Ikifika 2025 kale kautamaduni ka ccm kakuprint fomu moja ya mgombea rais watajifanya hawakajui.2025 wingi ni kubwa mno. Ccm wanatunga yao, ulifika muda huo utaona wagombea 150 wanautaka urais. Wa kwanza M. M yule wa fedha
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ikifika 2025 kale kautamaduni ka ccm kakuprint fomu moja ya mgombea rais watajifanya hawakajui.2025 wingi ni kubwa mno. Ccm wanatunga yao, ulifika muda huo utaona wagombea 150 wanautaka urais. Wa kwanza M. M yule wa fedha
Kutoka sasa hadi 2025 ni kipindi cha miaka minne.Miaka 14 kutoka sasa. Soma ibara ya 40 (2).
Kama unayo ibara nyingine ya kuonesha miaka 9 naomba ilete hapa tuijadili.
Nilisoma 40(2) naona huko chini wanefafanua zaidi. Shukurani.Kutoka sasa hadi 2025 ni kipindi cha miaka minne.
Kwa mujibu wa Katiba ibara ya 40(4) hapa chini; anaruhusiwa kugombea Urais mara moja kwa kipindi cha miaka mingine mitano tu.
Kama atashida atakuwa na jumla ya miaka tisa tu. Uzi ufungwe.
View attachment 1756505
Kwa mama hapa tunakubaliana ,,siyo yule mtesaji ,, nilikuwa sikwelewi kabisa.Usiogope
Uhai wetu sote ni mali ya Mungu
Mi10 tena kwa mama rais Samia Suluhu Hassan[emoji1241][emoji95]
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 na marekebisho yake yote, baada ya mhula huu mfupi wa urais wake wa kurithi kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 37(5), Rais Samia Suluhu Hassan anaweza kuchaguliwa tena kwa mhula mwingine mmoja. Ibara ya 40(4) ambayo ndiyo inahusika inasema hivi:
Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili, lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu.
Obviously, kulikuwa na sloppiness katika uandishi wa Ibara ya 40(4). Limit ni ya kuchaguliwa sio kugombea. Kama hujachguliwa unaweza kugombea hata mara tano kama alivyofanya Hayati Maalim Seif kule Zanzibar. Ukiisoma ibara hii sanjari na ibara ya 40(1), utabaini kwamba walichokusudia kuweka katika ibara ya 40(4) ni ukomo wa kuchaguliwa na sio ukomo wa kugombea kama waandishi wa Katiba walivyoandika!
Kwa kuwa mhula huu mfupi unazidi miaka mitatu, Rais Samia Suluhu Hassan anaweza kugombea na kuchaguliwa tena kushika kiti hicho mara moja tu, baada ya mhula huu.
Tofauti na ilivyozoeleka, kwa uchaguzi wa 2025, Lissu na wafuasi wake (na Kambi ya Upinzani kwa ujumla) wajiandae kukimbizwa mchakamchaka na mwanamama (iwapo ataamua kugombea).
😂😂😂😂😂Hizi nyuzi watu wanaandika wamelala au nini hasa?