Baada ya Rais Samia kufungua soko la nyama falme za Kiarabu. Je, wanaopuuza zoezi la uwekaji hereni mifugo ni wasaliti wa Rais aliyewateua?

Baada ya Rais Samia kufungua soko la nyama falme za Kiarabu. Je, wanaopuuza zoezi la uwekaji hereni mifugo ni wasaliti wa Rais aliyewateua?

IMG_0288.jpg
 
Hadi uanze kupeleka live stock au meat, M.E bado sana. Ndio maana wanakuja wenyewe kutengeneza mazingira ya kuweza kusafirisha hai au nyama.

Sio kila mtu anachinja, kupakia nyuma la pick-up lake na kupeleka sokoni nyama; kama tulivyozoea sisi.

Kwa wenzetu ukisha chinja kuna mazingira ya ku-maintain hiyo nyama at certain temperature ibaki fresh (sio kugandisha) na una masaa yasiyozidi 48 baada ya kuchinja mzigo uwe sokoni kwao.

Same thing kwenye matunda na mbogamboga zinaviwango vyake vya freshness, jumlisha na viwango vya quality ya mifugo na mboga-mboga; ndio maana wawekezaji wanakuja kutengeneza hayo mazingira ya kuweza kupeleka hizo biashara kwenye nchi zao kabla ya kuanza ku-import huko.

Kama lengo ni kusafirisha mifugo ungeanza kufuga kisasa wanone, elewa viwango vyao kujipa advantage badala ya kudhani kesho tu waarabu wanakuja kununua mifugo ovyo ovyo kama ulivyozoea kupeleka mnadani.
 
kwanza mtoa mada ni mjinga asiejua falme za kiarabu . kwa ufupi ukiwa falme za kiarabu kuna mifungo kama mbuzi kondoo na ngombe kuku ni wengi sana inategemea na weww unataka mbuzi au kondoo kutoka nchi gani, mbuzi huko au kondoo ni rahisi kuliko tanzania nimeishi huko miaka 30 ninaijua vizuri. kila nchi duniani inaleta mifugo na matunda wanashindana. falme za kiarabu haitaji saana tanzania kwa mifugo yake na matunda yake wale wana kilakitu mungu kawajaalia kuna matunda huko yapo tanzania hakuna wale wanaishi pepo ya ulimwenguni
Mkuu unataka kutuambia nini umesoma vizuri umelielewa babdiko?
 
binafsi nasikitika sana, hilo soko huwa lipo miaka mingi sana, lakini je? hawa wabongo wanaweza kuingia kwenye hii biashara au iko monopolized na watu kadhaa matycoon wanaofanya umafia na kuhakikisha wengine hawatoboi.

Inawezekana viongozi baadhi wanajitahidi kufungua njia kwa watanzania wengi kunufaika lakini wanasahau kwenye ground mambo hawajaweka sawa ili watanzania wasipate vikwazo.
Mbona unakata tamaa mapema?
 
Ukweli ni kwamba wateule wengi wa Magufuli na baadhi wa yeye wanamsaliti sana huyu Mama huu ndio ukweli mchungu,

Hata wakimbiza mwenge nao mbona hawahamasishi hii sensa ya mifugo?
 
Hadi uanze kupeleka live stock au meat, M.E bado sana. Ndio maana wanakuja wenyewe kutengeneza mazingira ya kuweza kusafirisha hai au nyama.

Sio kila mtu anachinja, kupakia nyuma la pick-up lake na kupeleka sokoni nyama; kama tulivyozoea sisi.

Kwa wenzetu ukisha chinja kuna mazingira ya ku-maintain hiyo nyama at certain temperature ibaki fresh (sio kugandisha) na una masaa yasiyozidi 48 baada ya kuchinja mzigo uwe sokoni kwao.

Same thing kwenye matunda na mbogamboga zinaviwango vyake vya freshness, jumlisha na viwango vya quality ya mifugo na mboga-mboga; ndio maana wawekezaji wanakuja kutengeneza hayo mazingira ya kuweza kupeleka hizo biashara kwenye nchi zao kabla ya kuanza ku-import huko.

Kama lengo ni kusafirisha mifugo ungeanza kufuga kisasa wanone, elewa viwango vyao kujipa advantage badala ya kudhani kesho tu waarabu wanakuja kununua mifugo ovyo ovyo kama ulivyozoea kupeleka mnadani.
Unamawazo mazuri ila usiasa mwingi sana unaingiza,
 
Hii biashara ya UAE ni kubwa sana, kama kuna mtu bado hajaiona basi hafai kuwa hapo alipo,

Hongera Rais Samia,
Hongera Waziri,
Hongera wafugaji
Ndio mjiandae bei kupanda.
Km hamjaishia kula kwato na ngozi.
 
Tokea lini Mfugo ukauwekea Mfugo mwingine Hereni? Samia anahangaika tu aweke Watu makini.
tocry.png
 
Nawasalimu kwa Jina la JMT,

Tanzania kuna mambo ya kubishaniwa ila sio uhodari,Umakini na Uchapakazi wa Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ,

Mtakumbuka hivi majuzi Rais Samia alifanya ziara katika nchi za falme ya kiarabu ( UAE) akihangaika kuifungua Tanzania ili kuwaletea Watanzania anawaongoza mendeleo endelevu,

Moja ya jambo kubwa la mafanikio ya ziara hiyo ni kufanikiwa kuzishawishi tena nchi hizo za kiarabu kununua ngo'mbe mbuzi na kondoo toka Tanzania,

Mtakumbuka, ni karibu nusu karne nzima waarabu waligoma kula nyama toka Tanzania wakihitaji wauziwe viumbe hao wakiwa hai ili kwa imani yao wao wenyewe wawapeleke "Kibra " yaani wawachinje wao,

Tanzania wakati wote imeshindwa kutimiza takwa la mifugo yake kuwa na utambuzi,unaotambulika kitaifa na kimataifa, yaani kuwa na hereni zenye "Bar code " kama ilivyo kwa wenzetu Uganda,

Tanzania kwa sasa inakadiriwa kuwa na mifugo inayofikia milioni 50,kama kadirio la chini na iko nafasi ya pili baada ya Ethiopia Africa,

Endapo Tanzania itafanikiwa kusajili walau 70% tu ya mifugo yake basi mifugo hii itachangia kwenye pato la Taifa kwa zaidi ya 20%, karibu sawa na sekta ya madini,

Kama kunajambo Rais Samia atapiga bao marais wote waliomtangulia basi ni hili la 'Livestock identification ' kwani bei ya ngo'mbe itapaa juu mno, wafugaji wanakwenda kuwa billioners,

Mfugo wenye " Id " anakuwa tayari ni "International based " anaweza kuuzwa kokote duniani, tofauti na ilivyo sasa wanaishia tu pale Pungu au kale kamnada kakwampalange,

Fankly, Sijawahi kmpongeza Ndg yangu Mhe Mashimba Ndaki waziri wa Mifugo na Uvuvi kwenye hili wacha niseme ameupiga mwingi kwelikweli,na anastahili heshima sana pamoja na team yake yote,

Kinachonisikitisha zaidi ni kuona baadhi ya wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi kutolipa uzito unaostahili zoezi hili litakalo maliza migogoro ya muda mwingi kati ya wakulima na wafugaji na kuwaacha wafugaji wakiwa matajiri wa kutupwa,

Napendekeza uwekaji wa hereni uwe ndio kipimo cha utendaji wa viongozi hao,

Kazi na iendelee,#Samia5Tena

View attachment 2279979
Huyu ni ng'ombe mwenye hereni huko Mbarali Mbeya,

Wacha nimpongezi Mhe RC wa Mbeya, Mhe DC wa Mbarali na Mhe Mkurugenzi wa Mbarali kwa kumsaidia vema kazi Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan,
kazi nzuri sana,
 
Back
Top Bottom