Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Hii episode ya mwisho imeniudhunisha sana.. Nimejikuta naumia sana aiseee...
Kweli wanaume tumeumwa mateso...
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana mkuu sio ubakaji ni hilo hilo la bangi sema tu sikutaka kufunguka saana kuhusiana na agustino. Nilikuwa na elezea maisha yangu binafsi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu tukio kama hili limewahi kumtokea ndugu yangu kabisa wa baba yangu mkubwa akiwa na rafiki yake, walianzia kwa mganga ili kupata utajiri wakafuata masharti yote kabisa na sharti la mwisho wakapewa kamba za katani na kuambiwa waende nje kidogo ya kijiji (ni jirani na mbuga ya serengeti) watawakuta ngo'mbe wawafunge na zile kamba na kuwaleta kwa mganga baada ya hapo pesa itakuw ni ya kumwaga. Walipofika pale walichokiona kwanza ni vumbi linatimka na muda si mrefu Nyati wawili walioshiba wako vichwa chini spidi 240 km/h. Ndugu yangu anasema mbio alizotimka siku hiyo si za dunia hii. Hii si hadithi na mimi si muumini wa mambo hayo lakini tulikuwa tunajua katumwa kwenda kuleta ng'ombe na mganga na miaka ile mgodi wa Nyamongo (sasa North Mara) ulikuwa chini ya wenyeji na mambo ya ushirikina yalikuwa mengi sana.
 
Nipe namba mkuu[emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila mkuu inaonekana huyo mganga alikuwa kiboko haswaa.
 
Ila mkuu inaonekana huyo mganga alikuwa kiboko haswaa.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]sema mganga kazingua sasa angewapa hata nusu hasara..

Ila nawaza vipi kama joooh saivi akienda tena kwa mganga huyohuyo kumwambia afanye mautundu amtoe mwanetu agustino?

Ila jooohs hili wazo akikumbuka yale mawe yaliyokuwa yanaongezwa lazima aseme tuende na mtu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Msimuliaji Jooohs akiwa shule boarding alipata rafiki aitwaye Augustino ambaye pia alisoma naye shule moja, Augustino alikuwa Mwanafunzi wa day

Katika urafiki wao Augustino alionesha kutaka kuwa Tajiri kwa udi na uvumba, hali iliyosababisha ajiingize kwenye biashara ya bangi na baadae kwenda kwa mganga ili apate utajiri, katika hizi harakati Augustino alimshirikisha Jooohs

Walienda kwa mganga, wakafanyiwa dawa lakini wakaja kugundua kuwa ili pesa zianze kumiminika inabidi watoe kafara wazazi wao, hivyo jamaa wakaghairi. Kumbuka wakati huo wote walikuwa wanaendelea kuuza ganja.

Kwenye gheto la Augustino ambapo alipanga, palikuwa na matukio mfano mara kwa mara Jooohs alikuwa anakuta damu magetoni na kuna siku walikuta viganja vya mikono vya watoto wachanga.

Majirani wa mama mwenye nyumba wote walijua kuhusu uchawi wa huyu mama, na walimchoka mpaka walipokuja kumchomea moto nyumba yake lakini kipindi hicho akina Augustino walishahamia nyumba nyingine kumkimbia mother mchawi

Katika maisha yao ya utafutaji kupitia ndumu walikuwa na upinzani na ma pusher wengine ambao ni wazawa wa pale, hawa jamaa walishamuonya Augustino, lakini Augustino aliendelea na biashara ya ndumu.

Kama kawaida Serikali iliendeleza kubana mianya ya biashara ya bangi, hivyo ma dealers waligundua mbinu ya kusafirisha bangi ndani ya madumu. Biashara iliendelea kwa muda, siku moja katika harakati za kupokea mzigo Augustino alikamatwa na polisi akiwa na madumu yake akapelekwa mahakani akahukumiwa miaka 30 jela na kwa sasa yupo gereza la Butimba.

Augustino ambaye ameshatumikia kifungo miaka 5 na amebakiza miaka 15 (miaka ya jela) , alitembelewa na Jooohs siku moja, Jooohs ambaye kwa sasa ni graduate alikwenda kumsalimia Augustino, na Augustino alimsisitiza Jooohs aendelee kukomaa mpaka atusue maisha.

Tayari summary mkuu, usije sema nikusomee [emoji23][emoji23], acha uvivu
Ambaye anaweza kunipa kifupisho cha hili swala anionee imani anipe. Naona mnauliza habari za Augustine kua gerezani lakini mi nipo page ya 26 na zipo zaidi ya 50.

msaada wakuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mbona huku uliandika jamaa alifungwa kwa kubaka,afu huku amefungwa kwa bangi au ni watu wawili tofauti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa naona ni mtunzi wa stori make kuna nyuzi zake nyingi sanaaa
Mkuu unajua unachekesha sana

Wewe umejiunga jamii forum Jana una nyuzi tano

Mimi huu mwaka wa 4 na nyuzi tano

Kati yangu na yako nani ananyuzi nyingi??

Unajua kabla hujahukumu mtu jiangalie wewe kwanza huko salama

Mimi sii mwandishi wa story za udaku ningekuwa nataka ningekuwa kila siku nafyatua uzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…