Baada ya muhula huu, Rais Samia Suluhu Hassan anaweza kuchaguliwa kushika kiti hicho mara moja

2025 wingi ni kubwa mno. Ccm wanatunga yao, ulifika muda huo utaona wagombea 150 wanautaka urais. Wa kwanza M. M yule wa fedha
Ikifika 2025 kale kautamaduni ka ccm kakuprint fomu moja ya mgombea rais watajifanya hawakajui.
 
Kulingana na katiba SSH hawezi kukaa madarakani miaka 14 ,
Ingewezekana kama magufuli angefariki madarakani amebakiza miaka 3 kushuka chini.
Maximum yake ni 9 years
 
Miaka 14 kutoka sasa. Soma ibara ya 40 (2).

Kama unayo ibara nyingine ya kuonesha miaka 9 naomba ilete hapa tuijadili.
Kutoka sasa hadi 2025 ni kipindi cha miaka minne.

Kwa mujibu wa Katiba ibara ya 40(4) hapa chini; anaruhusiwa kugombea Urais mara moja kwa kipindi cha miaka mingine mitano tu.

Kama atashida atakuwa na jumla ya miaka tisa tu. Umechemka Mkuu.
 
Nilisoma 40(2) naona huko chini wanefafanua zaidi. Shukurani.


Katiba imeeleweka na atagombea kipindi kimoja.

Lakini uzi kufungwa ni jambo tofauti kwa sababu katiba inaweza kujadiliwa kwamba iko arbitrary.

Mfano, miaka mitatu umepatikanaje? Maana hata ukisema nusu ya muhula ni miaka miwili na nusu si mitatu.

Naona mabadiliko ya katiba chini ya Rais Samia yatakuwa topic ngumu sana.
 
Usiogope
Uhai wetu sote ni mali ya Mungu

Mi10 tena kwa mama rais Samia Suluhu Hassan[emoji1241][emoji95]
Kwa mama hapa tunakubaliana ,,siyo yule mtesaji ,, nilikuwa sikwelewi kabisa.
 
Mkimnyima fomu chama chenu kitaingia kwenye uchaguzi mkiwa na Mkuu wa kaya na mwenyekiti asiye na hamasa ya kutumia dola kufanikisha ushindi wenu kama ambavyo imezoeleka.

Mkumbuke yeye bado ndiye mpangaji wa tume ya uchaguzi. Kama bado atataka kutawala na mkanyima fomu mtamuambia nini asiweke tume huru itakayomtangaza yeyote atakayeshinda.Hapo ndipo utabiri wa Pole pole utakapotimia.

Mtajua hamjui.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…