Baada ya TPA kutangaza tenda kuhusu uwekezaji Terminal 2, Bado mnaamini Bandari zote zimeuzwa?

Baada ya TPA kutangaza tenda kuhusu uwekezaji Terminal 2, Bado mnaamini Bandari zote zimeuzwa?

Dp world nawatakiwa wafaamishwe kabla tenda kutangazwa au hujakiona iki? Hujasoma mkataba Nini?
Nimekuuliza kifungu gani, hujakiweka kifungu hapa tukichambue.

Wote tunaweza kuwa tumesoma kifungu kimoja, lakini tukawa na uelewa tofauti.
 
Utaratibu unahitaji mwekezaji apatikane baada ya ushindani, hizi sifa ulizomwagia bado hazitoshi kuhalalisha ukiukwaji wa taratibu na sheria.
Waliompa hiyo nafasi walijiridhisha juu ya uwezo wake, kampuni inayoendesha bandari za UK na China huwezi kuishindanisha na makampuni mengi yaliyopo duniani kwenye sekta husika.
 
Ko mkataba umefutwa au?😂😂😂
Nyie nikwenda polepole mnataka kupindua meza kibwege
Haujafutwa, hauwezi kufutwa kirahisi tu wakati ulipitishwa bungeni na mahakama imesaidia kuipa uhalali hiyo DP World baada ya hukumu ya kina Mwabukusi kuwekwa hadharani.
 
Kwa wachache tuliobarikiwa kuielewa vizuri nchi hii na jamii yake pamoja na siasa zake tunaposimamia jambo kwa maslahi ya taifa naomba tuheshimiwe na tueleweke vizuri.

Kwa miezi 2 sasa kuna kikundi cha wanasiasa na viongozi wa dini, kwa maslahi binafsi na kutumiwa na watu ambao kila siku wamekuwa wakineemeka kwa michezo yao michafu wanayoifanya kwenye njia zetu kuu za uchumi walianzisha maneno kuwa Bandari zote za Maziwa na Bahari ikiwemo Bandari ya Dar es Salaam zimeuzwa kwa waarabu.

Kikundi hichi cha watu kilisambaza maneno haya nchi nzima huku kikisema kuwa Bunge letu limeshurutishwa na Rais Samia kuuza Bandari zetu na hivyo linauza nchi.

Kwa wachache tunaowajua vizuri tulisema kuwa haya maneno ya hawa watu hayana ukweli wowote ule ila ni hila za watu ambao wamekuwa wakineemeka kwa kuifisadi nchi yetu kupitia Bandari ambao wanatunga maneno ili ku sabotage nia nzuri ya Rais katika kuleta mapinduzi ya kiuchumi kupitia njia zetu kuu za kiuchumi ikiwemo Bandari.

Tuliosimamia ukweli huu na kukataa upotoshaji wa kundi hili la wanasiasa na viongozi wachache wa kidini tuliitwa majina yote eti tumehongwa, mara sisi ni chawa wa Rais Samia.

Kuna mzee mmoja aliwahi kuniambia kuwa, ukweli una tabia moja, unatembea taratibu sana ila uzuri wake ni lazima tu ufike mahali pake.

Baada ya Mamlaka ya Bandari kutoa tangazo la kukaribisha maombi ya uwekezaji katika Terminal 2 ya Bandari yetu ya Dar es Salaam sasa nimeamini rasmi maneno ya yule mzee.

Kilichonifurahisha ni kwamba, baada ya tangazo hili la Bandari, Sijasikia maneno yale ya wale wanasiasa pamoja na wale viongozi wa dini hasa TEC kuwa Rais kauza Bandari ya Dar es Salaam au Bandari zote kwa waarabu!


Wale watu waliokuwa wanasema kuwa Bandari zetu zimeuzwa wameufyata kimyaaaaaa na siwasikii wakisema neno lolote lile zaidi ya kuhamisha magoli saivi wameanza kuzungumzia kampuni ya Adani.

Wale waliokuwa wanasema tumeondoa our National Sovereignty kwa kuwapa Bandari yetu Dubai ndo siwasikii kabisa sasa sijui wamelala usingizi wa pono hawajaona hili tangazo la TPA?

Napenda kumaliza kwa kusema
Tanzania kuna kundi maslahi ambalo limekuwa likinufaika kwa ujinga wa Watanzania. Kundi hili ni zito na lina wanasiasa na watu wa dini pia.

Endapo msiposimama na Serikali kuiunga mkono katika kuleta mapinduzi ya kweli ya kiuchumi, nchi yetu itakuwa maskini hadi ukamilifu wa dahali.

Tumsifu Yesu Kristo!

Nakala kwa
The Boss FaizaFoxy GUSSIE
Unaibishia hata IGA iliyosainiwa na Prof. Mbarawa?

Vv

Sent from my SM-A045F using JamiiForums mobile app
 
Hapakuwa na sababu ya kumshindanisha na mtu yoyote. Anamiliki meli 400 zinazozunguka dunia nzima, nitajie mshindani wake mwenye wingi wa meli zenye kufikia angalau nusu tu ya hizo 400.

Anaendesha bandari za Uingereza, China na Ulaya nzima, ni mzoefu sana wa end to end logistic chain ambayo kisasa ndio maana mpya ya neno PORT.

Kwa suala la vigezo kawazidi wengi sana. Kanisa limechemka vibaya kuja na waraka wakati walikuwa hawajui kwa kina malengo ya serikali ni yapi.
Kwa hiyo hakutakiwa kushindanishwa kama sheria ya manunuzi ya umma inavyotaka sababu ya meli 400 alizonazo na kazi nyingine azifanya katika nchi zingine?
 
Kwa hiyo hakutakiwa kushindanishwa kama sheria ya manunuzi ya umma inavyotaka sababu ya meli 400 alizonazo na kazi nyingine azifanya katika nchi zingine?
Waziri na wanasheria wa wizara ndio waliompa. Tatizo wengi wetu hatuna ufahamu wa ukubwa wa DP World kidunia.

Na hili ni tatizo letu la ndani ambalo ni dogo sana.
 
Back
Top Bottom