Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

ok mkuu kabla hujafunga mahesabu hebu tueleze sasa umeamua kufanya nini kuusaka utajiri baada ya njia za giza kugoma...
shukurani na asante kwa stori nzuri yenye kufurahisha ,kuhuzunisha na mafundisho ya kutosha,,
 
Inatakiwa wabadilishe mfumo uwe hata wa kiistaarabu kidogo

Ndomaana trump alituita shithole hakukisea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ok mkuu kabla hujafunga mahesabu hebu tueleze sasa umeamua kufanya nini kuusaka utajiri baada ya njia za giza kugoma...
shukurani na asante kwa stori nzuri yenye kufurahisha ,kuhuzunisha na mafundisho ya kutosha,,
Nitaandikia mada nyingine nieleze kila kitu

Nilikuwa nataka nieleze humu lakini lengo linesha haribika

Hii mada inatakiwa ikae kwenye jukwaa la hoja na habari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
AGUSTINO HAS FALLEN[emoji31][emoji31]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah mwanangu nusu nitoe chozi ....afu nipo na manzi na nlimwambia natokea bara sasa ningetoa chozi nahisi angejua uhalisia wangu kuwa mwanaume wa Dar...

Ila mkuu tuambie sasa zile damu ni nini?[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
Mkuu umeanza sasa ubongo movie unaadisia mpka mambo ya nilenda kbandani nkanuaa vocha sijui ya jero nkarudisjiwa jero. Mara vocha ikapotea nkarudi nkatoe ile jero. Nikascratch nkaweka vocha nkampigiia hapatikani....yanini yote hayo? Unaanza kupoteza mvuto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu panga safari uwende kumchek mwamba usisahau kumpelekea zawadi nyingi kama box za soap, redio, nyembe n.k.

Nitajitolea box moja la sabuni kama ukitaka kwenda niPM nitachangia mkuu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Unajua mkuu, ukiwa unaandika story ni kama uko kwenye chumba cha mtihani unashirikisha ubongo, macho pamoja na mikono

Soo kilichokuwa kunatoka kwenye ubongo ndio nilichokuwa naandika
Sorry kama huo uandishi umekukwaza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu panga safari uwende kumchek mwamba usisahau kumpelekea zawadi nyingi kama box za soap, redio, nyembe n.k.

Nitajitolea box moja la sabuni kama ukitaka kwenda niPM nitachangia mkuu


Sent from my iPhone using JamiiForums
Sawa mkuu nikitaka siku nikitaka kwenda nitaku PM pengine yaweza kuta sumu za huu uzi zimepungua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu narudia tena achana na mpango huo unaotaka kufanya. Acha kabisa.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nitaandikia mada nyingine nieleze kila kitu

Nilikuwa nataka nieleze humu lakini lengo linesha haribika

Hii mada inatakiwa ikae kwenye jukwaa la hoja na habari

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata humu kwa mtazamo wangu bado inakidhi vigezo vya kubaki kwani bado inaelezea mapito wanayopitia watu kwenye utafutaji

Kwa vile moderators wameamua kuiunganisha kule juu ni vizuri sasa ukaweka mbinu mpya za halali unazotumia kwa sasa kupambana na swala zima la utafutaji baada ya mbinu zenu kugonga mwamba

Hii itaipa nguvu kubwa story yako na itabaki kuwa funzo kwa wengine wanaodhani kwa waganga kuna kupata utajiri kirahisi au wanaouza bangi na madawa mengine ya kulevya wanapata utajiri kirahisi

Ulichokieleza kinafunzo kubwa kwa watafutaji kwani katika utafutaji watu tunapitia mahangaiko mengi sana ikiwemo kuwaza hayo ya waganga

Pamoja na yote kama utakuwa umechagua kuandika hicho kipengere chako cha mwisho kinachoelezea unayo yafanya kwa sasa kwenye post hii, jitahidi kuiweka kwa kulenga pointi za msingi unazotaka watu wajifunze

Mwisho kabisa kwani tangu uzi unaanza sikuchangia popote ila nimeufuatilia vizuri tu ili kujua hatima ya Augustino, nikushauri tu kwa vile umekiri ni story ya kweli iliyokutokea mwenyewe tafuta namna ya kwenda kumuona jamaa yako huko gerezani

Ni kweli kabisa wafungwa huwa wanahamishwa hamishwa ila ukiamua utampata tu! Nenda kampe hi atajisikia faraja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…