Baada ya mshahara kutoka watu wenye harusi wameanza simu

Baada ya mshahara kutoka watu wenye harusi wameanza simu

Me nadhani watakua washanichoka kwenye magroup ya michango sasa.. Maana napokea tu kadi ninapotupa hata sikumbuki
Siku hizi wala sipokei, namwambia hamna shida ujumbe umefika usipoteze kadi, itumike kwa mwingine, tuendelee kuombeana tutaona kitakachopatikana wakati ukifika. Hongera sana. Atajua mwenyewe kama atafuta jina au ampe mwingine kwa jina langu. Ila ikifika natoa kisichoniumiza.
 
Tujifunze kusema HAPANA. Wanaume tunalaani wanawake wasioweza kukataa anamvulia yoyote ila unakuta kwenye sekta yetu ni hivyo hivyo, huwezi kukataa ukasema "SICHANGI" unatoa miahadi inayokuumiza.
Kwenye mambo ya kijamii kama haya,. Sio mbaya kuahidi ila iwe ndani ya uwezo,.
Huwezi jua wewe utamchangia kwenye sheree yeye atakuchangia kwenye ugonjwa..
Maisha ni kushirikiana na kushirikishana
 
Siku hizi wala sipokei, namwambia hamna shida ujumbe umefika usipoteze kadi, itumike kwa mwingine, tuendelee kuombeana tutaona kitakachopatikana wakati ukifika. Hongera sana. Atajua mwenyewe kama atafuta jina au ampe mwingine kwa jina langu. Ila ikifika natoa kisichoniumiza.
Mimi za watu ambao najua ni wakaribu na tunasaidiana kwa namna moja au nyingine napokea na ikibidi kuahidi naahidi iliyo ndani ya uwezo..
Ila za ambao siwafahamu napiga tu kimya
 
Kama walijuchangia basi huna budi kufanya hivyo. Ule mchango ni deni.

Kama hawakuchanga na wala huna mpango huo hapo baadae ukioa, basi waambie tu ukweli.

Kuja kulalamika jukwaani wakati ungeweza tu kuandika 'Ndugu Mwanaharusi, acha hela yangu ipoe. Bado ni ya moto'.
Kabisa
 
Ondoa 'vi bday party vya kichuochuo' sababu sijafika elimu ya chuo

Kadi zinaletwa, mara ya mwisho ni jana usiku tushafunga mlango mtu kaja kugonga katualika kwenye sherehe hela ya kijora ni 20k na kadi humohumo

Maza akataka kutoa nikamuita chobingo nikampiga mkwara kwamba atoe elfu 5k kama mchango hiyo 15k hamna kutoa kama kijora atavaa cha zamani ndani vipo vingi..!

Natoa kilicho ndani ya uwezo wangu
Maisha magumu..!
Walimletea mama na sio wewe kumbe..
Ukikua utaelewa
 
Kwenye mambo ya kijamii kama haya,. Sio mbaya kuahidi ila iwe ndani ya uwezo,.
Huwezi jua wewe utamchangia kwenye sheree yeye atakuchangia kwenye ugonjwa..
Maisha ni kushirikiana na kushirikishana
Upo sawa, ila huwezi mchangia kila mtu. Kuna watu huna hata ukaribu nao, uliye na ukaribu nae hawezi kukuumiza ukimchangia.

Sasa mtu umesoma nae sekondari drs moja miaka imeenda amechelewa kuoa anaoa at 45 huko anakupigia mpaka akukumbushe weee ukishamkumbuka ndo akupe hiyo ajenda kuwa ana kadi yako.
 
Nikue mara ngapi?
Huo ni mfano wa jana
Ningetaka ya zamani ningekupa inayonihusu
Sina utoto huo mimi hadi uniambie nikikua nitaacha
Bado hauko kwenye ile position unayotakiwa usimame wewe kama wewe binti,..
Anyways am sorry
 
Upo sawa, ila huwezi mchangia kila mtu. Kuna watu huna hata ukaribu nao pengine

Sasa mtu umesoma nae sekondari drs moja miaka imeenda amechelewa kuoa anaoa at 45 huko anakupigia mpaka akukumbushe weee ukishamkumbuka ndo akupe hiyo ajenda kuwa ana kadi yako.
Kama hao ndo wakuwakalia kimya,.. ila workmates na majirani na ndugu tunachanga
 
YANI KWA SASA HIYO FURAHA WABAKI NAYO TU WENYEWE..
Screenshot_20240517-162223.jpg
 
Mkuu kwenye zile kadi huwa hakuna sehemu inayosema mchango ni "lazima" ila huwa waandika wanaomba, ombi huwa lina matokeo mawili kukubaliwa ama kukataliwa. Sio lazima utoe unauchuna tu hakuna atakaekuja kukuhoji.
 
Back
Top Bottom