Baada ya mshahara kutoka watu wenye harusi wameanza simu

Baada ya mshahara kutoka watu wenye harusi wameanza simu

Daaah,

Inakata stimu kwa kweli. Yaani hata mama sijamrushia muamala. Yaani hata kuhemea bado napotezea ili mshahara upoe kwanza.

Yaani hata hela haijampumzika kwenye akaunti. Yaani hata mwenyewe sijajipa pole na tulizo la nafsi.

Wenye maharusi tupumzisheni jamani, wekeni bajeti kulingana na uwezo wenu sio kutegemea mishahara yetu
KIHASIBU: HASARA YA KUTUMA MICHANGO KABLA KUMTUMIA HELA MAZERI
 
Daaah,

Inakata stimu kwa kweli. Yaani hata mama sijamrushia muamala. Yaani hata kuhemea bado napotezea ili mshahara upoe kwanza.

Yaani hata hela haijampumzika kwenye akaunti. Yaani hata mwenyewe sijajipa pole na tulizo la nafsi.

Wenye maharusi tupumzisheni jamani, wekeni bajeti kulingana na uwezo wenu sio kutegemea mishahara yetu
mkuu ulilazimishwa kuchukua kadi
 
Mimi Huwa nawaaambia wenye harusi hivi,miaka au mwaka alijipanga kuoa na hakuniambia. Imebaki miezi mi 3 halafu ndo anakuja kunishirikish. Nawaeleza Waziri kuwa nishabanga mapato na matumizi ya mwaka mzima. Hilo la kwake limekuja ghafla
 
  • Nmeshapokea kadi 4, nimeamua kuchangia 1; hao wengine nimewaambia SICHANGI, wamekunja sura, ila ndio msimamo ilivyo.
  • Utamaduni wa hovyo unaota mizizi kwa kasi kunufaisha wajanja wachache.
  • Wanaooana watumie gharama zao ili wanapofiria kutengana wakumbuke na gharama walizotumia. Kuna watu michango ya harusi wanalipia mahari, wanapata kuanzia maisha n.k hawana uchungu na ndoa
 
Back
Top Bottom