Ni wazi kabisa CCM ndiyo inayokwamisha mchakato mzima, ukianzia pale mheshimiwa alipoendakutoa maoni yake mbele ya bunge la katiba na kulazimisha kwamba kama selikari tatu tusubiri yeye atoke madarakani, hii maana yake nini , yaani wabunge wa chama chake lazima wasimamie maelekezo ya mwenyekiti wao kwa gharama yoyote ile.hivyo basi aliye kwamisha ni CCM kwa kutaka kuleta kitu kipya ili kumuunga mkono mwenyekiti. pia mwenyekiti wa bunge lile muheshimiwa 6 pia hana nia ya kuwaletea watanzania katiba mpya kwani alikuwa akikalia kiti kimya na akiangalia wajumbe wakitukanana na lugha za matusi sasa leo anatafuta maridhiano gani.