Hapana mkuu hiyo ilikuwa sio ndoto hayo yalikuwa mawazo ya ulichokuwa kuwa unakiwaza mchana.Usiku nikaanza kuwaza eti mtoto wangu, kaenda kwa mganga, kapanda maharage, kaenda kuyachuma kakuta Ni mimi, akajisemea nimuue mama au niachane na utajiri? Basi nikashtuka nikaanza kuomba na kukemea hiyo roho ya kishirikina kwa wanangu
Mungu niepushe mimi maisha matamu hivi
Sent using Jamii Forums mobile app
Aminaa sana pyaarAisee! Pole sana kamanda.
Endelea na mapambano katika kuusaka udon kwa njia halali pasipo dhuluma ya nafsi, roho ama mali. Na Mwenyezi Mungu akutangulie katika mapambano. Siku Mwamba Aug. akitoka msaidie kwa chochote utakachobarikiwa,endapo utakuwa umeneemeka kidogo usiache kumuinua.
Usiache kwenda kumpa company na kumfariji hata kwa hizo dakka 3 zinatosha sana kwa yeye kufarijika.
Uwe na kiu ya mafanikio ila kiu hiyo ikatwe kwa njia zilizo halali.
Nikutakie ijumaa njema takatifu na yenye baraka...[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Mambo hubadilika Jitsudaah me huwa najiita mwanaume wa shoka but asubuhi hii machozi yamenitoka especially the way life hustles za mzee Agu zilivyokata na kuishia kwa jela,...
Hapana mkuu kipimo cha akili sometimes nikuweza ku control hisiaUna Moyo... Mimi hapo nishampa Kitusi.
Angemalizia kule porini na mama angekata rohoIngekuwa mbele sasa hivi kungekuwa na movie inaitwa AGUSTINO!
AU AGUSTINO HAS FALLEN
AU Kibongo movie ungesikia HARAKATI ZA AGUSTINO.
Vipi hukiwahi kuconfess kwa bi mkubwa kuwa kile kisanga cha yeye kuvamiwa na wezi ni outcome ya mambo ya utajiri uliokuwa unatafuta?
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana sio kesi ya ubakaji.jooohs
Je, Augustino alihukumiwa kwa kosa la kukutwa na bhangi au alibambikiziwa kesi ya ubakaji?
James Jason
Dah sure nimekumbuka mpska raia wakachoma moto....
Ila mwanangu Joooh mwamba agustino nimemkubali kichizi.Ningekuwa nna mamlaka jamaa ningemwachia huru alipambana kuzifikia ndoto zake ila daah naona mapoti wakampenda zaidi.
Ila ni wakati wako wa kuonesha thamani unayompa mastermind Agustino maana hakukutaja wala kumtaja yeyote yule aliamua ateketee kama mshumaa.Bless sana kwa huyu Jamaa
Aiseee inavyoonekana wale jamaa wa mkwara ndio waliosuka mipango ya Augustino kukamatwa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Baada ya kufuta lile tope mdogo mdogo nikaanza kupandisha kimpando cha kuelekea kwa babu nikafika pale nikazuga kama nimeenda kuomba ganja akaanza kusema asubuhi yote umekuja kufanya nini nikamwambia nimekuja kufata dawa.
Akaniambia yamebaki makapi , kisha akaniuliza yule mwenzako agustino mzigo amesha leta nikasema hapana.
Ikabidi aingie ndani aniletee yaleyale makapi
Nilitoka pale kwa babu nikijua agustino hakuuza mtu yoyote kwa polisi basi nikaanza kutembea kurudi shuleni kwa yale mavazi nilishindwa nitarudi vipi ikabidi nitafute sehemu nikae nitulie nione jinsi gani nitatunga hoja .
Nilikaa mahali nikawaza agustino hana ndugu mahali pale nikasema nitafanyaje niende hata kumuona kituoni nikakosa jibu maana na mimi nilikuwa na hofia usalama wangu nilimpigia tena ndugu yake yule nikamwambia awaambie wazazi wake hata na yeye pia aje kumuona maana haikuwa mbali sana
Nilimwambia pia aje niwaoneshe getto ikiwezekana wachukue vitu vyake vya muhimu wa mtunzie jamaa aliniambia yeye anatangulia kashamwambia baba yake atakuja kesho
Basi alivyofika nilienda kumpokea pale centre tukaenda hadi getto jamaa akajitambulisha kuwa nikakaake tukavunja kufuli tumeingia ndani tafuta vitu muhimu kama simu, kadi ya banki,walet vyote hakuna na baadhi ya vitu vingine sivikumbuki
Basi yule kaka yake japo wakuvuta na kamba kesho yake akasema nije nimpeleke kituoni tumpelekee msosi mimi nilikubali ila nikamwambia nitabaki mbali kabisa usikie maafande watakwambiaje.
Kweli kesho yake nilivunja vipindi nikamsindikiza Yule jamaa alivyorudi akaniambia walimuoji ikabidi awaambie yeye ni kaka yake alitokea wilaya nyingine kuja kumletea msosi, Jamaa aliulizia kama anaweza muwekea dhamana ya pale kituoni maafande walikataa wakasema tena jarada lake linapelekwa mahakama ya wilaya
Daa jamaa alichoka tulirudi nae hadi getto kesho yake tena tukaenda kumuona na yule jamaa ndio nikajua kweli bongo nyoso yani hawakupi nafasi ya kuongea na mtu ukishapeleka msosi unaonja askari wanachukua unatembea mbele huwezi ongea hata siri na mtuumiwa , Halafu kituoni kumbe hawapiki sasa nikawa najiuliza hivi waliokamatwa na hawana ndugu karibu huwa wanakula nini kabla hawajapelekwa magereza
Kiufupi agustino kesi yake ilipelekwa mahakama ya wilaya, tena alishitakiwa na jamuhuri kwa kosa la kukamatwa na zaidi ya kili 100 za bangi tena alikamatwa na ushahidi kabisa boda boda wake kwa kujitetea ikabidi amchomee kabisa alisimama kama shahidi wa mwisho
Kulingana na mapambano ya bangi kipindi kile bila huruma hakimu alimtundika miaka 30 jela. Nimechoka kutype
Oky ngoja niendelee nakumbuka siku ya mwisho nimeenda kumuona pale magereza nikiwa nimeshika mkate na vipande vya sabuni + wembe nikajua labda kidogo kule magereza kutakuwa na utaratibu mzuri wa kuongea na mfungwa asee kufika tuliruhusiwa raia kama 20 hivi kwa mkupuo eti tuongee na wafungwa wetu kwa zile kelele sikuweza kumsikia vizuri neno nililolisikia kutoka kwake ni MWANANGU ENDELEA KUKOMAA
Na hapo nilikuwa nimetoka shuleni wilaya nyingine wakati natoka kwenye lile gereza nilijisikua huzuni sana kiasi kwamba nilijikuta na bubujikwa na machozi baada kama ya mwaka na nusu kupita nikiwa chuoni niliongea na yule kaka yake akaniambia agustino alihamishwa butimba mwanza
Kunakipindi niliona magufuli ameenda pale niliangaika sana kumtafuta agustino kwenye zile camera lakini sikufanikiwa kumuona rafiki yangu kipenzi now kamanda agustino amemaliza miaka 5 gerezani. kwa kifungo cha miaka 30 kwa jinsi wanavyo hesabu amebakiza miaka 15 gerezan
Mimi bado nikijana sana mwaka huu mwezi fulani na fikisha 24 yrs damu bado inachemka naendelea kupambana rafiki yangu mpambanaji agustino, kufa na kupona, kwa hali na mali nijipanue kiuchumii ili siku ukitoka gerezani husije kunicheka eti nilikuwa napoteza muda kitaa
Nataka uje unikute nimesha tengeneza bara bara nzuri ya kiuchumi uje tuishi maisha ya kidoni kama zilivyokuwa ndoto zako.
Nilichojifunza urafiki bora haupimwi kwa muda unapimwa kwa matendo maana niliishi na agustino katika kipindi kifupi sana lakini ameacha historia kubwa sana ndani ya maisha yangu
Nineandika kwa haraka vibaya vibaya kama kutakuwa na makosa tusameeane
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu swali la kwanza kuhusu zile damu mimi mwenyewe nilikuwa na muhisi agustino lakini mara ya kwanza nikijua atakuwa na tatizo kiafya hata alikuwa akivua shati nilikuwa najaribu kumchunguza, wakati mwingine nilikuwa nikimuuliza anasema anaziona lakini hajui zinapotoka, pia muda mwingine nilikuwa nikizikuta nikaondoka kurudi nikimuuliza anasema hajaona kitu yaani mambo haya ya ushirikina yanachanganya sanaMkuu hongera kwa story tamu sana, pia kwa jinsi ulivyosimulia umeitendea haki
Kwani maswali mawili matatu naomba uyatolee ufafanuzi:-
Kwa jinsi nilivyosoma story yote inaonesha zile damu ilikuwa kazi ya mikono ya Mama Mwenye nyumba na ulipokuwa unaiona damu ulikuwa unastuka, lakini ulipokuwa unamwambia Augustino alikuwa hajali (hii kuna wakati ilinifanya nihisi yeye ndio mhusika). Je kwanini hili suala lilikuwa hata halimuumizi kichwa Augustino?
Hata kwenye kuhama nyumba, pamoja na kugundua kuwa mama ni kigagula Augustino alikuwa mzito kukubali ushauri wako wa kuhama. Lakini pia kuna siku Augustino alikimbizwa na yule Mother House, hakukueleza kwa undani? Yaani from no where huyo mama ilikuaje akawa anamkimbiza Augustino? (Hapa inanifanya niamini Augustino alikuwa ana mambo yake mengine ambayo wewe hukuyafahamu)
Mwisho, yule msaidizi wa mganga aliwahi kuwaambia kwamba msipovuna zile mbegu, zikivunwa na watu wengine mtaadhibiwa na mizimu, je kuna jambo baya lolote lililokupata, ukahisi ni mizimu ipo kazini?
Mkuu ukijibu hayo utakuwa umefanya jambo la maana sana
Sent using Jamii Forums mobile app
Muulize Mshana Jr akupe uzoefu.Uganga unalipa?
Mi mwenyewe nilimtukana kimoyomoyo jamaa aliyeandika ile comment...nikajiuliza ivi anamlipa jooohs kwa kuandika hii story?Una Moyo... Mimi hapo nishampa Kitusi.
We jamaa uko matured sanaHapana mkuu kipimo cha akili sometimes nikuweza ku control hisia
Kuwa emotional intelligent
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu swali la kwanza kuhusu zile damu mimi mwenyewe nilikuwa na muhisi agustino lakini mara ya kwanza nikijua atakuwa na tatizo kiafya hata alikuwa akivua shati nilikuwa najaribu kumchunguza, wakati mwingine nilikuwa nikimuuliza anasema anaziona lakini hajui zinapotoka, pia muda mwingine nilikuwa nikizikuta nikaondoka kurudi nikimuuliza anasema hajaona kitu yaani mambo haya ya ushirikina yanachanganya sana
siku nilipo muamini kuwa sio yeye niilesiku tumekuta damu zimetapakaa kuchumbani ikabidi tumuite mama mwenye nyumba ili tumueeleze chaajabu alipokuja sikuona wote hatukuziona
Pia hata wakati namwabia agustino acheki kile kimkono chini ya kitanda akaniambia haoni kitu.
Pia na wanakijiji walivyoingilia kati nikajua atakuwa ni yule yule mama maana wakati ameamia kwenye getto lingine sikuwahi shuhudia mauza uza kama yale
Swali la 2 yule mama hakumkimbiza Agustino siku ile agustino alirudi asubuhi akaniambia alikuwa zake njee usiku kugeuka akamkuta mama mwenye nyumba yuko nae zero distance ikabidi atimue mbio nikamuuliza au ni bangi zimekuchanganya
Pia hata mimi nilivyo eleza kwenye story yote kulitokea na matukio tofauti tofauti usiku nikawa na muona live kipindi hata naenda kuke kwenye muembe nikiwahi kumuona
Kuhusu agustino kusita sita kuondoka pale nadhani ilikuwa mazingira maana tulikuwa tunajitawala wenyewe pale chumba kilikuwepo pembeni yetu lakini kilikuwa hakina mtu
Swali la mwisho Mimi niliamin amini kuna nguvu za maganga zinatumika kwa kiasi kukubwa siku ile nimeenda kuchimba mbegu nikakuta geneza mauza uza mengine yalikuwa chanzo ni kule tulikotoka nadhani walikuwa wanatupima imani
Sent using Jamii Forums mobile app