Huyu Selasini ni ''project''. Baada ya kuihujumu NCCR akisaidiana na Msajili sasa ana project ya CHADEMA
Selasini anasema CHADEMA wanatakiwa kuingia hayo Maridhiano. Hivi nani amewakataza CCM na Serikali yake kufanya maridhiano na Wananchi? CHADEMA hawakushiriki uchaguzi sasa wanaenda kujadili nini
Pili, maridhiano ni kuhusu nini! na akina nani wanatakiwa kuridhiana. Hakuna anayejibu
Selasini ni mamluki na hili la HECHE lina mikono mingi. Kinachotakiwa ni kumuondoa Heche ili waje vibaraka zipatikane picha zipelekwe commonwealth na Nchi za magharibi
Kitu kimoja CCM na Serikali yake hawakitambui. Hivi ni kwanini CHADEMA wanaungwa mkono na UMMA kwa kukataa maridhiano ? Kuna nini katika Umma ambacho CHADEMA wanapata uungwaji mkono nacho
CCM na Serikali yake waliingia uchaguzi na vyama 16, wakatoa magari na kila msaada. Vyama vikasaini kukubali matokeo. Sasa maridhiano ni ya nini na wale waliosusia uchaguzi?
Kwanini CCM isikae na vyama 16 n kutengeneza maridhiano! au CCM isikae na wanachi.
Why mbinu hizi chafu za kununua watu kuivuruga CHADEMA. Hii mbinu imeshikiwa bango na CCM kiasi kwamba hata kama kweli kuna hicho wanachosema cha pesa, Wananchi wanaona wazi kuna hujuma. Hili limebuma watafute jingine na muda si mshiriki kwao.
JokaKuu