Baada ya Mwl. Mussa Iddy kulalamika, HESLB yatoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa urejeshaji mikopo

Nadhani Kuna watu wanajificha na kichaka Cha magufuli na hii Sheria kuibia watu na hzo za juu zinaingia kwa watu. Mimi naona Kuna wizi wa kisiri kabisa unafanyika na hivi sikuhizi watu hawaruhusiwi kuhoji Mambo.
 
Mimi inabidi tu nikwepe makusudi maana huu ni wizi wa kinguvu kabisa
 
Mwaka 2013 nilipoenda kuangalia deni langu bodi lilikuwa Tsh 12,908,741 (hii inajumuisha hela halali niliyotumia mwenyewe pamoja na ada ilikuwa Tsh 11,394,700, Administration fee Tsh 113,947, retention fee Tsh 1,400,094).

Baada ya miaka 6 kupita huku nikiendelea kulipa deni lilifikia Tsh 14,101,163.82 hii inaonesha kulikuwa na ongezeko la Tsh 1,192,422.82 ambayo kwao walisema ni retention fee.

Mwajiri alipeleka deni la awali la Tsh 12,908,741 na hii ndio walikuwa wanapunguza huko kila nikilipwa salary na naishukuru serikali ilipoongeza 15% ilinisaidia kuwahi kumaliza kulipa deni hili la awali maana nilitakiwa kumaliza 2024 au 2025 kama wangeendelea kukata 8% lakini kwa maamuzi magumu ya serikali ikanifanya nimalize deni hilo 2019.

Hii Tsh 1,192,422.82 ambayo iliongezeka na haikuwekwa kwenye deni la awali bado natafakari namna ya kuilipa maana sijaridhika na hili ongezeko la retention fee kipindi nilichokuwa nalipa.

Na kama ni halali mbona serikali huwa tunaidai hela kwa mda mrefu hata zaidi ya miaka hiyo 6 lakini wao wakija kutulipa hawatulipi na retention fee?

Nawaza nilipe hili deni lililobaki au nisubiri hadi serikali itakaponilipa hela ninayoidai kwanza ndio nimalizie kuwalipa bodi ya mikopo.
Ni mwaka na sehemu umepita bado sijapata jibu kama niwalipe au nisubiri AREAS kwanza.

Note:
Niliwauliza watu wa bodi ya mikopo kama hii retention fee nisipolipa nayo ina retention fee?
Walisema kama ukimaliza kulipa principal loan basi retention fee huwa haiongezeki tena, inabaki hiyo hiyo hata ukidelay kulipa.
Sasa kwa majibu hayo waliyonipa yalinipa kiburi cha kusubiri serikali inilipe kwanza AREAS za kuanzia 2019 ndipo nimalizie kuwalipa. Hadi wa leo sijarudi kuangalia kama retention bado iko hiyo hiyo au nayo wameifanyia retention.

Ila niwatie moyo tu kuwa deni la bodi linalipika na linaisha as long as unalipa hata kama ni kidogo kidogo.
HABA NA HABA HUJAZA KIBABA
 
Watu mbalimbali wamehoji kwa nini Watumishi wanapoidai Serikali hakunaga hiyo 'Rentetion fee'?

Hii iwepo hata pale watumishi wanapoidai serikali,na walipwe hizi haki zao zilizopo kisheria
 
Najiuliza kila siku hivi serikali wasiponiajiri nitawalipaje Mimi.
 
Kuna watumishi wanadai nauli za likizo za mwaka 2014, wakilipwa madeni wanalipwa fedha ileile hiyo value retention fee ni ya upande mmoja?
Magufuli nchi imekushinda.
Alisema ni Rais wa wanyonge unategemea kuna siku mtakuja msiwe wanyonge?Huyu mtu aligombea Urais ili kuwafanya waTZ waendelee kuwa wanyonge
 
Ni aibu kanchi dhaifu kama Tanganyika kuongozwa kitapeli.

Hao wanaotunga hizo sheria zinazorudi kinyuma nyuma huwa ni wanasheria au wanasiasa wajinga wajinga?

Maana huko Tanganyika kila kitu ni janja janja! Hata wanaoitwa wasomi nao ni janja janja tupu!

Mkataba ulisema makato ni 8%, wao wakabadili kinyemela mpaka 15%! Na makato yanawagusa hata wale ambao waliingia mkataba kabla ya sheria mpya!

Ni aibu nchi kuendeshwa KIHUNI. Ni aibu na fedheha!
 
Comment no.100, hiyo retention fee inachajiwa kwenye principal amount kwa reducing formular au inasalia hivyo hivyo?

Pili hii retention inachajiwa before hujaanza kulipa au kwa kipindi chote utakachokuwa unalipa?
 
Majibu ya bodi kwa bwana Iddy ni siasa tu.

Bodi ya mikopo ina matatizo makubwa sana.

Tatizo lao kubwa ni kughushi taarifa za madeni na kuwabambikia watu...yaani kwa ufupi hawana taarifa sahihi na hawataki kuekeweshwa.

Naamini kuna siku mh raisi Magufuli ataangazia huko na kutuokoa watanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…