Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Oky Inaendelea..........

Basi wakati tuko pale kwa mganga akaendelea kutapa masharti na maelekezo tofauti tofauti huku akitusisitizia sana tufanye kama alivyosema pengine nilidhani labda anahofia umri tuliokuwa nao wakati ule.

Baada ya hapo alichukua kopo la tosi lililokuwa pembeni yake lilikuwa kuukuu akalifungua ndani kulikuwa na visu vya kuchongesha kienyeji yaani ni kipande kidogo cha mti halafu kimechomekwa kichuma flani hivi kwa mbele kama spoku ya baiskeli akatoa viwili akatugawia kila mtu kimoja

Akatuambia kabla hatujapanda mbegu lazima tumwage damu kwenye lile shimo lakini kuku yule hatutakiwi kumchinja kawaida inatakiwa tumtoboe toboe na kile kisu mfano wa bisibisi kuanzia kichwani hadi miguuni mpaka apoteze uhai kisha tupande mbegu tufukie .Mzoga wa yule kuku tukatupe njia panda tena inayopitwa na watu wengi

Basi akatusisitizia kuoga na zile dawa alizokuwa ametupatia kipindi cha nyuma pamoja na kunywa lakini tusioge kwenye bafu ambalo humo humo ni choo bora usubiri usiku ukaoga kibarazani. Kisha akatuambia baada ya lile zoezi kukamilika pesa ndio zitakuwa zinaangaika kututafuta na sio sisi kuziangaikia tena

Baada ya hapo akatutakia safari njema na mafanikio mema na kutuambia tutapata mafanikio kwa haraka na kabla mwezi hauja chomoza tumpelekee zawadi kama malipo yake kisha tukawaaga na wale masela pamoja na yule mkee wa mganga tukasepa.

Tukaenda getto tukawa tumetoa nguo tufue tukakuta majaa wasukuma vijana walikuwa na umri kama wa maika 25 hivi wako pale njee wanapiga story baada ya kupiga nao story ikabidi wafunguke eti kunajamaa wamemleta pale kwa mganga kulingana na tatizo lake wameambiwa usiku wapeleke mbuzi beberu waizike nzima nzima ili jamaa yao apate kupona.

Ilipofika usiku agustino ikabidi amcheki yule jamaa aliyetupeleka akamwabia tumemaliza kazi kesho tunapita kwake kumuaga sisi tunasepa basi usiku ule kila mmoja alitoa vitu vyote na nguo zote kwenye begi lake tukatanguliza kwanza yale madawa tuliokuwa tumepewa ndio tukapanga nguo kwa juu.

Kesho yake bila kupoteza muda tukaenda kwa yule jamaa tulishukia njiani akatufata na gari yake akatupeleka mpaka kwake tulipiga msosi wa nguvu kisha akaanza kutuambia kama mmesha toka kwa mganga kila kitu mmemaliza na kama mkifata alivyoelekeza maisha yenu yataenda kubadilika kabisa baadae akasema atutoe tukatembee kidogo mjini lakini wote tuligoma maana tulikuwa tumechoka balaa

Pia wote baada ya kutoka kwa mganga kila mtu alionekana hana furaha nafsini kwake kwani wakati niko njiani nilikuwa najiuliza hivi nitawezaje kwenda usiku saa 7 tena mimi peke yangu mahali nikachimba kishimo nikapanda mbegu kisha nikauwa kuku mwenyewe hivi nitaweza kweli

Kila muda akili yangu ilikuwa inavuta picha kwenye ule mtaa pale shuleni ni sehemu gani nitaweza fanyia kile kitendo lakini nilikuwa sipati majibu moyo unazidi kujaa hofu lakini nikawa nasema potelea mbali liwalo na liwe

Basi usiku tukaanza kujadiliana lakini jamaa yangu agustino anasema nikitu rahisi sana wale kisinipe mawazo basi mimi nikaamua kujilaza baadae story zikachange tukaanza kukumbushiana mdogo mdogo economics zile topic za mwanzo subject matter na demand n supply mimi kichwa kilikuwa kimesha haribika ila jamaa alikuwa anapenda masomo sijui hata ule moyo wa kukumbushana alikuwa anautoa wapi katika hali ile

Basi kesho yake asubuhi yule jamaa akatupeleka hadi stand kwa gari yake safari ikaanza kurudi kwenye getto la agustino basi ilituchukua zaidi ya masaa 9 mpaka kufika stand tukashuka nikamwabia agustino hapa tutafute boda boda maana mizigo sio mingi ni haya mabegi.

Laķini jamaa akaniuliza sii wewe unapitiliza hadi shuleni hostel daa nikamwabia shule bado hatujafungua na hivi vitu nilivyonavyo humu inatakiwa tufikie getto kwako siunajua form 6 hawajafunga wamebaki pale wakiniona nimefika wanaweza kunipora mizigi yangu basi jamaa akatoa 30000 akanipatia akaniambia lete begi lako nikampatia akaniambia tafuta wanapo uza kuku uchukue hata wa 13000 wawili kama mganga alivyosema mimi natangulia wewe utakuja nao

Basi mimi nikampatia begi langu nikaenda kutafuta kuku mjini nilizunguka nikawa nauliza hadi nikaenda kuwapata kwenye vibanda vya soko nikanunua wawili jumla 24000 basi nikamaliza nikachukua boda boda hadi getto kufika nikamkuta jamaa amechangamka kudeki nyumba basi nikaanza kutafuta kamba ya kufungia jamaa akaniambia kuna net iko chini ya uvungu imechakaa nichukue nikate nitoe kamba

Daa ile nimeinama nikaona matone ya damu ambazo ni mbichi chini ya uvungu asee roho ilitaka kupasuka lakini nilisema uchawi hauwendi kwa mentali nikatoa chandarua nikaanza kutengeneza kamba basi jamaa akafua fua baadhi ya mashuka tukapika msosi tukala tukaelekea shuleni kupiga story na wanaa waliokua hawajaenda likizo huku tukiacha kuku zetu pale njee.

Lakini mawazo yalinijaa kichwani zile damu zinatoka wapi na nini sababu baadae akaniambia turudi geto kabla giza halijazidi tuone nijinsi gani tutachora ramani ya kukamilisha ule mchezo usiku ule siku lala nikawa najiuliza maswali ni alama gani nitaweka kwenye aneo nitakalo panda mbegu zangu ili nisisahau kila sehemu naona haiwezekani

Kesho yake tukaanza survey mtaani njiani tunaulizana hivi pale pata faa basi baada ya kuzunguka sana mimi nikaona muembe mkubwa maeneo ya pale pale yaani ulikuwa ni mkubwa kama mbuyu nikamwabia jamaa yangu mimi nitafanyia pale baada tena ya pita pita yeye kasema ataenda pembeni ya mwamba mkubwa raia wa pale waga wanatumia kuanikia nafaka.

Basi kesho yake akaniacha asubuhi nimelala pale akasema anaenda kumuona pusha flani hivi wa bangi waongee biashara maana alimpigia simu akasema mzigo umeisha wakati najigeuza geuza kwenye kile kitanda nilisikia kama kuna sarafu basi nikaamua kuichukua lakini papasa mkono kumbe jamaa alikuwa ameishonea ndani ya godoro kwa ndani kabisa daa nikasema huyu baharia ni hatari

Baada ya muda nikawaza sana lakini roho ya ujasili iliniingia nikasema nikienda kwenye eneo la tukio kuku ndio mgumu kumuuwa nikasema nguvu zote nitawekeza Kwenye kuuwa kuku

Nilitoka pale kikafunga mlango nikaenda kutafuta kifungua kinywa kunamgahawa flani hivi nikakuta wapiga msuli tunao soma nao wanadiscus tu habari za masomo mara sijui integral sijui differentiation hawakwenda likizo basi baada ya kutoka pale nikarudi getto nikafungua begi kuaandaa zana ili usiku mimi nikamilishe kila kitu.

Nilitoka tena nikaenda pale chini ya muembe kufanya survey ikiwezekana niweke alama kabisa ya wapi nitafaanyia tukio pale chini ya muembe maana eneo la pale lilikuwa kubwa kama unavyojua maeneo ya kijiji ni majani majani marefu na matuta yaliyokuwa yamezunguka ule muembe basi nikabeba jiwe kubwa kiasi nikategesha pembeni ya ule muembe

Nikarudi getto nikamkuta agustino basi nikampanga kila kitu na yeye akaniambia leo usiki tumalize mchezo tukapiga mahesabu kuku tutafanyaje asipige kelele akaniambia tutatumia kamba za manila tuwazibe midomo basi.

Tulienda shuleni tukapoteza muda na wadau halafu tukaondoka tulaelekea kwa yule babu tukavuta bangi za kufa mtu siku hiyo tulipata hadi wanajeshi wanagwanda kabisa wanapuliza tukapeana high tukapiga vitu vyetu tukasepa tukarudi hadi getto kiukweli nilikuwa na ogopa kutoka saa 7 tena kila mtu na njia yake bora hata tungekuwa pamoja lakini baada ya kupiga zile ganja uoga ulipungua sana.

Tulikaa getto tukapiga story huku kuku tumezifunga kamba miguu kichwani na kwenye mabawa ilipofika saa 6 kama na dakika 50 kila mmoja akachukua tochi yake zile za sola udogo mbegu kisu na kuku akapitia njia yake njiani nilikuwa naogopa sana kwani kile kijiji watu wanasema ni mambo ya uchwawi ndio yanafanya kisiendele huku nikiwa nawaza au pale kwenye muembe mkubwa ndio huwa wachawi wa ule mtaa wanafanyai mkutano wao

Nilikuwa natembea haraka haraka huku nikiangalia nyuma tochi nilikuwa nimezima nilifatilia ramani hadi nikafika kwenye ule muembe haraka zangu nikataka nianze kuchimba kuaangalia kwenye ule mfuko niliokuwa nimebeba sioni kitu cha kuchimbia, kuku nilikuwa nimemuweka chini akaanza kutapa tapa nikasema ngoja niwashe tochi nitafute kijiti nianze kuchimba shimo kubwa kiasi ili wakati narudi nisije kupotea mahali nilipo panda mbegu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Stori yako imenikumbusha kunaa jamaaa nilimkuta barabarani kalala jua Kalli yaaani kibarabara kinachoingia morogoro road kavua shatii katulia tuli MI nikajua Labdaa anatatizo ita ita nawewe Saaa sielewi watu sijui hawamuoni. Ilaaaaa Dah ilee dhahama sijui tunafeli wapi. Pesaa izi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Oky Inaendelea....

Wakati niko pale chini ikabidi ni washe tochi tena kwa uoga sana maana kama unavyojua ukiwasha tochi usiku ni rahisi sana mtu hata wa mbali kukuona nikaanza kuangaika kutafuta kijiti nilizunguka kwenye ule muembe nikabahatika kupata kijiti chenye matawi matawi nikayatoa kisha nikarudi kwenye eneo la tukio nilianza kuchimba nikachinba sana hadi nikatengeneza kishimo kidogo

Kisha nikatoa zile mbegu tena kwa umakini mkubwa kama niko mahabara natafuta tiba ya corona nikazitumbukiza kisha nikachukua kile kijikisu kidogo nika mkanyaga kuku yule miguu na mabawa nikachoma sana shingoni toboa sana nikaamia sehemu nyingine toboa sana

Kisha damu zikaanza kumwagika kila sehemu nikamaliza nikawa nasubiri kuku akate roho ilichukua muda kidogo hadi kuku akatiulia kisha nikachuku ule udongo nikamwaga kwa juu nikachukua jiwe nikaweka kwa pembeni nikivyoona nimemaliza kila kitu nilichukua kuku nikatoka mbio kama Emanuel kipchonge wa kenye kuelekea njia panda ile sehemu ambayo boda boda wanapaki

Cha ajabu ile nimepiga kama atua tano nilisikia kicheko kikubwa kinatoka nyuma yangu halafu nikasika mkononi kama yule kuku anaangaika anitoke mkononi asee nilikimbai wala sikuangalia nyuma hadi njia panda huku tochi nikiwa nimezima hata siku fika kabisa nilitupa nakukimbia hadi getto kufungua mlango nilimkuta agustino kasha maliza kila kitu

Baada ya siku kama tatu kupita nilisikia mtu anakimbia kwa spidi kali nyuma ya lile getto mida kama ya saa 3 usiku lakini sikutilia shaka agustino alikuwa ametoka njee kwenda kukojoa lakini nilimsubiri bila mafaniko mpaka muda wa kulala ukafika sioni mtu asubuhi ninaamka nakuta tisheti niliokuwa nimeivaa ina matone ya damu nikazidi kuchanganyikiwa baada ya muda agustino alikuja akaniambai unaona jana usiku wakati nimetoka nilizunguka kukojoa hapo nyuma

Wakati nimemaliza nageuka nikamkuta mama mwenye nyumba amesimama nyuma yangu na siku sikia vishindo vyake na ule muda unakuta mama mwenye nyumba wamesha lala ilibidi atimue mbio hadi hosteli nikamwabia sio bangi kweli zilikuchanganya akakataa kata kata.

Ilabidi nimuoneshe nguo yangu nikamwambja na hizi damu vipi akasema eti hafahamu lakini alikuwa kama anasita sita

Basi baada ya siku kadhaa kukatika ikawa imebaki siku moja turudi kwenda kuangalia zile mbegu kama zimeota lakini nilikuwa kama nimekata tamaa nikijiiliza vile vicheko vimetokea wapi walikuwa kinanani lakini ilibaki siri yangu sikutaka kumwabia mtu nikijua naweza leta tatizo kuwa nimeaharibu dawa.

Basi siku yenyewe ikafika ilikuwa ni siku ya saba asubuhi na mapema moyo ukiwa unadanda kila mtu ikabidi apite njia yake kwenda kuvuna alichokipanda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nataka tu nitoe summary ya vitu vitabu

Damu zile zilisababishwa na nini

Mimi na yeye baada ya kwenda kuangalia mbegu tulikuta nini

Agustino nini kilimkuta na sasa yuko wapi

Kila kitu kitakuwa kwenye final episode

Nitaruka vitu vingi sana maana story imekuwa ndefu

Sent using Jamii Forums mobile app
Simulia mkuu usihofu be free!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimecheka sana

Back
Top Bottom