Baada ya mshahara kutoka watu wenye harusi wameanza simu

Me nadhani watakua washanichoka kwenye magroup ya michango sasa.. Maana napokea tu kadi ninapotupa hata sikumbuki
Siku hizi wala sipokei, namwambia hamna shida ujumbe umefika usipoteze kadi, itumike kwa mwingine, tuendelee kuombeana tutaona kitakachopatikana wakati ukifika. Hongera sana. Atajua mwenyewe kama atafuta jina au ampe mwingine kwa jina langu. Ila ikifika natoa kisichoniumiza.
 
Tujifunze kusema HAPANA. Wanaume tunalaani wanawake wasioweza kukataa anamvulia yoyote ila unakuta kwenye sekta yetu ni hivyo hivyo, huwezi kukataa ukasema "SICHANGI" unatoa miahadi inayokuumiza.
Kwenye mambo ya kijamii kama haya,. Sio mbaya kuahidi ila iwe ndani ya uwezo,.
Huwezi jua wewe utamchangia kwenye sheree yeye atakuchangia kwenye ugonjwa..
Maisha ni kushirikiana na kushirikishana
 
Mimi za watu ambao najua ni wakaribu na tunasaidiana kwa namna moja au nyingine napokea na ikibidi kuahidi naahidi iliyo ndani ya uwezo..
Ila za ambao siwafahamu napiga tu kimya
 
Kabisa
 
Walimletea mama na sio wewe kumbe..
Ukikua utaelewa
 
Kwenye mambo ya kijamii kama haya,. Sio mbaya kuahidi ila iwe ndani ya uwezo,.
Huwezi jua wewe utamchangia kwenye sheree yeye atakuchangia kwenye ugonjwa..
Maisha ni kushirikiana na kushirikishana
Upo sawa, ila huwezi mchangia kila mtu. Kuna watu huna hata ukaribu nao, uliye na ukaribu nae hawezi kukuumiza ukimchangia.

Sasa mtu umesoma nae sekondari drs moja miaka imeenda amechelewa kuoa anaoa at 45 huko anakupigia mpaka akukumbushe weee ukishamkumbuka ndo akupe hiyo ajenda kuwa ana kadi yako.
 
Nikue mara ngapi?
Huo ni mfano wa jana
Ningetaka ya zamani ningekupa inayonihusu
Sina utoto huo mimi hadi uniambie nikikua nitaacha
Bado hauko kwenye ile position unayotakiwa usimame wewe kama wewe binti,..
Anyways am sorry
 
Kama hao ndo wakuwakalia kimya,.. ila workmates na majirani na ndugu tunachanga
 
Mkuu kwenye zile kadi huwa hakuna sehemu inayosema mchango ni "lazima" ila huwa waandika wanaomba, ombi huwa lina matokeo mawili kukubaliwa ama kukataliwa. Sio lazima utoe unauchuna tu hakuna atakaekuja kukuhoji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…