Baada ya TAKUKURU kusema itawahoji TFF kuhusu Bilioni 1 ya AFCON ya vijana iliyotolewa na Rais Magufuli, TFF yasema haijawahi kupokea fedha hizo

Baada ya TAKUKURU kusema itawahoji TFF kuhusu Bilioni 1 ya AFCON ya vijana iliyotolewa na Rais Magufuli, TFF yasema haijawahi kupokea fedha hizo

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetolea ufafanuzi kuhus Tsh. Bilioni 1 zilizotolewa na Rais Magufuli kwa ajili ya fainali za AFCON kwa Vijana chini ya umri wa miaka 17 zilizofanyika mwaka 2019

Katibu Mkuu wa TFF, Kidai Wilfred amesema fedha hizo hazikuingia kwenye akaunti za fedha za TFF na wala haihusiki kwenye matumizi yake. Pia, amesema TFF haijapokea fedha yoyote wakati wa fainali hizo zilizochezwa Jijini Dar

Awali, taarifa zimeeleza kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imejiandaa kuwahoji baadhi ya Maafisa wa TFF kwa matumizi mabaya ya fedha hizo zilizotolewa na Rais Magufuli

Pia soma > TAKUKURU: Kwenye TFF kuna hela zimetumika vibaya

EYEAldyWkAAvZcf.jpg
 
Shirikisho la soka nchini TFF limekanusha kutafuna Bilioni 1 za Magufuli alizotoa kwa ajili ya Maandalizi ya Serengeti boys wakati ikijiandaa kushiriki michuano ya Afcon 2019.TFF inasema pesa hizo haziingia kwenye account Yao.
Awali mapema asubuhi Takukuru alisema imeanza Maandalizi ya kuwahoji maofisi wa TFF kufuatia utafunwaji ya pesa hiyo Bilioni 1 aliotoa Rais Pombe Magufuli
 
sasa nani aliyezichukua na kuzifanyia matumizi hizi hela!...watupe ufafanuzi na siyo kukana wakati wao ndiyo wasimamizi na waongozaji wa football hapa nchini...
 
TFF wanadai hawana taarifa na hizo hela...kwamba hata kwenye akaunti zao hakuna. Takukuru wanawahoji, TFF ina maana wana uhakika fedha zilikwenda kwenye shirikisho hilo. Ngoja tuone mwisho wake.
 
sasa nani aliyezichukua na kuzifanyia matumizi hizi hela!...watupe ufafanuzi na siyo kukana wakati wao ndiyo wasimamizi na waongozaji wa football hapa nchini...

Sent using Jamii Forums mobile app
Karia kawazunguka wenzie kama kawaida kafanyaa mbinu za kimedani za kiuharamia

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh mie naamini mpk Taasisi kubwa kama TFF kutoa tamko hili na kwa utawala huu kuna kitu kinaendelea hapo katikati
Hizo fedha ziiingia kwa Mkuu wa Mkoani kwa za chini chini
Kuna zile kamati kamati zao za ushindi zile ,zitafutwe ziulizwe
 
Unakula pesa iliyotolewa kwa jina la Jiwe? Hahaaaa ni sawa na kutoboa meli halafu upo ndani.
 
Nina uhakika hilo jibu lao ni la kweli, hawawezi kujibu hivyo kama ingekuwa hela imeingia kwao.

Na PCCB wangekuwa na uhakika na kazi yao, wangechunguza kwanza ndo waje na allegations. Ikiwa ni pamoja na kuwakamata wahusika na si kuwaambia eti warudishe.
 
Kwa style hii sijui ni wangapi hua wana ahidiwa mamilioni kwny mikutano ya hadhara na hawapewi mpunga huo.
 
Pombe anataka ligi zichezwe ili watu waambukizane kwenye vibanda umiza licha ya uwepo wa Corona. Anataka watu wasahau kuwa Kuna Covid-19 aendelee kupokea kodi!

TFF walikwepa kwa kusema kuwa hawana fedha za kuzipa timu ili zijigharamie kwani mpira unategemea viingilio vya mashabiki. Of course FIFA wameshauri kusimamiwa ligi kwa kusema maisha na afya kwanza.

Kinachofuata ni TATAKURU kuchunguza ,kwa ukaidi' wa TFF
 
Kuna kitu nyuma ya hili swala, haiwezekani iwe upigaji halafu mtu uwaambie watu eti walete hiyo hela.
 
Hahaha kwa hiyo mjomba aliwaahidi bilioni moja halafu hakuwapa.
 
Back
Top Bottom