Baada ya miaka 39, Taifa Stars yafuzu kucheza michuano ya AFCON 2019 baada ya uicharaza Uganda goli 3-0, Uwanja wa Taifa-Dar

Baada ya miaka 39, Taifa Stars yafuzu kucheza michuano ya AFCON 2019 baada ya uicharaza Uganda goli 3-0, Uwanja wa Taifa-Dar

Hivi kwa akili yako unadhani stars wangefungwa kama Makonda asingeweka hayo maneno yake?
 
Haya mambo mengine tungetumia busara kwa kukaa kimya yangetusaidia maana safari bado ni ndefu.
Msuva, Samatta, Nyoni, Boco nk ni zaidi ya kamati na ni kuwaundermine kwa kusema kuwa walichokifanya ni kwa sababu ya hizi siasa. Haya tuelezeni na Mwakinyo ni kamati ya nani!?
 
Waliopata kutumia vinywaji kwa nusu punguzo watoe mrejesho ilikuwa wapi? au hapo big brain hakumaanisha?
 
Nakereka sana kila naposikia kila kiongozi anazungumza kuhusu hii mechi ya Taifa stars na Uganda akinza kwa kumpongeza rais wetu mpendwa Magufuli.
Nachojiuliza Magufuli anapewa pongezi ya kazi gani? Kati ya Magufuli na mashabiki na wachezaji ni nani wa kwanza kupewa pongezi?
Huu ni ujinga wapeni pongezi wachezaji na mashabiki kwa kufika na kucheza vizuri Magufuli hana hata chembe ya pongezi kwenye mchezo huu... Bora hata Makonda alikua kwenye kamati na kiki zake za msimu...


Sent using Jamii Forums mobile app
JPM mwenyewe amesema alicheki mechi nyumbani kwake ksb alikuwa ana wasiwasi na timu. Japo alinishangaza jinsi anavyovaa akiwa nyumbani au kuna shamba ikulu? Wajuzi mtujuze?
 
Hata ungepewa wewe jukumu lile la kuhamasisha ungeshindwa?

Funzo kwa maccm Magufuli akiwa muungwana Taifa linaweza kusimama pamoja kama jana, aache kuwagawa Watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na anaweza kuwaunganisha watu kupitia huu mpira, watz wanapenda sana soka.
 
Yeye ndio Mkuu wa Nchi

Kila Jambo likivurugika Kwenye Nchi Lawama anapewa Rais Kwanini likikaa sawa tusimsifu?

Hongera Dkt Magufuli kwa ushindi mfululizo kuanzia wa Simba, Hasana Mwakinyo Na Leo Taifa Stars

Wanafiki wakiongozwa Na Da Mange wameumbuka
Ingefungwa wangekuja na ngojera za oooh LAANA, mara mikono yao imejaa damu mara Mungu hadhihakiwi na porojo kibao.Ukisoma post zao kabla ya mechi utaona hawa jamaa ni wa kupuuzwa. Walikua wanashabikia Uganda na Lesotho, Mungu si mange kimanbe wameumbuka balaa .

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Mkiwa na kiongozi mkuu ambaye hataki siasa anataka kazi tu ,mambo yote hubadilika kutoka juu mpaka chini ,tofauti na tulivyokuwa tunaaminishwa na baadhi ya wasomi hasa Chadema kwamba rais hata akiwa mwizi ,mvivu mzururaji mambo yataenda tu kisa eti urais ni taasisi?

Katika sekta ya michezo asante Taifa stars, Simba na bondia Mwakinyo

Asante kasi ya Rais Magufuli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo ni coincidence tu.
1-Kwa Taifa Stars ushindi wetu umetokana kwanza waganda wamesha-qualify hivyo hawakuwa na haja ya ushindi, pili hata kama tungemfunga Uganda magoli 10 na Lesotho angeshinda ingekuwa ushindi wetu ni wa bure tu.
2-Kuhusu Simba SC wa kupewa credit ni Mo Dewji ambaye anaigharamia club na kuhakikisha timu inafanya vizuri.
3-Hassan Mwakinyo kama alivyosema mweyewe ame-struggle kivyake mpaka amefika alipofika.
Tuache kutumia siasa katika michezo, usitake kuwafanya wanamichezo wote ni wanachama wa CCM, unaweza kufanya perfomance yao kuteremka.
Tumeona tu kamati ya uhamasishaji ya Taifa Stars ikiongozwa na baadhi watu wa CCM kuna watanzania walikuwa wakiiombea timu yetu ifungwe.
Kama tunavyosema tusichanganye dini na siasa, hivyo hivyo tusichanganye michezo na siasa.
 
Hivi ulichoandika umekifikira kwanza? Au ofa za Makonda zinaongea? Mbwa ww, Mbowe anahusikaje kwenye mada hii?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mbona UNATESEKA?Sifa zote ziende kwa Jpm hutaki kanywe sumu.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
JPM mwenyewe amesema alicheki mechi nyumbani kwake ksb alikuwa ana wasiwasi na timu. Japo alinishangaza jinsi anavyovaa akiwa nyumbani au kuna shamba ikulu? Wajuzi mtujuze?
Hahahahahah ile dressing code ni shida.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Uchaguzi huwa unakuja na mengi.. Yaani ikifikia kipindi hiki tunashuhudia mengi sana. Ila mengi ni ya kuwatengenezea njia baadhi ya watu waendelee kuitafuna keki ya taifa pasi na shaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
A
Ushindi wa goli 3 kwa 0 ilioupata timu ya taifa stars leo dhidi ya Uganda na hivyo kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Nchi za African@ AFCON zitakazochezwa Misri mwezi June mwaka huu ni uthibitisho mwingine kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mh Paul Makonda ni hadhina kwa taifa kwenye upangaji na usimamizi wa masuala ya kitaifa.

kwa faida ya wengi ni kwamba Mh Makonda alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya kuiwezesha taifa stars kufuzu AFCON 2019 ambapo pamoja na mambo mengine ilikuwa na jukumu la kushirikiana na Uongozi wa timu kubuni mbinu na mikakati ya kiufundi ndani na nje ya uwanja, bila shaka kwa matokeo yaliyopatikana inahitaji kiburi na husuda na wivu kupinga kwamba hajafanikiwa.

Jukumu lingine kubwa lilikuwa ni kuhamasisha Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia timu ili kuwapa nguvu na hamasa wachezaji ya kupambana na kushinda. Katika hili la kuhamisha watu kujitokeza tumpe Kongole Makonda kwa niaba ya kamati aliweza kuwaunganisha watu maarufu kutoka tasnia za muziki, filamu, wanamitindo, wanasiasa na kuwaomba kutumia vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii kuhamisha wananchi na matokeo yake yameonekana uwanja ulijaa yaani zaidi ya watu 60,000 walikuwepo taifa.

Kwa kurejea baadhi ya mambo mengine mengi ambayo mhe Makonda amewahi kufanya;-

## kufanikisha kama kusaidia Walimu katika Mkoa wa Dar es salaam kupanda daladala bure,

## kufanikisha upatikanaji wa bima za afya @ toto kadi kwa mamia ya watoto ambao wametelekezwa na wazaz.

## kuwapatia viatu bandia walemavu, kuchangia matibabu ya wagonjwa mbalimbali nje ya Nchi.

## kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi zinazohusu ardhi na kuwasaidia wakina mama hasa wajane waliodhurumiwa Nyumba na mashamba.

## kupanua huduma za kijamii kama vile ujenzi wa hospital Temeke, shule za sekondari na Msingi hivyo kuwawezesha wananchi na wanafunzi wengi kupata huduma.

Makonda ni binadamu pamoja na mafanikio hayo Lukuki aliyofanya katika kipindi kifupi ambacho amekuwa mkuu wa Mkoa yaweza kuwa kuna mapungufu ya hapa na pale amefanya lakini hayaondoi ukweli kwamba amejitanabaisha kuwa ni asset kwa taifa letu.
lifunga magoli mangapi vile?
 
Back
Top Bottom