Baada ya Ole Nasha kufariki ni wakati wa Mkataba wa bandari ya Bagamoyo kuwa wazi

Mkuu Kamundu , hili la uadilifu wa Comred Ole Nasha, nakuunga mkono hata mimi nimezungumzia hapa Tribute to William Ole Nasha: Alikuwa Miongoni Mwa Viongozi Wachache Bonafide Genuine Wazalendo wa Kweli waTaifa Hili. RIP Comred William Ole Nasha!
Lakini naomba usilete any conspiracy theories zozote kwenye kifo chake, kifo ni kazi ya Mungu.

Pili ujenzi wa bandari ya Bagamoyo, ilikuwa ndio iwe a feed port ya mzigo wa kushibisha SGR. Bandari ya Dar es Salaam hata iki operates kwenye full capacity, haiwezi kushibisha SGR ikajiendesha kwa faida. Reli ya SGR: Je, Tujifunze kwa wenzetu Kenya kuepusha SGR yetu kuwa ‘A White Elephant’? Wenzetu yameshawakuta...

Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo, inakuwa ni a free port, zile yards za magari Japan, Dubai na Singapore, zinahamia Bagamoyo, hivyo nchi zote za Africa South of Sahara, wanakuja kununua mahitaji yao yote Tanzania.

Na kwa vile tunafanya miradi kibao mikubwa ya kimkakati, sijaona ukiuliza mkataba wa SGR, Stigler, Ununuzi wa Ndege, Ujenzi wa Flyovers etc, why utake mkataba wa Bagamoyo?. Mikataba yote ina confidentiality clause. Kwani umeona mkataba wa Barrick?. Why so much noise on Bagamoyo Port?.
P
P
 
Hii bandari lazima Ile vichwa vya watu tunadubiri upuuzi wa hawa kina mangungo wa msovero .kwa kweli wazarendo tuliobaki tutapambana. Yaani huyu JK sijui anafanya nini kwetu
Rais mstaafu JK anastahili heshima yake, tumuache ale pension yake kwa amani, kama una hoja kuhusu matatizo ya bandari ya Bagomoyo, itoe na hiyo ndiyo ioneshe JK ana makosa.
Siyo wewe umshambulie bila kutuelewesha.
 
LOoooh, hata sijui kama wewe ndiye hasa mwasisi na mwandishi wa mada hii; na kama ni kweli, basi huenda Tanzania tumekwishaingiliwa hadi mvunguni.
Hii itakuwa ni hatari kubwa sana kwa taifa hili.

Kuna kitu ambacho waTanzania wengi inapasa wakijue na wasikichanganye kabisa katika kujadili habari za uwepo wa Bandari ya Bagamoyo au nyingine yoyote mpya.
Mkanganyiko uliopo ni huu wa kuihusisha Bagamoyo na waChina, tukiondoa mkanganyiko huo nadhani wengi watakubali kwamba Bandari ya Bagamoyo au Mwambani zilizobora kabisa ni muhimu kwa taifa letu. Tunahitaji uwepo wa bandari kubwa yenye uwezo zaidi ya ule unaopatikana kwa bandari zilizopo sasa. Hili ndio takwa.
Tatizo ni mpango upi unaotakiwa tuutumie ili kupata hiyo badari. Huu wa wachina, au watu wengine wowote wenye kuhusisha kutukamua ni tatizo, bila kujali ni nani anahusika.

Tunaweza kujenga bandari mpya na kubwa taratibu kwa uwezo wetu wa ndani; mfano ni hiyo Lamu, mbona bandari imejengwa na inaendelea kujengwa kwa hatua. Maswala ya kukabidhi miradi kama hii kwa watu/makampuni/nchi zingine yana umuhimu gani kwa ufanisi wa nchi yetu?
Kwa nini ushiriki wetu kama nchi kwenye miradi ya aina hii iwe ni nongwa, mbona bomba la mafuta tunashiriki kama nchi!

Kwa hiyo, niseme tu kwa ufupi. Kuna mambo ninakubaliana nawe kuhusu huu mradi wa bandari ya Bagamoyo.
1. Ninakubaliana nawe kwamba kuna kundi la watu wanaousukuma mradi huu kwa manufaa yao binafsi zaidi kuliko manufaa ya nchi yetu, na kundi hili linaonekana wazi kuwa hatari sana kwa nchi yetu. Lisipodhibitiwa haraka tutakuwa matatani.
2. Ninakubaliana nawe kwamba hatuhitaji bandari na viwanda kushusha na kupakia bidhaa toka nje, huku tukifaidika kidogo na uwekezaji wa namna hiyo.

Nisiyokubaliana nawe ni
1. Uhitaji wa bandari kubwa yenye uwezo mkubwa kuliko unaopatikana kutokana na zilizopo sasa hivi. Ni muhimu sana tuwe na bandari ya kisasa kabisa na kubwa kuhimiri ongezeko kubwa la biashara katika ukanda huu miaka michache iinayofuata.
2. Wachina, kwani wana kizuizi gani cha kupeleka miradi yao Lamu, ambako najua wakitaka ni haraka sana wanakabidhiwa kila kitu.

Hizi 'Consipiracy theories' hizi zinazoibuka kila mahali wakati huu, ni mwanzo tu wa makubwa yatakayofuata baada ya hapa.
 
Tusisahau watanzania ni karibia mil 60. Tuache mambo ya kukopa au kuanzisha miradi ya kuneemesha watu wachache tu.
Hivi hatukomi kuanzisha kashfa zisizoisha?

Wanaofanya hivyo wanajulikana. Ukiandika kwa umoja kama wote tunahusika hututendei haki. Ni viongozi wa serikali ya CCM ndio mambo zao miaka yote katika makundi na mitandao yao. Na kwa vile wameshajihakikishia ukiritimba wa mamlaka ya kuitawala Tanzania “milele” kamwe hawatabadilika.

Hakuna tishio la kuwaondoa madarakani kiasi cha kuwatia uoga wajinyime ulaji wa wazi kabisa. Hawahitaji kura za wananchi kushika madaraka. Kila dili kubwa: EPA, ndege ya Rais, rada, Tegeta Escrow, n.k. kuna mkono wa Ikulu. Hakuna Mtanzania wa kuwarudi. Wanaojaribu wanakuwa neutralized kwa namna tofauti tofauti.

Bila demokrasia ya kweli ufisadi wa viongozi utaendelea kuwa mtindo wa maisha nchini hadi taifa lisambaratike au hadi ule mwisho. Itabidi tuzoee kuishi na ufisadi kama corona au ukimwi.
 
Mkataba wa Bandari ulisainiwa wa kwanza. Huu ndio tuujadili kwa sasa. Pia hakuna mchina kwenye ununuzi wa ndege. Tupo wenyewe. Tunamudu.
 
Bandari ya Bagamoyo haina maslahi kwa Taifa. Ni shinikizo la Uchina. Ni mtindo wa ukoloni mamboleo wa Uchina. Tupanue Bandari zetu 3. DSM, Mtwara na Tanga.
Bandari ya Bagamoyo haina Maslahi kwa Taifa.
 

Shida ni kuamini kwamba bila chama flani nchi haiendelei
 
What a stroke of a genius !!!
 
Hiyo inakuwa Bandari ya Uchina. Nil sawa tumemuuzia Mchina ardhi ya kujenga bandari wakati sisi tuna Bandari zetu.
Halafu tumieni akili na kuona kisichoonekana kwa macho ya kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…