Baada ya TAKUKURU kusema itawahoji TFF kuhusu Bilioni 1 ya AFCON ya vijana iliyotolewa na Rais Magufuli, TFF yasema haijawahi kupokea fedha hizo

Baada ya TAKUKURU kusema itawahoji TFF kuhusu Bilioni 1 ya AFCON ya vijana iliyotolewa na Rais Magufuli, TFF yasema haijawahi kupokea fedha hizo

Mkuu wa Nchi inawezekana alitoa ila zikaishia mikono ya wajanja au inawezekana pia alijimwambafy lakini hakutoa hata dala.
Tff toka aondoke Mzee Tenga wamejaa wahuni tu ,imerudi enzi za Fat

Lazima warudishe pesa walizotafuna

Haiwezekani Mkuu wa Nchi atoe pesa tff wazipige

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetolea ufafanuzi kuhus Tsh. Bilioni 1 zilizotolewa na Rais Magufuli kwa ajili ya fainali za AFCON kwa Vijana chini ya umri wa miaka 17 zilizofanyika mwaka 2019

Katibu Mkuu wa TFF, Kidai Wilfred amesema fedha hizo hazikuingia kwenye akaunti za fedha za TFF na wala haihusiki kwenye matumizi yake. Pia, amesema TFF haijapokea fedha yoyote wakati wa fainali hizo zilizochezwa Jijini Dar

Awali, taarifa zimeeleza kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imejiandaa kuwahoji baadhi ya Maafisa wa TFF kwa matumizi mabaya ya fedha hizo zilizotolewa na Rais Magufuli

Kwan nani aliyekabidhiwa hizo pesa akaziweke kwenye hiyo account ya TFF

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa anataka kutuambia kuwa muheshimiwa aliahidi alafu hakutoa? Kwamba muheshimiwa alichukua tu ujiko mbele ya kamera alafu akapiga kimya, mbona anamkosea adabu mkuu namna hii?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuwa na maana hiyo mkuu, anakiri ahadi ilitolewa ila hajasema hela haijatolewa alichosema haijafika kwenye acc. ya TFF. Inawezekana rais katoa ila wahuni wamezila, cha muhimu takukuru waanze kutrace hizo pesa wajuwe zimeishia wapi na waje majibu sahihi.
 
Tff toka aondoke Mzee Tenga wamejaa wahuni tu ,imerudi enzi za Fat

Lazima warudishe pesa walizotafuna

Haiwezekani Mkuu wa Nchi atoe pesa tff wazipige
Inasemekana hiyo pesa kuna jamaa kaenda kuilia pasaka na atamalizia na Eid kabisa huko kijijini kwao, haikufika tff mkuu.
 
sasa nani aliyezichukua na kuzifanyia matumizi hizi hela!...watupe ufafanuzi na siyo kukana wakati wao ndiyo wasimamizi na waongozaji wa football hapa nchini...

Hii hoja umeilekeza TFF?

Sasa unataka wakupe ufafanuzi gani zaidi ya huu kuwa hawajawahi kupokea fedha hizo kwenye Akaunti zao?

Huwezi kutolea ufafanuzi wa matumizi ya fedha ambazo uliyempa hajazipata zaidi ya kukuambia, "sijapokea fedha hizo"

Wao serikali au Rais Magufuli aseme baada ya kuzitoa hizo fedha, alimpa nani badala ya TFF maana aliowakusudia kuwapa wanasema hawajawahi kupokea!!
 
Nina uhakika hilo jibu lao ni la kweli, hawawezi kujibu hivyo kama ingekuwa hela imeingia kwao.

Na PCCB wangekuwa na uhakika na kazi yao, wangechunguza kwanza ndo waje na allegations. Ikiwa ni pamoja na kuwakamata wahusika na si kuwaambia eti warudishe.
Naona Kama pccb Kama washawahukumu hivi
 
Back
Top Bottom