kusema hayo lakini pia Ali Kiba amedhihirisha alivyo mweupe kichwani. Kwa msanii ambaye watu wanaona anajiheshimu, kutoa majibu ya kiswahili si sawa

Au wewe unaona sawa kumuhusianisha master jay na ushoga. Kwa nini asingemjibu kimuziki kama Master alivyofanya
 
Mkuu hayo unayoyaongea kwa wasanii wa bongo ni ndoto kwa sababu wengi hawana hiyo level ya professionalism na bongo hatupo sensitive sana na vitu vingi. Ndio maana Diamond anafanya vitu vingi na bado anapewa endorsements nyingi. Angekuwa nchi za magharibi angeshakuwa cancelled
Haihitaji Bongo yaani pale ni simu kuyoka London ku-terminate contract! Ali Kiba ana shida hata alivyoondoka Trace Zanzibar ni scandalous!
 
Ubaya live show zao unakuta wanabadiri Ala za muziki.

Ukifuatilia show za wenzetu live band inapiga kama Audio ilivyo.

Sasa sikia hiyo live show ya kiba. Drums zinapigwa tofauti kabisa na audio ya huo wimbo. Sexaphone inapigwa tofauti yaani hupati ile ladha iliyoufanya wimbo ukapendwa
Kiba hayupo comfortable kwenye kuimba, watu wote ambao wako na idea na muziki wanaelewa hivyo, keys ameziimba mwenyewe huko studio ila akija live hawezi kuzipanda na akipanda lazima awike😅😅😅 (hii sio kwa ubaya ila ndio uhalisia)

Wanatakiwa wakubali na wajifanyie improvement kwenye hilo eneo ili wawe Bora zaidi.

Mtu ambae huwa anajitahidi kwenye live band ni Mbosso, katika hao wasanii wa bongo fleva ambao wanasikika mara kwa mara.
 
Ni kweli Ali Kiba ni mbana pua.

Ni kweli Ali Kiba hawezi kufanya aina ya muziki anaofanya Bien.

Ni kweli kabisa Bien kamwacha Ali Kiba kwenye ubobevu wa Multiple Music Genres.

Ni kweli wasanii wengi wa Bongo hawawezi kufanya Live Performance and Theatre Music.
 
Tatizo Master Jay mziki anaujua. Am sorry king, he got you this time.

Sema na wewe Master jiheshimu. Profile yako ni kubwa sana kuzungumza kama ulivyozungumza. Ni kama umemtukana Kiba ungeweza kutetea hoja yako katika namna nyingine bora zaidi ya hiyo.

Kiba naye kapanic kajibu kama msela wa Manzese.
Huyu ni kawaida yake kutoa maneno ya shombo na dharau juu . Kama ameona Ali haimbi vzr basi angetumia lugha ya heshima na siyo kama hivyo alivyosema. Amezidi muache apate za uso babu mzima hana hekima
 
Kiba hayupo comfortable kwenye kuimba, watu wote ambao wako na idea na muziki wanaelewa hivyo, keys ameziimba mwenyewe huko studio ila akija live hawezi kuzipanda na akipanda lazima awike😅😅😅 (hii sio kwa ubaya ila ndio uhalisia)

Wanatakiwa wakubali na wajifanyie improvement kwenye hilo eneo ili wawe Bora zaidi.

Mtu ambae huwa anajitahidi kwenye live band ni Mbosso, katika hao wasanii wa bongo fleva ambao wanasikika mara kwa mara.
Angeshauri hivyo kama wewe sidhani kama angetukanwa. Anazeeka vby huyu mzee .
 
Tatizo Master Jay mziki anaujua. Am sorry king, he got you this time.

Sema na wewe Master jiheshimu. Profile yako ni kubwa sana kuzungumza kama ulivyozungumza. Ni kama umemtukana Kiba ungeweza kutetea hoja yako katika namna nyingine bora zaidi ya hiyo.

Kiba naye kapanic kajibu kama msela wa Manzese.

Kwasasa sio master ni Upinde Jay
Amejibiwa kama alivyojibu 😂😂
 
Sio sawa Ali Kiba kumuita Master Jay ni shoga kisa kamkosoa. Hakuna tusi kwa mwanaume ni la kudhalilisha kama kuitwa shoga.
Yeye nae kwanini amzungumzie mwanaume mwenzake? Yeye ni nani hadi awe anatoa confirmation za mambo? Aimbe yeye basi. Namuunga mkono Ali, kumzungumzia mwanaume mwenzako ni ushoga
 
Back
Top Bottom