Maswa Yetu
JF-Expert Member
- Mar 18, 2023
- 1,398
- 2,619
Kwa tathimini iliyofanyika ni kwamba Rais Samia hawezi tena kuongoza nchi hii ya Tanzania hivyo unahitajika mbadala wa haraka ambao ni Luhaga Mpina
Chini ya utawala wa Rais Samia ni salama zaidi ukiwa fisadi kuliko ukipinga ufisadi! Ndiyo maana Askofu Gwajima amefungiwa kwa kukemea utekaji.
Wabunge 28 waliokuwa vinara wa kuihoji serikali na kupinga ufisadi bungeni wote wameondolewa bungeni kwa kukatwa majina yao!
Kwa hiyo Rais anataka serikali ya kutohoji iliyojaa ndugu na marafiki ambao anawahamasisha wale kutokana na urefu wa kamba zao.
Wote waliohoji mkataba wa hovyo wa DP World na mikataba mingine ya kinyonyaji kwa taifa wote wanawekewa zengwe na kukatwa majina yao.
Hivyo basi kutokana na ulegelege huu wa Rais Samia hawezi kupewa miaka mingine 5 hivyo kanda ya ziwa tutamchagua Luhaga Mpina ili atusaidie kukata kamba za mafisadi yaliyotengenezwa na kukumbatiwa na Rais Samia