Baada ya TAKUKURU kusema itawahoji TFF kuhusu Bilioni 1 ya AFCON ya vijana iliyotolewa na Rais Magufuli, TFF yasema haijawahi kupokea fedha hizo

Baada ya TAKUKURU kusema itawahoji TFF kuhusu Bilioni 1 ya AFCON ya vijana iliyotolewa na Rais Magufuli, TFF yasema haijawahi kupokea fedha hizo

Jana mkuu wa takukuru Kaongea na katibu wa huko TFF katoka kujibu sasa hii mikanganyiko ni takukuru kukurupuka au Magu hakutoa hela yoyote maana naona TFF kama wana hoja
Hoja ya tff ijibiwe na serikali kwa uwazi
 
TFF wanakanusha sasa sijui serikali haikutoa pesa kweli?
Screenshot_20200516-101108.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tff toka aondoke Mzee Tenga wamejaa wahuni tu ,imerudi enzi za Fat

Lazima warudishe pesa walizotafuna

Haiwezekani Mkuu wa Nchi atoe pesa tff wazipige
 
TFF==Tafuna Fuja Filisi
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetolea ufafanuzi kuhus Tsh. Bilioni 1 zilizotolewa na Rais Magufuli kwa ajili ya fainali za AFCON kwa Vijana chini ya umri wa miaka 17 zilizofanyika mwaka 2019

Katibu Mkuu wa TFF, Kidai Wilfred amesema fedha hizo hazikuingia kwenye akaunti za fedha za TFF na wala haihusiki kwenye matumizi yake. Pia, amesema TFF haijapokea fedha yoyote wakati wa fainali hizo zilizochezwa Jijini Dar

Awali, taarifa zimeeleza kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imejiandaa kuwahoji baadhi ya Maafisa wa TFF kwa matumizi mabaya ya fedha hizo zilizotolewa na Rais Magufuli


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haaa kwanini hili limeibuka baada ya fifa kugawa mgao kwa TFF ??? Au serikali inataka kuwany'ang'anya hilo fungu

California love
 
Back
Top Bottom