Baada ya matendo yake sina hisia nae tena, nifanyaje?

Umekuja kuomba ushauri huku....heeee kwa wanaume wenzieee tena wanaona kawaida ila ingekua ni wewe umefanya wote wangesema muache
 
Nilikwambia Kapeace wanawake hata mjue mume anachepuka ni ngumu sana kuwaacha waume zenu
Sio wote tuna uoga huo budaa, kwanza kujichua mbele yake ili iwe nini wakati mijulubeng ipo!!! Halafu ni suala la muda tu hiyo kulia katikati ya game ni mbaya mno na very soon kuna kijana wa ovyo atajipakulia minyama,
 
Huyo mumeo ni mshenzi wa tabia na ni mdhaifu mno hata hivyo una moyo sana kuendelea kuwa nae.

Kingine rafiki na mahusiano yako ni vitu ambavyo havipaswi kuchangamana, binafsi huwa sitak mazoea kabisa na mashem shem maana najua balaa lake.
Kumbe na ushauri unatoa
 
Pole sana kwa unayopitia.
Machozi yanayokuja katikati ya tendo ni ishara kwamba kuna sehemu ya moyo wako bado haijapona. Sawa kabisa kulia ni sehemu ya kuachilia maumivu.

Jitunze na ujipende mwenyewe kwanza (self-care)
Fanya vitu vinavyokufurahisha au vinavyokupa utulivu wa moyo vaa vizuri pendeza vaa na usuke fashion pia inasaidia.

Usilazimishe kusamehe haraka
Kusamehe si jambo la ghafla, ni mchakato. Pia, kusamehe haimaanishi kwamba unasahau aliyotenda au kurudisha hali kama ilivyokuwa. Inaweza kuchukua muda mrefu, na hiyo ni sawa.

Chukua muda wa kutafakari maisha yako ya mbele. Je, bado unataka kuendelea na ndoa au lah.. Unajiona ukipata furaha tena ndani ya ndoa yenu?

Kumbuka kuwa Afya yako ya akili ni ya muhimu sana, na unastahili amani na furaha, hata kama itabidi kuchukua muda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…