jooohs
JF-Expert Member
- Jul 26, 2017
- 2,524
- 10,287
- Thread starter
- #961
Asee since the beginning [emoji23]Ni kipindi kifupi lakini jooohs katuteka hasaa.!
Acha tu mama, ndiyo nimemaliza yote hapa.!
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asee since the beginning [emoji23]Ni kipindi kifupi lakini jooohs katuteka hasaa.!
Acha tu mama, ndiyo nimemaliza yote hapa.!
Hahaha..
Inatakiwa wabadilishe mfumo uwe hata wa kiistaarabu kidogoUmenikumbusha niliwahi kumtembelea rafiki yangu Magereza ya Butimba Wakati fulani..
Nilichokiona ndicho ulichoandika.. Watu mnaingia wengi,mnaongea kwa nguvu kwenye nyavu.. hakuna kusikilizana.. Sikuwahi kuingia.. Nikivyotoka pale nililia njia nzima.. Wafungwa wanateseka sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante kwa storyOky wakuu hii ndio itakuwa episode ya mwisho nawashukuru wote waliokuwa baga kwa bega toka uzi unaanza mpaka sasa tumemaliza
Sent using Jamii Forums mobile app
Shukrani sana Carleendaaaaaah'..!!.
thank you so much Jooohs'..!
Sijui I am too emotional hapo mwisho pameniumiza moyo.!!
May the Agustino Legendary Live Long..!
'Urafiki wa kweli haupimwi kwa muda bali unapimwa kwa matendo'..!!
Nitaandikia mada nyingine nieleze kila kituok mkuu kabla hujafunga mahesabu hebu tueleze sasa umeamua kufanya nini kuusaka utajiri baada ya njia za giza kugoma...
shukurani na asante kwa stori nzuri yenye kufurahisha ,kuhuzunisha na mafundisho ya kutosha,,
pamoja mkuu...Nitaandikia mada nyingine nieleze kila kitu
Nilikuwa nataka nieleze humu lakini lengo linesha haribika
Hii mada inatakiwa ikae kwenye jukwaa la hoja na habari
Sent using Jamii Forums mobile app
AGUSTINO HAS FALLEN[emoji31][emoji31]Baada ya kufuta lile tope mdogo mdogo nikaanza kupandisha kimpando cha kuelekea kwa babu nikafika pale nikazuga kama nimeenda kuomba ganja akaanza kusema asubuhi yote umekuja kufanya nini nikamwambia nimekuja kufata dawa.
Akaniambia yamebaki makapi , kisha akaniuliza yule mwenzako agustino mzigo amesha leta nikasema hapana.
Ikabidi aingie ndani aniletee yaleyale makapi
Nilitoka pale kwa babu nikijua agustino hakuuza mtu yoyote kwa polisi basi nikaanza kutembea kurudi shuleni kwa yale mavazi nilishindwa nitarudi vipi ikabidi nitafute sehemu nikae nitulie nione jinsi gani nitatunga hoja .
Nilikaa mahali nikawaza agustino hana ndugu mahali pale nikasema nitafanyaje niende hata kumuona kituoni nikakosa jibu maana na mimi nilikuwa na hofia usalama wangu nilimpigia tena ndugu yake yule nikamwambia awaambie wazazi wake hata na yeye pia aje kumuona maana haikuwa mbali sana
Nilimwambia pia aje niwaoneshe getto ikiwezekana wachukue vitu vyake vya muhimu wa mtunzie jamaa aliniambia yeye anatangulia kashamwambia baba yake atakuja kesho
Basi alivyofika nilienda kumpokea pale centre tukaenda hadi getto jamaa akajitambulisha kuwa nikakaake tukavunja kufuli tumeingia ndani tafuta vitu muhimu kama simu, kadi ya banki,walet vyote hakuna na baadhi ya vitu vingine sivikumbuki
Basi yule kaka yake japo wakuvuta na kamba kesho yake akasema nije nimpeleke kituoni tumpelekee msosi mimi nilikubali ila nikamwambia nitabaki mbali kabisa usikie maafande watakwambiaje.
Kweli kesho yake nilivunja vipindi nikamsindikiza Yule jamaa alivyorudi akaniambia walimuoji ikabidi awaambie yeye ni kaka yake alitokea wilaya nyingine kuja kumletea msosi, Jamaa aliulizia kama anaweza muwekea dhamana ya pale kituoni maafande walikataa wakasema tena jarada lake linapelekwa mahakama ya wilaya
Daa jamaa alichoka tulirudi nae hadi getto kesho yake tena tukaenda kumuona na yule jamaa ndio nikajua kweli bongo nyoso yani hawakupi nafasi ya kuongea na mtu ukishapeleka msosi unaonja askari wanachukua unatembea mbele huwezi ongea hata siri na mtuumiwa , Halafu kituoni kumbe hawapiki sasa nikawa najiuliza hivi waliokamatwa na hawana ndugu karibu huwa wanakula nini kabla hawajapelekwa magereza
Kiufupi agustino kesi yake ilipelekwa mahakama ya wilaya, tena alishitakiwa na jamuhuri kwa kosa la kukamatwa na zaidi ya kili 100 za bangi tena alikamatwa na ushahidi kabisa boda boda wake kwa kujitetea ikabidi amchomee kabisa alisimama kama shahidi wa mwisho
Kulingana na mapambano ya bangi kipindi kile bila huruma hakimu alimtundika miaka 30 jela. Nimechoka kutype
Oky ngoja niendelee nakumbuka siku ya mwisho nimeenda kumuona pale magereza nikiwa nimeshika mkate na vipande vya sabuni + wembe nikajua labda kidogo kule magereza kutakuwa na utaratibu mzuri wa kuongea na mfungwa asee kufika tuliruhusiwa raia kama 20 hivi kwa mkupuo eti tuongee na wafungwa wetu kwa zile kelele sikuweza kumsikia vizuri neno nililolisikia kutoka kwake ni MWANANGU ENDELEA KUKOMAA
Na hapo nilikuwa nimetoka shuleni wilaya nyingine wakati natoka kwenye lile gereza nilijisikua huzuni sana kiasi kwamba nilijikuta na bubujikwa na machozi baada kama ya mwaka na nusu kupita nikiwa chuoni niliongea na yule kaka yake akaniambia agustino alihamishwa butimba mwanza
Kunakipindi niliona magufuli ameenda pale niliangaika sana kumtafuta agustino kwenye zile camera lakini sikufanikiwa kumuona rafiki yangu kipenzi now kamanda agustino amemaliza miaka 5 gerezani. kwa kifungo cha miaka 30 kwa jinsi wanavyo hesabu amebakiza miaka 15 gerezan
Mimi bado nikijana sana mwaka huu mwezi fulani na fikisha 24 yrs damu bado inachemka naendelea kupambana rafiki yangu mpambanaji agustino, kufa na kupona, kwa hali na mali nijipanue kiuchumii ili siku ukitoka gerezani husije kunicheka eti nilikuwa napoteza muda kitaa
Nataka uje unikute nimesha tengeneza bara bara nzuri ya kiuchumi uje tuishi maisha ya kidoni kama zilivyokuwa ndoto zako.
Nilichojifunza urafiki bora haupimwi kwa muda unapimwa kwa matendo maana niliishi na agustino katika kipindi kifupi sana lakini ameacha historia kubwa sana ndani ya maisha yangu
Nineandika kwa haraka vibaya vibaya kama kutakuwa na makosa tusameeane
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umeanza sasa ubongo movie unaadisia mpka mambo ya nilenda kbandani nkanuaa vocha sijui ya jero nkarudisjiwa jero. Mara vocha ikapotea nkarudi nkatoe ile jero. Nikascratch nkaweka vocha nkampigiia hapatikani....yanini yote hayo? Unaanza kupoteza mvuto.Oooky Inaendelea..................
Wakati naendelea kujiuliza huyu agustino atakuwa kaenda wapi wazo likaniijia nimpigie tena yule ndugu yake labda atakuwa kapata baadhi ya information nikampigia tena akaniambia bro siumetoka kunipigia sasa muda si mrefu nimekwambia sina taarifa yake akinitafuta tu nitakupigia basi nikatoka pale getto nikaanza safari kuelekea centre pengine nikae pale naweza kumuona labda anapita na madumu nikampokee
Muda ulikuwa unayoyoma jua linaelekea kuzama nikaanza mwendo ukumbuke hapo alipokuwa anakaa ilikuwa kunaka umbali hadi kufika centre ikabidi nitembee haraka haraka hadi kufika pale nikakuta maboda boda kibao wamekaa wanapiga story, wengine wanakunywa uji kulikuwa kunamama anapika pale centre.
Mimi muda huo nimechanganyikiwa kila muda napiga simu ya agustino lakini haipatikani nikajipa moyo labda simu yake itakuwa imezima maana alikuwa anakatecno kadogo sana lakini touch screen. Basi nikaendelea kuzuga pale huku nikiendelea kusikiliza sauti za wale boda boda wa kibishana kuhusu simba na yanga, wengine wakiongea lugha za kienyeji
Wakati na zidi kutafakari huku nikikodolea macho kila piki piki inayopita pale nikawa na matumaini labda itakuwa ni agustino lakini nilikuwa naambulia patupu daa nikiangalia muda unazidi kwenda nikipiga simu haipokelewi mara muda kidogo naona message kutoka voda kifurushi chako kimeisha.
Ikabidi nisimame nitazame kibanda ambacho kiko karibu nikaona kimoja kiko upande mwingine nikavuka upande wa pili wa bara bara nikaenda kibandani nikatoa noti ya elfu moja nikapewa vocha ya mia tano nukarudishiwa mia tano
huku nikiendelea kukodolea macho kila usafiri unaopita pale
Ikabidi nivuke tena bara bara niende kukaa ile sehemu niliokuwa nimekaa kufika nataka kukwangua vocha mkononi siioni kusachi mfukoni na ile jero peke yake nikaanza kurudi kukagua pale chini labda nitakuwa nimedondosha wapi nikafatilia barabara yote hadi pale kibandani sikuona kitu.
Nikatoa tena ile 500 nikanunua vocha nyingine kuweka nampigia jamaa bado simu haipatikani daa nikaendelea kukaa pale hadi giza kabisa likaingia nikawaza huyu jamaa atakuwa yuko wapi nilikaa pale hadi wauza mboga kina mama kila mmoja akaanza kubeba sinia anaondoka zake
Daa nikapiga mawazo au kati ya zile taxi zilizokuwa zinapita hapa moja kati yake atakuwa alikuwa ni agustino ngoja nirudi getto kwake kufika pale nikakuta baadhi ya wapangaji pale kuwauliza wanasema bado jamaa hajarudi labda atakuwa yuko shuleni.
Asee niliondoka huku nimechoka hata nguvu za kutembea nilikuwa sina nilitembea hadi nikafika pale hostel nikamwambia muddy kuwa nimeenda kwa agustino lakini sijamkuta lakini jamaa alichukulia kawaida ikabidi kwenda jikoni kwa mpishi nikapiga nae msosi maana wanafunzi walikuwa wameshamaliza kula wengine wameenda prepo ikabidi niingie hostel nianze kuuchapa usingizi
Sijui wenzangu walikuwa wananionaje, nadhani walikuwa wananiona kama mtu aliyekata tamaa na masomo halafu siko serious maana prepo nilikuwa sionekani, soma yangu ya kusua sua kila siku nasingizia naumwa kichwa kumbe hali yangu naijua mwenyewe kunasiku nilikuwa natoka darasani naenda hostel nikapita nyuma ya darasa la wanaosoma arts nikasikia wanacheka vibaya sana huku head boy anasema wale majamaa hawako serious
Kama yule anae doji prepo anasingizia kuumwa kichwa halafu jioni unamuona anaenda kuvuta bangi asee nikapita tu walivyoniona dirishani wakazuga kunyamaza kumbe baharia nimesikia kila kitu.
Wakati nimejilaza pale kitandani huku nikiendelea kupiga ile namba ya agustino bila mafanikio nikawaza sana nitafanya vipi nimpate huyu jamaa maana nilikuwa na hofu sana, niliendelea kupiga ile simu bila mafanikio kesho yake asubuhi ilikuwa ni siku ya shule nikawahi kuamka mapema sana nikajiandaa vizuri nikavaa sare za shule nikamwabia muddy ngoja niwahi kwa agustino maana ndio nilikuwa namuona kama rafiki nilie kuwa nimebaki nae wengine wote wananiona kilaza
Basi nikaanza kutembea fasta hadi nikaiacha kwa mbali mipaka ya shule nikaanza mdogo mdogo kumezwa na vichaka vilivyokuwa vimetapakaa kila sehemu ya ule mtaa basi nilitembea haraka Hadi nikafika kwenye ile nyumba kuangalia mlango umefungwa ikabidi nigonge mlango wa yule mpangaji pale nikamuuliza agustino hajarudi asee
Majibu aliyonipa yalikuwa ni yakusikitisha sana na kuniogopesha maana yule mpangaji akasema alirudi hapa usiku sana na maaskri wakafungua mlango wakapekuwa ila hawakujua walichukua nini kisha wakaondoka nae yaani nilitaka kupooza palepale ilibidi nikae chini ya udongo nikajua mambo ndio yamesha haribika kabisa.
Basi ilibidi niondoke pale nikiwa na maswali mengi , nijajiuliza nirudi shuleni au nikachukue mizigo yangu niwaambie nimezidiwa naenda kulazwa hospital, nkajiuliza tena hivi shule na maisha yangu kipi bora wakati naendelea kujiuluza nikakumbuka yule ndugu yake alietuma mzigo ikabidi nimvutie kamba alipokea nikamwambia jamaa agustino kakamatwa na maaskari jamaa kashituka sana kaniuliza mara mbili mbili nikamwambia ndio walikujanae hadi kupekuwa alipopanga jamaa akakata simu.
Kisha nikatembea fasta kurudi shuleni nikaenda kuingia hadi hosteli nikakuta jamaa ndio wanajiandaa wanavaa nguo waende kwenye ratiba za shule mimi nilipofika nikaanza kuvua yale mavazi yangu kisha nikabadili nguo nyingine za kawaida nikasepa
Nilisema ngoja kwanza niende hadi kule kwa babu labda atakuwa kupigwa kaambiwa ataje wafuasi wake nikanza mchaka mchaka haraka zangu nimefika pale mtoni navuka haraka haraka nikateleza kiatu chote kikazama ndani ya matope ikabidi nivue nikaanza kutoa yale matope kisha nikavaa hivyo hivyo kibichi nikaendelea na safari........
Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua mkuu, ukiwa unaandika story ni kama uko kwenye chumba cha mtihani unashirikisha ubongo, macho pamoja na mikonoMkuu umeanza sasa ubongo movie unaadisia mpka mambo ya nilenda kbandani nkanuaa vocha sijui ya jero nkarudisjiwa jero. Mara vocha ikapotea nkarudi nkatoe ile jero. Nikascratch nkaweka vocha nkampigiia hapatikani....yanini yote hayo? Unaanza kupoteza mvuto.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa mkuu nikitaka siku nikitaka kwenda nitaku PM pengine yaweza kuta sumu za huu uzi zimepunguaMkuu panga safari uwende kumchek mwamba usisahau kumpelekea zawadi nyingi kama box za soap, redio, nyembe n.k.
Nitajitolea box moja la sabuni kama ukitaka kwenda niPM nitachangia mkuu
Sent from my iPhone using JamiiForums
Kweli aseeIts all about struggle.
Pambana mkuu huyo ni ndugu yako mwisho msiwe wote loser. Ukiwin wewe ni kama na yeye kawin.
Haya mambo yapo wazee. Kuna nyumba huku kwetu huwa haifahamiki mmiliki wake. Kila siku usiku watu hutoa vilio wakiwa ndani ya nyumba hiyo, ukiwa kwa nje unaona kama watu wanatembea mle ndani kupitia pazia zile za transparency. Nyumba ni kubwa haina umeme kwa hiyo mwanga unaotumika mule ni kama mwanga wa mshumaa. Eneo hilo linaogopeka sana na ukipita wakati wa mchana unakuta pako kimya kwelikweli, kuanzia usiku saa tano huwa mwanga wa mshumaa unawashwa, halafu sauti za vilio zinaanza kusikika, ni wake kwa waume huku mipishano ikiendelea mule ndani. Wanasema mwenye nyumba alishafariki miaka mingi na sijui hakuwa na familia au laa. Leo nitajiaribu kupapiga picha au kuchukua video
Hata humu kwa mtazamo wangu bado inakidhi vigezo vya kubaki kwani bado inaelezea mapito wanayopitia watu kwenye utafutajiNitaandikia mada nyingine nieleze kila kitu
Nilikuwa nataka nieleze humu lakini lengo linesha haribika
Hii mada inatakiwa ikae kwenye jukwaa la hoja na habari
Sent using Jamii Forums mobile app