Baada ya Mdahalo: Nani anazuia upatikanaji wa Katiba Mpya?

Baada ya Mdahalo: Nani anazuia upatikanaji wa Katiba Mpya?

Baada ya mdahalo uliokusanya Itv juu ya wananchi kujua nani anataka kuwazuia watanzania kupata katiba Mpya.

Je sasa unaweza kutoa jibu ulilopata?

Karibu....

Wewe Hukuona Aliyekuwa Anazomewa?? Yule Na Chama Chake Ndo Hawawatakii Mema Watz
 
Kwa hoja zipi?

kama nikwakupiga kelele hata mtoto mdogo akigongwa sindano ikamwingia hufunika kwa kelele waaah, waah watu wakapigwa butwaa na kutatizwa na mayowe.

Wassira kashushiwa nondo kapaniki

moja ya swali lilomshinda .ni hili

Dr shein anapigiwa mizinga kama nani kule zanzibar? unakumbuka alijibu nini.............leta majibu.

hoja inayosumbua wengi hapa ni muundo wa serikali tu, xo mbona vipengele vingi vinarekebishwa kwa nini serikali tatu kama haina mashiko tusiitupilie mbali?
ukifuatilia kwa undani cio mambo yote yaliyopendekezwa a wananchi yalichukuliwa na tume kazalika cio yote waliyokuja nayo tume yawepo kwenye katiba.
 
Wassira Kaniuzi Sana, Eti Kwavile Walopendkeza 3 Ni Wa Kigoma Kwahyo Maoni Hayo Hayafai, Hiv Alitaka Yatoke Mkoa Gan Ndo Akubali Au Kigoma Siyo Tz??
 
Tena huyo jamaa ndiyo alitema pumba zaidi pale alipoingiza propaganda kwenye upatikanaji katiba mpya, pale aliposema kuwa waTz, hawahitaji katiba mpya, badala yake ukiwagawia fulana, khanga na kofia, basi itakuwa poa kabisa, kwani watakuwa weshapata maisha bora, kama walivyoahidiwa na JK!
Ndiyo haya ya kufunga tovuti ya tume huru ya katiba. Kwa nini mmeitoa hii topic harakaharaka hivi, mmeshatishiwa na mahitarahamwe!
 
Kwenye mdahalo wa leo live ITV, Wassira akiwa peke yake dhidi ya Prof.Lipumba,Tundu Lissu,Humphrey Polepole na mashabiki wa ukawa mdahalo ulikuwa Moto.

Mpaka mwisho wa Mdahalo Wassira has become the Man of the Match, Lissu kaaibika na Lipumba akaishiwa Takwimu.

Wassira kawabwaga ukawa kwa aibu kubwa huku ukawa wakibaki kulialia kuwa wanataka kuonana na Rais.
 
tundu lissu anasema tupige kura ya kutaka muungano au la? kazaliwa 1968 muungano unamhusu nini?

Khaa!! Una akili kichwani au makamasi? Hata mtoto aliyezaliwa leo muungano unamhusu! Unafikiri muunagano unawahusu waliozaliwa kabla ya 26-04-1964 tu?? Kapimwe akili yako wewe sio mzima.
 
Dah! Tulikuwa tunaangalia ITV wote au wengine tulifanywa viini macho? Mbona Wassira alizidiwa pamoja na kubebwa sana na da Rose? Wewe hukumuona Wassira akipandwa na Jazba mara kwa mara? Hoja ipi ya maana aliyoweza kuipangua? Mbona zote zilimuelemea mwanzo mwisho? Kuwa mkweli wa nafsi yako utakuwa huru ndugu yangu... CCM hawachomoi this time...
 
Nilikua Nafatilia Kwa Ukaribu Mdahalo Wa Katiba.. Katika Hali Ya Kushangaza Na Kusikitisha Mh Masatu Wasra Amesema Kwamba Maoni Mengi Ya Kutaka Serikali 3 Yalitoka Kigoma Tu... Hivi Inamaana Kigoma Siyo Tz?? Je Sisi Wakigoma Hatuna Haki Ya Kutoa Maoni Ya Katiba?? Au Yeye Alitaka Maoni Yatoke Mkoa Gani Ndo Ayakubali Kwamba Ni Ya Wanainchi?. Watu Wa Kigoma Tumekua Tukibaguliwa Sana Kwamba Ni Wakimbizi, Je, Wasira Anataka Kutoa Ujumbe Kwa Watu Wa Kigoma Kwamba Siyo Watanzania?? Naomba Kutoa Hoja..
 
Nilikuwa ndani ya ukumbi kwakweli vijana wa chadema wamejiaibisha sana, wanapiga kelele zisizokuwa na maana, uchunguzi umeonyesha kuwa vijana hao wamelipwa kwa kukaa Bagamoyo siku tatu na wamesombwa kwa coster mbili kutokea huko.

Wassira has made the Tanzania mass aware.
Ukawa wameburuzwa kwa hoja zilizojaa afya.
 
Huwa natamani ningesomea upasuaji vichwa, ningependa sana kufahamu kilichomo kichwani mwa mleta mada. Loh!
 
Nilikua Nafatilia Kwa Ukaribu Mdahalo Wa Katiba.. Katika Hali Ya Kushangaza Na Kusikitisha Mh Masatu Wasra Amesema Kwamba Maoni Mengi Ya Kutaka Serikali 3 Yalitoka Kigoma Tu... Hivi Inamaana Kigoma Siyo Tz?? Je Sisi Wakigoma Hatuna Haki Ya Kutoa Maoni Ya Katiba?? Au Yeye Alitaka Maoni Yatoke Mkoa Gani Ndo Ayakubali Kwamba Ni Ya Wanainchi?. Watu Wa Kigoma Tumekua Tukibaguliwa Sana Kwamba Ni Wakimbizi, Je, Wasira Anataka Kutoa Ujumbe Kwa Watu Wa Kigoma Kwamba Siyo Watanzania?? Naomba Kutoa Hoja..

Mngemuuliza Wasira: Na waliotoa maoni ya serikali 2 wanatoka mkoa gani?
 
Back
Top Bottom