Baada ya TPA kutangaza tenda kuhusu uwekezaji Terminal 2, Bado mnaamini Bandari zote zimeuzwa?

Baada ya TPA kutangaza tenda kuhusu uwekezaji Terminal 2, Bado mnaamini Bandari zote zimeuzwa?

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Kwa wachache tuliobarikiwa kuielewa vizuri nchi hii na jamii yake pamoja na siasa zake tunaposimamia jambo kwa maslahi ya taifa naomba tuheshimiwe na tueleweke vizuri.

Kwa miezi 2 sasa kuna kikundi cha wanasiasa na viongozi wa dini, kwa maslahi binafsi na kutumiwa na watu ambao kila siku wamekuwa wakineemeka kwa michezo yao michafu wanayoifanya kwenye njia zetu kuu za uchumi walianzisha maneno kuwa Bandari zote za Maziwa na Bahari ikiwemo Bandari ya Dar es Salaam zimeuzwa kwa waarabu.

Kikundi hichi cha watu kilisambaza maneno haya nchi nzima huku kikisema kuwa Bunge letu limeshurutishwa na Rais Samia kuuza Bandari zetu na hivyo linauza nchi.

Kwa wachache tunaowajua vizuri tulisema kuwa haya maneno ya hawa watu hayana ukweli wowote ule ila ni hila za watu ambao wamekuwa wakineemeka kwa kuifisadi nchi yetu kupitia Bandari ambao wanatunga maneno ili ku sabotage nia nzuri ya Rais katika kuleta mapinduzi ya kiuchumi kupitia njia zetu kuu za kiuchumi ikiwemo Bandari.

Tuliosimamia ukweli huu na kukataa upotoshaji wa kundi hili la wanasiasa na viongozi wachache wa kidini tuliitwa majina yote eti tumehongwa, mara sisi ni chawa wa Rais Samia.

Kuna mzee mmoja aliwahi kuniambia kuwa, ukweli una tabia moja, unatembea taratibu sana ila uzuri wake ni lazima tu ufike mahali pake.

Baada ya Mamlaka ya Bandari kutoa tangazo la kukaribisha maombi ya uwekezaji katika Terminal 2 ya Bandari yetu ya Dar es Salaam sasa nimeamini rasmi maneno ya yule mzee.

Kilichonifurahisha ni kwamba, baada ya tangazo hili la Bandari, Sijasikia maneno yale ya wale wanasiasa pamoja na wale viongozi wa dini hasa TEC kuwa Rais kauza Bandari ya Dar es Salaam au Bandari zote kwa waarabu!

Wale watu waliokuwa wanasema kuwa Bandari zetu zimeuzwa wameufyata kimyaaaaaa na siwasikii wakisema neno lolote lile zaidi ya kuhamisha magoli saivi wameanza kuzungumzia kampuni ya Adani.

Wale waliokuwa wanasema tumeondoa our National Sovereignty kwa kuwapa Bandari yetu Dubai ndo siwasikii kabisa sasa sijui wamelala usingizi wa pono hawajaona hili tangazo la TPA?

Napenda kumaliza kwa kusema
Tanzania kuna kundi maslahi ambalo limekuwa likinufaika kwa ujinga wa Watanzania. Kundi hili ni zito na lina wanasiasa na watu wa dini pia.

Endapo msiposimama na Serikali kuiunga mkono katika kuleta mapinduzi ya kweli ya kiuchumi, nchi yetu itakuwa maskini hadi ukamilifu wa dahali.

Tumsifu Yesu Kristo!

Nakala kwa
The Boss FaizaFoxy GUSSIE
 
Screenshot_2023-09-01-08-56-57-38_f541918c7893c52dbd1ee5d319333948.jpg
Screenshot_2023-09-01-08-58-19-47_f541918c7893c52dbd1ee5d319333948.jpg
 
Fedheha ni kwamba makanisani waraka ulishapelekwa na hivi sasa tunaishi na gharama za kuitengeneza hiyo chuki kati ya serikali na ukatoliki.

Tulilishwa matango pori kwamba mwarabu anataka kuinunua nchi hivyo ule waraka ulikuwa na ujumbe wa siri wa kukataa kuiuza Tanzania kwa mwarabu haswa muislam.

Leo hii tangazo la TPA linamtaka mwekezaji mwenye uwezo ajitokeze na vigezo vyake vitazamwe kama vinakidhi mahitaji ya uendeshaji wa bandari kisasa, tangazo linasema hata wale wazalendo wenye uwezo wa kuendesha bandari kisasa na wao wanaalikwa pia.

Maana yake ni kwamba hata sisi walei wa kawaida tunaosali makanisani tunaalikwa kufanya biashara na serikali yetu kama vigezo vyetu vinatimia!, hii ni aibu kubwa sana ambayo maaskofu pengine kwa kutokujua walichokifanya waliamua kuitafuta wao wenyewe!.
 
DP ilishindanishwa na nani? Na kimsingi tunapinga aina ya mkataba wa kishenzi.

Hii spinning yenu imefeli, tunalikumbusha kanisa katoliki kuwakumbusha maparoko wote waraka uendelee kusomwa kwenye parokia zote kwa wiki tano mfululizo.
 
Back
Top Bottom