Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Stori yako imenikumbusha kunaa jamaaa nilimkuta barabarani kalala jua Kalli yaaani kibarabara kinachoingia morogoro road kavua shatii katulia tuli MI nikajua Labdaa anatatizo ita ita nawewe Saaa sielewi watu sijui hawamuoni. Ilaaaaa Dah ilee dhahama sijui tunafeli wapi. Pesaa izi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Oky Inaendelea....

Wakati niko pale chini ikabidi ni washe tochi tena kwa uoga sana maana kama unavyojua ukiwasha tochi usiku ni rahisi sana mtu hata wa mbali kukuona nikaanza kuangaika kutafuta kijiti nilizunguka kwenye ule muembe nikabahatika kupata kijiti chenye matawi matawi nikayatoa kisha nikarudi kwenye eneo la tukio nilianza kuchimba nikachinba sana hadi nikatengeneza kishimo kidogo

Kisha nikatoa zile mbegu tena kwa umakini mkubwa kama niko mahabara natafuta tiba ya corona nikazitumbukiza kisha nikachukua kile kijikisu kidogo nika mkanyaga kuku yule miguu na mabawa nikachoma sana shingoni toboa sana nikaamia sehemu nyingine toboa sana

Kisha damu zikaanza kumwagika kila sehemu nikamaliza nikawa nasubiri kuku akate roho ilichukua muda kidogo hadi kuku akatiulia kisha nikachuku ule udongo nikamwaga kwa juu nikachukua jiwe nikaweka kwa pembeni nikivyoona nimemaliza kila kitu nilichukua kuku nikatoka mbio kama Emanuel kipchonge wa kenye kuelekea njia panda ile sehemu ambayo boda boda wanapaki

Cha ajabu ile nimepiga kama atua tano nilisikia kicheko kikubwa kinatoka nyuma yangu halafu nikasika mkononi kama yule kuku anaangaika anitoke mkononi asee nilikimbai wala sikuangalia nyuma hadi njia panda huku tochi nikiwa nimezima hata siku fika kabisa nilitupa nakukimbia hadi getto kufungua mlango nilimkuta agustino kasha maliza kila kitu

Baada ya siku kama tatu kupita nilisikia mtu anakimbia kwa spidi kali nyuma ya lile getto mida kama ya saa 3 usiku lakini sikutilia shaka agustino alikuwa ametoka njee kwenda kukojoa lakini nilimsubiri bila mafaniko mpaka muda wa kulala ukafika sioni mtu asubuhi ninaamka nakuta tisheti niliokuwa nimeivaa ina matone ya damu nikazidi kuchanganyikiwa baada ya muda agustino alikuja akaniambai unaona jana usiku wakati nimetoka nilizunguka kukojoa hapo nyuma

Wakati nimemaliza nageuka nikamkuta mama mwenye nyumba amesimama nyuma yangu na siku sikia vishindo vyake na ule muda unakuta mama mwenye nyumba wamesha lala ilibidi atimue mbio hadi hosteli nikamwabia sio bangi kweli zilikuchanganya akakataa kata kata.

Ilabidi nimuoneshe nguo yangu nikamwambja na hizi damu vipi akasema eti hafahamu lakini alikuwa kama anasita sita

Basi baada ya siku kadhaa kukatika ikawa imebaki siku moja turudi kwenda kuangalia zile mbegu kama zimeota lakini nilikuwa kama nimekata tamaa nikijiiliza vile vicheko vimetokea wapi walikuwa kinanani lakini ilibaki siri yangu sikutaka kumwabia mtu nikijua naweza leta tatizo kuwa nimeaharibu dawa.

Basi siku yenyewe ikafika ilikuwa ni siku ya saba asubuhi na mapema moyo ukiwa unadanda kila mtu ikabidi apite njia yake kwenda kuvuna alichokipanda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simulia mkuu usihofu be free!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimecheka sana
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…