Baada ya TPA kutangaza tenda kuhusu uwekezaji Terminal 2, Bado mnaamini Bandari zote zimeuzwa?

Baada ya TPA kutangaza tenda kuhusu uwekezaji Terminal 2, Bado mnaamini Bandari zote zimeuzwa?

Hapakuwa na sababu ya kumshindanisha na mtu yoyote. Anamiliki meli 400 zinazozunguka dunia nzima, nitajie mshindani wake mwenye wingi wa meli zenye kufikia angalau nusu tu ya hizo 400.

Anaendesha bandari za Uingereza, China na Ulaya nzima, ni mzoefu sana wa end to end logistic chain ambayo kisasa ndio maana mpya ya neno PORT.

Kwa suala la vigezo kawazidi wengi sana. Kanisa limechemka vibaya kuja na waraka wakati walikuwa hawajui kwa kina malengo ya serikali ni yapi.
hapo vipi 👇👇👇👇👇
20230901_133231.png

Anaewaamini wanasiasa bila kuwaza basi huyo anautofauti mdogo na punda.
Tangazo la TPA ndo wote tulitaka ili apatikane Mwekezani kwa njia ya ushindani. Hapa hutasikia kelele tena na evaluation itafanywa na wataalam wabobezi na kwa njia ya uwazi.
 
Hapakuwa na sababu ya kumshindanisha na mtu yoyote. Anamiliki meli 400 zinazozunguka dunia nzima, nitajie mshindani wake mwenye wingi wa meli zenye kufikia angalau nusu tu ya hizo 400.

Anaendesha bandari za Uingereza, China na Ulaya nzima, ni mzoefu sana wa end to end logistic chain ambayo kisasa ndio maana mpya ya neno PORT.

Kwa suala la vigezo kawazidi wengi sana. Kanisa limechemka vibaya kuja na waraka wakati walikuwa hawajui kwa kina malengo ya serikali ni yapi.
Djibouti waislamu 90% lakini wana kesi na DP World
 
Sheria ya maliasili haihusiani na bandari hata siku moja. Hizi harakati zenu zinaambatana na maumivu makubwa ya nafsi.

Bandari ni lango la kuingia ndani ya nchi sawa sawa na uwanja wa ndege, huwezi kuiweka katika kundi la maliasili.

Pale bandaini kilicho katika kundi la maliasili ni maji tu, lakini huwezi kusema makontena yanayopakiwa melini ni sehemu ya maliasili. Huwezi kusema zile machine za kupakia na kupakua makontena eti ni sehemu ya maliasili.

Uelewa wetu ni tatizo kubwa.
Unafahamu maana ya MALIASILI? maliasili ni MALI ASILI. sasa niambie bandari sio MALI ASILI
 
Nina uhakika kuwa walioutoa huo waraka kwa sasa wanaona aibu baada ya tangazo la TPA la jana. Nina uhakika hujui kuwa upo msemo usemao ujanja mwingi mbele ni kiza.
Unajuaje TPA hawakwenda kuomba ruksa ya kutangaza tenda kwa mmiliki wa bandari wa sasa kama IGA inavyojieleza??
 
Mkataba wa IGA haujafutwa, lakini TPA inafanya kazi kwa kufuata waraka wa maaskofu
 
Kwa wachache tuliobarikiwa kuielewa vizuri nchi hii na jamii yake pamoja na siasa zake tunaposimamia jambo kwa maslahi ya taifa naomba tuheshimiwe na tueleweke vizuri.

Kwa miezi 2 sasa kuna kikundi cha wanasiasa na viongozi wa dini, kwa maslahi binafsi na kutumiwa na watu ambao kila siku wamekuwa wakineemeka kwa michezo yao michafu wanayoifanya kwenye njia zetu kuu za uchumi walianzisha maneno kuwa Bandari zote za Maziwa na Bahari ikiwemo Bandari ya Dar es Salaam zimeuzwa kwa waarabu.

Kikundi hichi cha watu kilisambaza maneno haya nchi nzima huku kikisema kuwa Bunge letu limeshurutishwa na Rais Samia kuuza Bandari zetu na hivyo linauza nchi.

Kwa wachache tunaowajua vizuri tulisema kuwa haya maneno ya hawa watu hayana ukweli wowote ule ila ni hila za watu ambao wamekuwa wakineemeka kwa kuifisadi nchi yetu kupitia Bandari ambao wanatunga maneno ili ku sabotage nia nzuri ya Rais katika kuleta mapinduzi ya kiuchumi kupitia njia zetu kuu za kiuchumi ikiwemo Bandari.

Tuliosimamia ukweli huu na kukataa upotoshaji wa kundi hili la wanasiasa na viongozi wachache wa kidini tuliitwa majina yote eti tumehongwa, mara sisi ni chawa wa Rais Samia.

Kuna mzee mmoja aliwahi kuniambia kuwa, ukweli una tabia moja, unatembea taratibu sana ila uzuri wake ni lazima tu ufike mahali pake.

Baada ya Mamlaka ya Bandari kutoa tangazo la kukaribisha maombi ya uwekezaji katika Terminal 2 ya Bandari yetu ya Dar es Salaam sasa nimeamini rasmi maneno ya yule mzee.

Kilichonifurahisha ni kwamba, baada ya tangazo hili la Bandari, Sijasikia maneno yale ya wale wanasiasa pamoja na wale viongozi wa dini hasa TEC kuwa Rais kauza Bandari ya Dar es Salaam au Bandari zote kwa waarabu!

Wale watu waliokuwa wanasema kuwa Bandari zetu zimeuzwa wameufyata kimyaaaaaa na siwasikii wakisema neno lolote lile zaidi ya kuhamisha magoli saivi wameanza kuzungumzia kampuni ya Adani.

Wale waliokuwa wanasema tumeondoa our National Sovereignty kwa kuwapa Bandari yetu Dubai ndo siwasikii kabisa sasa sijui wamelala usingizi wa pono hawajaona hili tangazo la TPA?

Napenda kumaliza kwa kusema
Tanzania kuna kundi maslahi ambalo limekuwa likinufaika kwa ujinga wa Watanzania. Kundi hili ni zito na lina wanasiasa na watu wa dini pia.

Endapo msiposimama na Serikali kuiunga mkono katika kuleta mapinduzi ya kweli ya kiuchumi, nchi yetu itakuwa maskini hadi ukamilifu wa dahali.

Tumsifu Yesu Kristo!

Nakala kwa
The Boss FaizaFoxy GUSSIE
Mnafikili watz wa sasa ni wajana ,kwamba mnaweza wapindua pindua mtakavyo,
 
DP World bye bye kivipi?

Kwa ujinga wenu huo hata hamjui kusoma na kuelewa vitu ndo mana hao wanasiasa na maaskofu wanawapelekesha kama makaratasi
Sasa kama tenda zinatangazwa dp walikua na haja gani kuingia mkataba?😂😂 Jibu kwa hoja
 
Mantiki ya huu uzi ni kuwapa elimu kuwa hakuna bandari iliyouzwa wala kugawiwa.

Makubaliana ya Tanzania na Dubai yanahusu uwekezaji katika Terminal 1 hasa gati 0-7. Hii ni sehemu ndogo sana ya Bandari ya DSM.

Ndo mana TPA amekaribisha uwekezaji mwingine katika Terminal 2

Waliowaambia sijui hakuna national sovereignty sijui bandari za maziwa na bahari zimegawiwa walikuwa wanawaokota na kuwadanganya vilaza nyie alafu mnapayuka tu
Kweny mkataba Ivo vifungu vipi au havipo?
 
Kingereza tatizo, pia na uelewa wa sheria za kimataifa ni tatizo jingine kwa wengi wetu tunaopiga makelele mitandaoni.
Hao wanaotetea wagekua na uelewa mpana wa Sheria zakimataifa it was my hope kwamba tusingetumia asilimia kubwa kuservice deni linalotokana na awards wanzopewa wawekezaji ambao tumevunja nao mikataba au kusaini vitu vya hovyo na Kuja kustuka mwishoni. Au ndege zetu kukamatwa hovyo, viongozi wawe na aibu wanapoabiwa wamekosea
 
Wewe ni mmoja wa wale waliopotoshwa. Mmemuogopa DP World bila ya sababu zozote za msingi. Eneo lake ndani ya JMT ni gati namba tano mpaka namba saba, ambayo ni asilimia nane tu ya eneo lote la bandari la Tanzania.
Umesoma mkataba kweli ?
 
Uingereza walimpa bandari zao zote?

Mkataba waliosaini uingereza ni sawa na huu tuliosaini sisi wa vipengele vy kipumbavu?

Kuwa na umiliki wa meli nyingi duniani ndio uwe mlango wa kusaini mikaytaba ya kisenge?
Uingereza walimpa baadhi ya bandari zao, Antwerp wamempa pia. China yupo pia.

Vipengele vya kipumbavu kama upeo wako ukiwa mdogo lakini kama ni mwelewa huu ni bonge la mkataba, na wengi wetu tunasema kwa kukaririshwa tu kama kasuku, hatuna huo uelewa mpana wa hicho kilichoandikwa.

Meli nyingi duniani zinampa uwezo wa kutawala shorobo mbalimbali za kibiashara, zinampa uwezo wa kufikisha biidha katika nchi mbalimbali na hivyo kuondoa gharama za usafiri zinazochangia ongezeko la ugumu wa maisha.
 
Hao wanaotetea wagekua na uelewa mpana wa Sheria zakimataifa it was my hope kwamba tusingetumia asilimia kubwa kuservice deni linalotokana na awards wanzopewa wawekezaji ambao tumevunja nao mikataba au kusaini vitu vya hovyo na Kuja kustuka mwishoni. Au ndege zetu kukamatwa hovyo, viongozi wawe na aibu wanapoabiwa wamekosea
Tunajifunza kutokana na makosa ya siku za nyuma.
 
Back
Top Bottom